Rais Samia huna nia njema na Wizara ya Nishati, haifiki kokote kwa teuzi za urafiki

Rais Samia huna nia njema na Wizara ya Nishati, haifiki kokote kwa teuzi za urafiki

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,705
Reaction score
4,703
Tukubali kwamba hii ni Wizara ambayo waliowekwa ni watu misheni town tu.

Nimesikiliza hata huyo anayeitwa Maharage Chande ni aibu tu. Yaani anahangaika na gharama za kuunganisha umeme! Hizo gharama zinaleta faida ktk shirika? Yeye anatakiwa azalishe na kuuza umeme kwa faida badala ya kuhangaika na kuunganisha kwa gharama kubwa. Hawa ni watu wasiojitambua. Nadhani kosa limeanzia kwenye uteuzi. Huwezi kuteua watu 'ngwini' kwenye wizara ambayo mambo yote ni sayansi.

Waziri 'ngwini'. Mkurugenzi Tanesco 'ngwini' Bodi ya watu 8 ina wahandisi wawili ambao walishasahaulika kwenye bodi ya mainjinia, wengine pia ni Ngwini.

Biashara ya umeme inahitaji uzalishaji wa kisayansi na kuuza umeme kisayansi. Ni tofauti na kutafuta wateja wa Multichoice au kuuza ticketi za TFF.
 
Kesho narudi hapa kueleza maoni yangu juu ya teuzi za Samia na ulimbukeni wa wateule wake. Wengi wamefanikiwa kwa kutumia majina ya wajomba na ukuadi ktk mitaa.
----------------
Nimerudi maana uzi huu unagusa maisha yetu huku mitaani kwa kinyozi. Nivumilieni niseme ili rais ajue tunayajua yanayofanyika
Masikitiko yangu yanaanzia kwa rais Samia. Mitaani kinachosikika ni kwamba kila kitu anaulizwa Kikwete. Suppose ni ukweli kwa uhusiano wowote walionao, hivi kweli unaweza kuendelea kuteua watu ambao walikuwa kwenye serikali ya mizaha, ya Kikwete, ukitegemea wa-TZ tutaona ni powa tu! Au ni ile hali ya kusema watafanya nini? Yes hatuna la kufanya lakini rais anajisiaje anaposimama mbele za watu wanaojua mizaha yake?

Hii Wizara kwa hali ya sasa ni laana tu! Mtu anasoma mitandaoni halafu anaingia nayo Bungeni kama rejea ya utaalamu wa matengenezo ya miundombinu ya umeme, anasema Duniani kote bhla!-bhla! Huyo bwana Maharage ndo kabisa! Kweli rais Samia hakumjua kwamba alikuwa kwenye kitengo cha upigaji dili za ikulu? Halafu akaambiwa na akamteua aiendeshe TANESCO! Tukubaliane kwamba CV ya kuendesha Multichoice siyo sawa na TANESCO. TANESCO ni umeme, bidhaa isiyohitaji matangazo ya biashara. Ni bidhaa isiyohitaji kusafirishwa kwa maroli. Ni bidhaa isiyo na ghala la kuihifadhi. Kuna mengi yanayofanya uzoefu wake kuwa uchafu kama atauingiza TANESCO.

Angalia hiyo Bodi ya akina Mafuru na skandali za mikopo ya Benki, akina Msechu aliyeamini ujenzi wa nyumba ni sawa na kutunza hesabu za fedha benki. Vyeo vya Ngwini vina mipaka jamani! biashara bila kuijua taaluma ya unachozalisha au kuuza ni kichaa kweupeeeee! Tuendelee na urafiki na uhawala na ubishoo!
 
FB_IMG_1645601155648.jpg
 
Kwanza anzia na Raisi wenu mwenyewe inaekekea hata logic ya Magu (RIP) kujenga SGR sambamba na Bwawa la Nyerere haijaeleweka, sasa wanasema (Samia) ananunua treni za umeme hapo hapo Bwawa la Nyerere linapotezewa siajabu limeshasimamishwa, sasa umeme wa kusukuma treni utatokea wapi ?
 
Kwanza anzia na Raisi wenu mwenyewe hata inaekekea hata logic ya Magu (RIP) kujenga SGR sambamba na Bwawa la Nyerere haijaeleweka, sasa wanasema (Samia) ananunua treni za umeme hapo hapo Bwawa la Nyerere linapotezewa siajabu limeshasimamishwa, sasa umeme wa kusukuma treni utatokea wapi ?
Wanapambania gesi mkuu.
 
Kwanza anzia na Raisi wenu mwenyewe inaekekea hata logic ya Magu (RIP) kujenga SGR sambamba na Bwawa la Nyerere haijaeleweka, sasa wanasema (Samia) ananunua treni za umeme hapo hapo Bwawa la Nyerere linapotezewa siajabu limeshasimamishwa, sasa umeme wa kusukuma treni utatokea wapi ?
Hiyo Bwawa la Nyerere limepotezewa kivipi?!

Tatizo mlikuwa mnadanganywa sana kiasi cha kuamini ujenzi pale JNHPP ulikuwa unaendelea kwa kasi kweli kweli!

Hata mradi ulipokuwa deleyed for 5 months bado mkaambiwa "mambo ni fire"

Hata pale by December 2020 ambapo mradi ulitarajiwa uwe umekamilika kwa 46% lakini ndo kwanza ulikuwa 28%, mkaendelea kudanganywa kwamba "mambo ni fire"!

Leo akina Phillip Mpango wanapoamua kuwa wakweli na kuwaambia mradi umechelewa kwa sababu hii na ile, na kwamba Contractor katoa kazi nyingi muhimu kwa Subcontractors, hamtaki kukubali kwa sababu mlishamaanishwa kila kitu kipo okay huku hata ripoti za CAG za miaka ya nyuma zilikuwa zinaonesha ni namna gani mradi unavyo-delay!!
 
Tukubali kwamba hii ni Wizara ambayo waliowekwa ni watu misheni town tu.

Nimesikiliza hata huyo anayeitwa Maharage Chande ni aibu tu. Yaani anahangaika na gharama za kuunganisha umeme! Hizo gharama zinaleta faida ktk shirika...
Nimeliona hili mkuu ni tatizo kubwa.Tunahitaji watu wenye uzalendo,weledi, commitment na taifa letu,teuzi za kirafiki,vimemo na undugu hazitatusaidia kama Taifa, Rais Samia chonde chonde, usitupeleke huko.
 
Mama hajui sasa afanyaje ,ila ni msikivu sana tumieni proper channel ,anajitahidi sana kapambana ,mungu amsaidie ila amepunguza wanafiki ,sema kwenye vya technical hakujua angesikiliza tulio maeneo technical ,ila nawaapia tunaenda poa balaa
 
Tukubali kwamba hii ni Wizara ambayo waliowekwa ni watu misheni town tu.

Nimesikiliza hata huyo anayeitwa Maharage Chande ni aibu tu. Yaani anahangaika na gharama za kuunganisha umeme! Hizo gharama zinaleta faida ktk shirika...
Atakuja bwana CM 1774858 kukusema una wivu na Makamba!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kesho narudi hapa kueleza maoni yangu juu ya teuzi za Samia na ulimbukeni wa wateule wake. Wengi wamefanikiwa kwa kutumia majina ya wajomba na ukuadi ktk mitaa.
Kama kuna Taasisi au Shirika lililo na changamoto za kiuongozi ni linalohusika na shughuli za uzalishaji kama vile viwanda. TANESCO kwa upande mmoja inazalisha umeme, hivyo basi, inahitaji uongozi wenye sifa na ujuzi wa kuzalisha.

Kwa uteuzi wa "mangwini" (waliopata elimu kwa kutumia vitabu vya "penguin") watapata shida sana kuliendesha kwa kuwa wafanyakazi wazalishaji watakuwa wanawalisha taarifa potofu inapotokea tatizo la kifundi (rejea kauli ya Waziri Makamba ati "umeme unakatikakatika kwa sababu ya waya uchi kugusana"!!!!)

Kama Rais SSH anawaona hao aliowateua wanafaa sana aigawanye TANESCO ya kuzalisha na kusambaza, na ya kutoa huduma (kuuza umeme). Wateule wake waendesha TANESCO huduma.
 
Back
Top Bottom