Rais Samia huenda akatawala kwa muda mrefu kama Nyerere

Rais Samia huenda akatawala kwa muda mrefu kama Nyerere

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Mwalimu Nyerere alitawala kwa miaka 24 (1961-1985).

Kwa mujibu wa katiba ya sasa iwapo rais Samia atatawala kwa katiba ya sasa bila kuibadili, anaweza kutawala kwa muda wa miaka 9, Lakini akileta katiba mpya kabla ya mwaka 2030, maana yake ataanza upyaaa kwa katiba mpya, na hatofungwa na masharti ya vipindi viwili vya katiba ya zamani!

Tena basi akitengeneza katiba mpya ya vipindi viwiliviwili vya miaka Saba saba, maana yake ana potential ya kutawala 9+7+7=23

Mama ashindwe yeye tu, lakini njia ya kutawala miaka 23 nyeupeeee, ajipange tu
 
Uoga, afya, stress chamani, umri, ni baadhi ya vikwazo kwake kufikia hilo lengo.

CCM ukiwaambia Katiba Mpya wanarukwa na akili, hawajui itakuwa na manufaa hata kwao, itawafanya wasijipendekeze tena ili wateuliwe, na wakiteuliwa watakuwa huru kufanya kazi huku wakilindwa na sheria sio mwenyekiti wa chama.
 
Hiyo katiba mpya lazima izuie marais waliopita kugombea, unless unachokitafuta na huu uzi wako utakipata.
 
Lengo lako ni kutaka atawale muda mrefu?
 
Mwaka 2028 tunapata katiba mpya, uchaguzi wa 2030 unafanyika kwa mujibu wa Katiba mpya na Samia anagombea kwa mujibu wa masharti ya katiba mpya!
Anatawala vipindi vyake vingine viwili kwa mujibu wa masharti ya katiba mpya, eventually kiujumla atatawala 9+7+7=23
Au 9+5+5=19
Okey
 
Mwaka 2028 tunapata katiba mpya, uchaguzi wa 2030 unafanyika kwa mujibu wa Katiba mpya na Samia anagombea kwa mujibu wa masharti ya katiba mpya...

Kama hiyo ndiyo ^Katiba Mpya^ inayotafutwa kwa jasho na damu, afadhali ^car-bee-sir^ tu tuendelee na hii ya sasa kwa miaka 1,000 ijayo!
 
Anataka Katiba Mpya hata Nape alisema kuhusu Katiba Mpya ni mambo yanazungumzika. Sasa hivi yuko ndani ya Nyumba nadhani watamshauri vyema.
 
Mwalimu Nyerere alitawala kwa miaka 24 (1961-1985).

Kwa mujibu wa katiba ya sasa iwapo rais Samia atatawala kwa katiba ya sasa bila kuibadili, anaweza kutawala kwa muda wa miaka 9, Lakini akileta katiba mpya kabla ya mwaka 2030, maana yake ataanza upyaaa kwa katiba mpya, na hatofungwa na masharti ya vipindi viwili vya katiba ya zamani!

Tena basi akitengeneza katiba mpya ya vipindi viwiliviwili vya miaka Saba saba, maana yake ana potential ya kutawala 9+7+7=23

Mama ashindwe yeye tu, lakini njia ya kutawala miaka 23 nyeupeeee, ajipange tu

Huo upupu wako muulize Kabila Jr wa DRC, Nkurunzinza wa Burundi na hata Kagame wa RW, endelea hadi kwa kina Gbagbo wa Corte de V
 
Back
Top Bottom