Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Duh! Kumbe hii JF Ni maarufu kiasi hicho jamani[emoji848]!!

Hongera Sana Maxence Melo
Laaaaa,unakosa mengi mazuri.
Screenshot_20230224-102948.jpg
 
Rais Samia: Hakuna kisichowezekana kwenye mazungumzo, tumesuhudia nchi kadhaa zimeingia kwenye vita hawakupata suluhu, suluhu imepatikana kwenye mazungumzo kwahiyo tuendelee kuzungumza. Najua si rahisi kabisa watu kuja na utamaduni huu mpya ukakubalika mara moja, si rahisi, kwangu kuna vikwazo kwangu kuna vikwazo.

Huwa napitia Jamiiforums naangalia maoni yenu kule ndani, nasoma nnacheka, nasema lakini huu ni utamaduni mpya, si rahisi kukubalika kwa ghafla, kwahiyo pande zote Tanzania nzima si rahisi kukubali utamaduni huu mpya kwa haraka.

Jamii forum ya Sasa imevamiwa na vitoto Fulani havina hoja zaidi ya matusi
 
Matusi ni makosa ila kejeli ni sehemu ya siasa, Hata wakina Socrates, Plato na Aristotle walikuwa wakifanyia kejeli kwa tawala za wakati wao.
Mods, JF imepewa heshima kubwa sana. Kama Rais huwa anapitia humu kupata maoni yetu kama sehemu ya umma wa Watanzania, hakika nawaambieni, hakuna kiongozi ambaye hatapita JF.

Lakini ili maoni yetu yapewe uzito wa kupewa tafakuri ni lazima Mods walinde hadhi ya jukwaa kwa kuwapa adhabu kale wale wote wanaoligeuza jukwaa lionekane ni la wahuni.

Mtu akitukana au kukejeli, apigwe ban hata ya miezi 6 au mwaka mzima. Kuna watu humu, wanashangaza, wanafikia kumtukana kiongozi, unatafakari na kujiuliza JF siku hizi imebeba watu wa namna gani?

Mods, lirudisheni jukwaa kwenye heshima yake ili kiwe ni chanzo muhimu cha habari kwa wasio na habari, liwe ni jukwaa la ushauri kwa viongozi wa Serikali, vyama na taasisi mbalimbali.
 
Rais Samia: Hakuna kisichowezekana kwenye mazungumzo, tumesuhudia nchi kadhaa zimeingia kwenye vita hawakupata suluhu, suluhu imepatikana kwenye mazungumzo kwahiyo tuendelee kuzungumza. Najua si rahisi kabisa watu kuja na utamaduni huu mpya ukakubalika mara moja, si rahisi, kwangu kuna vikwazo kwangu kuna vikwazo.

Huwa napitia Jamiiforums naangalia maoni yenu kule ndani, nasoma nnacheka, nasema lakini huu ni utamaduni mpya, si rahisi kukubalika kwa ghafla, kwahiyo pande zote Tanzania nzima si rahisi kukubali utamaduni huu mpya kwa haraka.

Kama kweli Mh. Rais unapitiaga maoni yetu yakiwemo ya kupunguza mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha, tunaomba usiishie tu kucheka, jitahidi kupitia kwa wasaidizi wako kutupunguzia ukali wa maisha ili 2025, usitumie nguvu kubwa kutuomba kura. Achana na usemi wa Waswahili kwamba; "Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa". Please mama, jitahidi kutulegezea gharama za maisha ili na sisi tukupende toka moyoni na siyo tukupende kwa unafiki au kwa sababu ya kukuogopa kutokana na nafasi uliyo nayo.
Binafsi ninaamini, ukiamua unaweza kupunguza gharama za maisha kwa wananchi wako.
 
Back
Top Bottom