Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha reli, shujaa wa Afrika,jasiri muongoza njia na nuru ya Wanyonge.
Amempongeza sana Jihan Binti yetu Watanzania aliyeliletea Heshima Taifa Letu Na kuipeperusha Vyema Bendera yetu na kufanya kwa Mara ya kwanza Wimbo wetu wa Taifa kupigwa Na kusikilizwa Duniani kote hadi Whitehouse Marekani.
Dunia imetambua nguvu ya Taifa letu la Tanzania na ushawishi tulionao kama Taifa. Tumeushangaza Ulimwengu na kuiduaza Dunia. Dunia imetambua Umoja na mshikamano wa watanzania.
Dunia Imetambua namna Rais wetu Mpendwa alivyoliunganisha Taifa letu na kuwa na nguvu ya Umoja na Mshikamano wa Pamoja . Taifa limegonga vichwa vya Habari vya Dunia yote na kuwa na kiu ya kufika Nchini.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.