Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Jamii forum ya Sasa imevamiwa na vitoto Fulani havina hoja zaidi ya matusi
 
Matusi ni makosa ila kejeli ni sehemu ya siasa, Hata wakina Socrates, Plato na Aristotle walikuwa wakifanyia kejeli kwa tawala za wakati wao.
 
Kama kweli Mh. Rais unapitiaga maoni yetu yakiwemo ya kupunguza mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha, tunaomba usiishie tu kucheka, jitahidi kupitia kwa wasaidizi wako kutupunguzia ukali wa maisha ili 2025, usitumie nguvu kubwa kutuomba kura. Achana na usemi wa Waswahili kwamba; "Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa". Please mama, jitahidi kutulegezea gharama za maisha ili na sisi tukupende toka moyoni na siyo tukupende kwa unafiki au kwa sababu ya kukuogopa kutokana na nafasi uliyo nayo.
Binafsi ninaamini, ukiamua unaweza kupunguza gharama za maisha kwa wananchi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…