Rais Samia, hayupo mchawi, pafahamu ulipotuchanganya

Rais Samia, hayupo mchawi, pafahamu ulipotuchanganya

Mama tunae mpaka 2025 na ukizingatia Mabeho na wote walio chini yake wamemhakikishia utii ndio kabisaa wale jamaa wa chokochoko inabidi silaha yao kuu iwe ni humu jukwaani na sio kwingineko.

Kuna waliokuwa na majeshi imara kuliko kina Mubarak?

Mama angali na nafasi ya kurekebisha mambo kungali asubuhi.

Hayawi hayawi huwa!
 
Huyu hatoboi

Uzuri ni kuwa anayo nafasi bado ya kuyaruka mengi kati ya haya. Mengine akawavesha Mbagusiro na mengine kuyarekebisha yanayomhusu moja kwa moja na maisha yakaendelea.
 
Kuna waliokuwa ba majeshi imara kuliko kina Mubarak?

Mama angalizo na nafasi ya kurekebisha mambo kungali asubuhi.

Hayawi hayawi huwa!
Sio kwa Tanzania hii ambayo mwasisi ni Nyerere na kule visiwani ni Karume.
 
Sio kwa Tanzania hii ambayo mwasisi ni Nyerere na kule visiwani ni Karume.

Kwani kuna starehe gani kwenye kutawala kidhwalimu? Yaani kutawala huku ukiwapora raia mali au hata na haki zao?

Haya si ndiyo ya kutangulia mbele za haki kibudu bila hata ya kuacha legacy?
 
Kategwa nae kaingiamo mzima mzima!
Maji yashakorogeka!!

IMG_20210704_051559_619.jpg
 
Kwani kuna starehe gani kwenye kutawala kidhwalimu? Yaani kutawala huku ukiwapora raia mali au hata na haki zao?

Haya si ndiyo ya kutangulia mbele za haki kibudu bila hata ya kuacha legacy?
Legacy iachwe mara ngapi?. Mlalamikaji mmoja hawazuii wenye mitazamo chanya elfu moja kuona mengi mazuri yanayofanywa kwa nia ya kuifanya Tanzania ipae kiuchumi.
 
Legacy iachwe mara ngapi?. Mlalamikaji mmoja hawazuii wenye mitazamo chanya elfu moja kuona mengi mazuri yanayofanywa kwa nia ya kuifanya Tanzania ipae kiuchumi.

Haya humo kwenye legacy unazozisema yamo?

1. Kuongezwa kwa tozo mbalimbali na kodi kipindi hiki cha Corona wakati nyie haziwahusu?
2. Kujikongoja kuhusiana na vita vya Corona wakati kwa gharama zetu, nyie mko salama?
3. Kukumbatia ubadhirifu pamoja na kuwapo ripoti za CAG wa hali iko vipi?
4. Kukumbatia ubadhirifu ikiwamo takrima kwa vigogo na wabunge kharam?
5. Kuwadhulumu watu mali na hata haki zao?

Hatuwezi kuweka utaifa mbele dhidi ya mambo fyongo kama hayo?

Sisi ni watanzania kwanza.
 
Sio kwa Tanzania hii ambayo mwasisi ni Nyerere na kule visiwani ni Karume.
Kama wewe ni mtu zamani kidogo. Hebu ifikirie Ivory coast ya wakati wa muasisi wake Felix H Bonnie . Ilikuwa tulivu ya amani na uchumi wa kokoa ya kutilia mfano. Lakini leo hii imekuwa valuvalu kama Tanganyika
 
Matumizi ya Umma WA watanzania hapo ndio tatizo. .unajua maana ya Umma. .Sema wananchama WA Chadema. .kwa sasa tunachojua CCM ndio imeshika hatamu ya uongozi
Umma ni uwingi katika umoja wao . Je Cdm hawana hiyo.

Ccm imeilemaza nchi 60 yrs nawe kwa kukosa exposure unaona ni sawa !!.

Hatamu huku mkiogopa haki (katiba) ?!
 
Matumizi ya Umma WA watanzania hapo ndio tatizo. .unajua maana ya Umma. .Sema wananchama WA Chadema. .kwa sasa tunachojua CCM ndio imeshika hatamu ya uongozi

Kwenye red kauli ni thabiti:

IMG_20210719_094526_263.jpg

Ikimaanisha:

1. Mama alipokamata hatamu za serikali amekuwa akiungwa mkono na takribani watanzania wote.
2. Baada ya kauli yake kuhusiana na katiba mpya na mwendelezo wa matukio yaliyofuatia, kumetokea sintofahamu kubwa. Baadhi ya waliokuwa wakimwuunga mkono hawakubaliani naye tena.

Kutokukubaliana na mtu ni jambo la afya tu. Hakipo kigeni hapo.

Wapi usipoelewa wewe jombi? Hoja hupingwa kwa hoja.

Labda kama unasema hajawahi kabisa kuwa na uungwaji mkono na umma wa watanzania?

Au ni kule kujitoa ufahamu tu kulikozoeleka tokea pale pande za hapo Lumumba?

Hiiiiii bagosha!
 
Kama wewe ni mtu zamani kidogo. Hebu ifikirie Ivory coast ya wakati wa muasisi wake Felix H Bonnie . Ilikuwa tulivu ya amani na uchumi wa kokoa ya kutilia mfano. Lakini leo hii imekuwa valuvalu kama Tanganyika
Msingi wa uwepo wa Ivory Coast ni tofauti na msingi wa uwepo wa Tanzania. Kila nchi inayo namna ilivyoanza kuwa kama taifa, na siku zote ni vigumu kukuta kuanza kwa Tanzania kuwe kunafanana na kuanza kwa Kenya au Nigeria.
 
Kwako msingi wa uwepo wa Tanganyika ni kutawala kwa Ccm !!. Kinyume chake ni wafuasi wa Ccm kuanzisha vurugu . Nikueleze tu , hakuna aliejua Yugoslavia ya Jusip Tito ingeanguka, wala USSR ingesambaratika na kuwa mataifa 15, Libya ya Gadhaafi kuwa uwanja wa fujo nk . Kila jambo na wakati wake . Hili la Tanganyika ipo siku itakuwa kinyume na matamanio ya wana Ccm.
 
Mkuu bongo hii katika uhai wako usitegemee kuyaona hayo ya Yugoslavia yakitokea. Ondoa kabisa hizo ndoto kichwani kwako.

Mama Samia asingekuwa Rais kama nchi hii ingekuwa ni ya mchezo mchezo, kipindi kile baada ya Magufuli kufariki kama yangekuwa mataifa mengine nchi ingeharibika mazima.
 
Back
Top Bottom