Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Hapo Hagaya atasema video wame edit hakusema hayo maneno.
Siku hizi kwenye ofisi za serikali hata hospitalini na mahakama huduma imesharudi hali ya zamani hawajali mtu
 
Is This A Compromise Or What !!?? If So Such Behaviours Won't End.
 
Hivi tunapoenda kupiga kura na kuwapa ulaji hawa tutayakumbuka haya maudhi na dharau zao?!
 
Mkuu umeandika kinyonge sana..πŸ˜‘πŸ˜‘
 
Maana yangu ni kuwa, kama Rais hayo maneno ya kuonyesha kuwa kupiga marufuku, na kuzuia upigaji sio kipau mbele kwake hakupaswa kuyatamka.
 
... huo ni mtazamo wako usilamishe kila mtu aelewe ulivyoelewa wewe! Rais alikuwa very clear, nanukuu,

" ... sio kwamba hampati; mnapata lakini jipimieni; jipimie! Kwa mfano kuna lile nililolisema la ujenzi wa meli; kuna kijiajenti huko pembeni kinalipwa milioni 2 dola kwa kila meli. Hiyo sio sawa, sio sawa! Sijui kuna ujenzi wa barabara, fedha itagawiwa kwanza weee barabara ikijengwa inakuwa compromised, viwango vinakuwa compromised ..."

... kwa nukuu hiyo unataka tusiwe "closed-minded" tuone kwamba hajazungumzia ufisadi. Hiyo USD 2 m Rais anayong'aka sio sawa kulipwa kwa "kijiajenti" ni hela ya mboga sio? Na hiyo ya fedha za barabara kugawiwa kwa kiwango cha ku-compromise ubora?

Rais alitakiwa akemee vitendo hivyo in strongest terms possible na sio kuviongelea kwa soft language - 'JIPIMIENI MSIVIMBIWE' maneno ambayo ameya-connect moja kwa moja na fedha za miradi tena kwa mifano. Kinyume chake wewe unataka tuamini alimaanisha "wasiingiliane na kugombana katika kutekeleza majukumu ya sirikali"; you must be joking.
 
... watu wengine kwa kujitoa ufahamu hawaoni tatizo! Kauli ile inatakiwa iombewe msamaha na mhusika mwenyewe aliyeitoa; na sio wapambe kujifanya kuitolea "ufafanuzi".
 
... watu wengine kwa kujitoa ufahamu hawaoni tatizo! Kauli ile inatakiwa iombewe msamaha na mhusika mwenyewe aliyeitoa; na sio wapambe kujifanya kuitolea "ufafanuzi".
Mkuu ile kauli haiwezekani mhusika aiombee msamaha kwa sababu ukiangalia hii hotuba yake hapo mwanzoni kabisa anadai kuwa ni mara ya pili anatoa ule msimamo/kauli.Hii maana yake ni kwamba alichokisema ndiyo msimamo wa serikali yake.

Wewe kudai kuwa mhusika aombe msamaha kitu ambacho ni msimamo wa serikali yake unajaribu kupaka ufisadi mafuta kwa mgongo wa chupa kitu ambacho kinakufanya kuwa kama hawa jamaa ambao ni mazezeta.
Your browser is not able to display this video.
 
Iko wazi waibe lakini wasizidishe!! Disgusting what a leader!!??
 
Kama niliwahi kuonesha japo chembe ya imani kwa SSH; naomba nikiri nilikosa mimi na nilikosea sana. Naomba mnisamee!
Performance ya urais wa SSH utakuwa juu kidogo ya A.H Mwinyi na chini ya JM Kikwete!
Na hivi upinzani nao bado wanajitafuta;
Hakika,
Tumepigwa!
 
Hii kauli inauma sana.
Wajipimie kiasi gani?
100Mil.
600Mil.
1Bil.
100Bil.
200Bil.
..........?
Halafu mwenye kamba ndefu zaidi(Rais)
atakula sh.ngapi?.
Tunampenda sana Mheshimiwa Samia,Ila kwa kauli hii ni vyema akaomba msamaha.
 
Hii kauli inauma sana.
Wajipimie kiasi gani?
100Mil.
600Mil.
1Bil.
100Bil.
200Bil.
..........?
Halafu mwenye kamba ndefu zaidi(Rais)
atakula sh.ngapi?.
Tunampenda sana Mheshimiwa Samia,Ila kwa kauli hii ni vyema akaomba msamaha.
Hata akiomba msamaha ndo kaongea ya moyoni
 
Kula kwa urefu wa kamba yako, hapo unahitaji ufafanuzi upi. Akili za kuambiwa changanya na zako...Tunaongozwa na mfalme juha.
 
History ina tabia ya kujirudia. Mzee Mwinyi alitoa RUKSA sasa SSH naye ametoa RUKSA. Nadhani hii itazua yafuatayo:-

1. Power struggle
Wengi wataanza kupambana hata kwa kuhonga kutafuta madaraka badala ya kudeliver. Utekelezaji wa ilani utazorota.

2. Security of property.
Wenye mashamba na viwanja wajipange kuhakikisha usalama wake. Uporaji wa mali za watu wasio na madaraka na ukwasi utashamiri. Mwenye nacho ataongezewa asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho. Hati juu ya hati. Wawekezaji wanaochukuwa kwa kificho ardhi yenye ukubwa hata wa Wilaya nzima. Vita ya wakulima na wafugaji.

3. Institutional failure.
PCCB, Land Court/Judiciary, Police, Ethics Commission zitapotezewa nguvu zao na hiyo high profile decree (kula mle lkn msivimbiwe na msigombane bali kila mtu kwa urefu wa kamba yake)

4. Proliferation of Mega & Giga Corruption.
Public finances at major risk, thus donours demoralized.

5. Unajuwa mimi ni nani?


Naunga mkono mada ufafanuzi upya ufanyike maana huku mitaani tafsiri ziko nyingi na mzuka unapanda.

NB.
Nadhani kazi ya urais inawafaa sana watu wa bara (kanda ya ziwa) kuliko wa mwambao.
 
Wamefukuzwa kazi wakurugenzi wanne wa halmashauri nne. Nadhani unaitafsiri vibaya maana ya hiyo video, au unafanya kisiasa zaidi ukiwa humpendi SSH.
 
Kauli iko clear kwamba watu wajipimie,wale kwa urefu wa kamba zao yaani wawe na kiasi.Ukizidi tuu urefu wa kamba yako tunakula kichwa na kizimbani unapandishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…