Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Hakuna haja ya kiherehere kama cha facebook na twitter.Yeye kasema huwa anasoma tu.Akitaka kujiunga atafanya mwenyewe na sisi tuambiwe kuwa yupo.Lakini ya nini kutafuta matusi humu.Asome tu kidogo vichwa vya habari.
Hata mi nashangaa,sijsikia akisema amejiunga,itakuwa anasoma kama Guest
 
Mama Samia. Tukiwa kwenye haya maridhiano, hepu walipe kifuta jasho hata Kama Ni flat rate waliovunjiwa nyumba zao Kimara, Mbezi mpaka Kiluvya bila kulipwa hata shilingi.
Watu bado wanateseka.
Asante kwa usikivu.
 
Hata mi nashangaa,sijsikia akisema amejiunga,itakuwa anasoma kama Guest
Wanasiasa wengi wakubwa ni member wa JF, kwa mtu ambaye yupo humu muda mrefu analijuwa hilo.

Huyu mama mkumbuke alikuwa ni mbunge tu, possibly ana fake I'd yake kitambo tu.

Sasa kama Jaji Werema na Anna Tibaijuka wana verified ID za JF mtashangaa mama Samia ambaye alikuwa hawafikii kihadhi hao watu Wawili kabla ya kupanda hadhi na kuwa vice President?
 
Ameyaweka wazi hayo katika mkutano wa Bawacha katika siku ya mwanamke duniani.

Rais Samia akihutubia taifa kupitia mkutano huo amewaambia kuwa huwa anasoma maoni ya katiba mpya, wabunge wa Covid19 na mengineyo kuhusu Serikali yake kupitia mtandao maarufu wa JamiiForums.

My take:
Leo ndio nimejua kuwa kumbe Rais Samia nae ni mdau wa JamiiForums.

Hii imetuinua sana wana jukwaa hili.

Faizafox
 
Wanasiasa wengi wakubwa ni member wa JF, kwa mtu ambaye yupo humu muda mrefu analijuwa hilo.

Huyu mama mkumbuke alikuwa ni mbunge tu, possibly ana fake I'd yake kitambo tu.

Sasa kama Jaji Werema na Anna Tibaijuka wana verified ID za JF mtashangaa mama Samia ambaye alikuwa hawafikii kihadhi hao watu Wawili kabla ya kupanda hadhi na kuwa vice President?
Ok, Inawezekana pia
 
JF ndo mtandao was wasomi hata nilipokuwa chuo kila Great thinker anatumia JF so lazima apite hapa Kupata madini
 
Faiza Fox nadhani ndiyo atakua Mama Samia humu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Siyo kweli, Faiza foxy ni kama robot, alishanyiwa analysis hapa miaka ya nyuma hakuna binadamu mwenye uwezo na speed ya comments kama Faiza Foxy.

Tukajiridhisha kabisa Faiza Foxy si binadamu wa kawaida au ni robot.

Mfano wewe uambiwe ndani ya dakika mbili uwe umepost thread na kucomment Mara 20, haiwezekani hilo limewezekana kwa Faiza Foxy pekee.

Na fact ya mwisho Faiza Foxy alikuwa yupo JF full time JF 24/7.

Hakuna mwanasiasa yeyote au mtu high profile anaweza kukaa active mtandaoni kuitwa nzima, usiku kuacha, vikao atafanya saa ngapi?
 
Back
Top Bottom