Wanataka rais atoe maneno kupingana na msimamo wa chama chake cha CCM. Akifanya hivyo, angewafurahisha. Hata hivyo, naona Samia ameepuka kukamatwa katika mtego wa CDM. Mbowe ametoa lawama nyingi na hata kumuita JPM dikteta na kudai kwamba aliwatesa watu. Hivyo, isitokee tena. Sijui kama Samia alijua. Njia ya maendeleo kwa Tanzania ni ile ya kimagufuli tu. Na hiyo ndio njia ya kinyerere, Ki Edward Sokoine, njia ya Kisamora Machel, njia ya Ki Thomas Sankara, njia ya kijamaa. Binafsi, nilihofu kuwa mtego utamfetukia Mama Samia lakini ameepuka hilo.
Vita kubwa inaendeshwa na maajenti wa ubeberu kupitia upinzani, ambao wanajaribu kufuta jina la JPM na ujumbe wake katika mioyo ya Watanzania. Hata hivyo, hili halitafaulu kamwe. Wametumwa watu kama Lissu, Lema, na Mbowe, lakini hawawezi kufaulu.