Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Ni leo tena.
Mheshimiwa Rais amewatupia lawama Wasukuma kwa kuharibu vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa sababu ya ufugaji wao wa ng'ombe wengi.
Nia yangu bayana kwenye andiko langu ni kumshauri Rais ikiwezekana ajizuie kuwataja moja kwa moja Wasukuma kwenye hadhira kwa sababu hali ile pengine inaweza kutafsirika tofauti na walengwa hasa ukizingatia ndani ya muda mchache wa Utawala wake tuhuma nyingi za kubaguliwa walengwa zi bayana.
Ingetosha mheshimiwa Rais angetoka kauli ya jumla tu kwamba wafugaji ni sehemu ya wanaoharibu vyanzo vya maji
Sasa unapowataja Wasukuma moja kwa moja ilhali wapo wamasai na makabila mengine mengi yanayofuga maelfu ya mifugo ni sawa na kuwabagua watajwa
Mungu ibariki Tanzania.