Rais Samia, hii Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ina ukakasi kidogo


Mimi naona kuwa wanaificha taaluma husika hapo na kuibeza moja hiyo wizara ilitakiwa iwe ya ustawi wa jamii kwasababu makundi maalumu jinsia watoto walemavu wote hao wanafanyiwa kazi au kushighulikiwa matatizo yao na ustawi wa jamii lakini kuiweka maendeleo ya jamii wametukosea sana maendeleo ya jamii ilitakiwa iwe kule kwenye wizara ya fedha na mipango
 
Mkuu nashukuru sana umeweza kuuweka mjadala sasa kwenye uelewa mpana.

Tukisema Wizara ya USTAWI WA JAMII inabeba nadharia pana zaidi kwa sababu hiyo ya kuanza kutaja constituencies za ndani ya ustawi wa jamii utakuta hatutaweza kumaliza leo.

serikali ikaliangelie hili nalo
 
Vulnerable group sio special needs ni vitu viwili tofauti.

Special needs au kundi la watu wenye mahitaji maalum kwa kiswahili inaashiria walemavu tu (physical disability only)...
Serikali hasa rais aangalie namna ya kukata haya maneno kwa kuiweka wizara hiyo kuitwa ya USTAWI WA JAMII...

mengine tutakuwa tunajenga dhana kila ahsubuhi
 

Na ndio maana ata katika kufanya kazi tuna banwa swana na hawa maendeleo ya jamii

Unapo ongelea maendeleo ya jamii ina husisha maendeleo yote yanayo husu jamii na wizara yake ingependeza zaidi kuwa kwenye wizara ya fedha na mipango

Ila makundi maalumu jinsia walemavu na watoto hawa baba yao na mam yao ni ustawi wa jamii na siku zote wanaenda huko kutatuliwa laikini kwakuwa hatuna wizara maalumu tuna tanga tanga sana kama watoto yatima mala tuna hamishwa kwenye wizara ya afy mara maendeleo ya jamii sisi kama wana taaluma tuna taka wizara yetu isimame mwenyewe
 
Serikali hasa rais aangalie namna ya kukata haya maneno kwa kuiweka wizara hiyo kuitwa ya USTAWI WA JAMII...

mengine tutakuwa tunajenga dhana kila ahsubuhi
Ndio inavyoitwa nchi nyingi ‘ustawi wa jamii’ (social services), ila ni department tu ya wizara ya afya.

Lakini ata huko kwenye ustawi wa jamii utakuta kuna junior ministers wa watoto, junior minister special needs na junior wanawake na wazee.

Kwa sababu social services ina mambo mengi sana kuweza kuwa wizara independent na sera za hayo makundi hazifanani so either way unaweza badili jina lakini shughuli na majukumu zinabaki vile vile in practice.
 

Lakini ushawai jiuiliza kwanini hawataki kuipa wizara yake yenyewe?
 
Namaanisha kuwa wizara inayo jitegemea kama wizara ya afya na isiwe inabebwa bebwa au kutambuliwa kama idara
Ndio mantiki ya kutoa maswala ya wanawake, wazee, watoto, vijana na watu wenye mahitaji maalum chini ya Afya ili wajikite na shughuli za ustawi wa jamii pekee (social services).

Jukumu lao sio kuwawezesha kifedha bali protection of their welbeing (safeguarding) be it they are failing miserably kwa matukio tunayosoma kila siku.

Wakuu shukran kwa mjadala mpaka jioni mungu akipenda. I really have to do other things now huku nikiwa msomaji tu wa JF.

👋
 
Neno JINSIA limeshazua taharuki huko Duniani na limepelekea kamusi zianze kutengeneza tafsiri mpya.

JINSIA linatupeleka kutambua Yale mambo yakishetwani ya sodoma na gomora, nashauri liondolewe itafutwe tafsiri isiyowapa watu wa magharibi mwanya wakupenyeza mambo Yao.

Huku kwao wameanza kuwa so sensitive kwenye haya maneno.....wanahita Haki sawa
 
Twende mbele zaidi kidogo. Kama wizara ni ya Jamii, kwani Jamii ni nini!!? Kwanini tuichanganue jamii kwa jinsia badala ya jamii kwa ujumla wake!!? Why tuwe wabaguzi wa Jinsia!!?
 
Ninachoonaga na Wakuu wa Wilaya kuwapa kibali cha kupita kuchangisha michango tu sijui wanafanya nini kama wataalam,hivi chuoni ndivyo mlivyofundishwa?.
Sijui huo utaalamu wenu mnautumia vipi kama hutoajiliwa serikalini?.kama kuna mnayoyafanya tuambie tuwaelekeze wenye shida za kijamii muwatatulie.
 
Twende mbele zaidi kidogo. Kama wizara ni ya Jamii, kwani Jamii ni nini!!? Kwanini tuichanganue jamii kwa jinsia badala ya jamii kwa ujumla wake!!? Why tuwe wabaguzi wa Jinsia!!?
Mhe Dkt Mwijuma anaweza kuwa msaada mzuri kutuelimisha hapa, kwa sababu ni sehemu ya msingi wa hoja yangu pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…