#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

Watu ni maskini tangu nchi ipate uhuru. Umaskini wa watu haujasababishwa na Samia
 
JPM alikosea sana. Na hii iwe wake-up call kwa presidential wannabes wote. Hii habari ya kuteua bora mgombea mwenza ni potential disaster. Rais hana mkataba na Mungu juu ya maisha yake!
Kama JPM alikosea kumteua kama mgombea mwenza kwa nini hamkupinga ili ateue mtu mnayemtaka nyie
 
Kwani amesema hakubaliani na KILA KITU kilichofanyika kwenye utawala wa JPM? Msimuwekee maneno mdomoni
 
Huyu Mama Samia hata hakumbuki aliapa nini hata ukiuliza atakwambia jaji alinipa kilikuwa kimeandikwa akasema nisome kwa sauti hata sikumbuki kilikuwa kinasemaje labda ukamuulize jaji aliyeniapisha
Inaonekana wewe unamchukia sana SSH
 
Msema ukweli siku zote ni mpenzi wa Mungu!

Mwacheni Mama aseme ukweli.
 
Si angeachia ngazi aache taarabu na vijembe
 
Chawa mkumbusheni huyu mama aweke akiba ya maneno
 
hivi kwa akili yako ya kawaida tu . unataka kusema angeamua kujiuzuru mbele ya bwana yule angekuwa hai huyu?

Unajiuzuru kwa kuangalia nature ya kiongozi wako .
Bora lakini umesimamia haki kuliko kujifanya harmonize unamponda diamond hali bila diamond ungekuwa unauza maji mtaani.
 
Atuambie na wasiojulikana walikuwa kina nani.
 
Bora lakini umesimamia haki kuliko kujifanya harmonize unamponda diamond hali bila diamond ungekuwa unauza maji mtaani.
Msipende kurahisisha jamani . makamu wa rais ni mtu mkubwa katika nchi si rahisi kuachia kama unavyofikiria .
Hivi unafahamu kuwa katika ushindi wa jiwe kulikuwa na jasho la Huyo mama?. Yeye kuwepo kwenye karatasi ya kupigia kura kikatiba na kisheria ni jambo zito sana .
Tujifunze kwa mgogoro wa Sudan kusini kati ya rais na makamu wake.
 
Kwann anamnanga aliyempa maisha ukosefu wa shukrani huo bila jiwe asingekuwa alipo hapo.
Tuwe na shukrani na waliotuinua
 
Rais Samia amewambia wamarekani kuwa ilikuwa ni vigumu kwake kufanya kazi na Magufuli.

Na alikuwa ana tofautiana nae sana kwenye mambo mengi hasa jinsi alivyokuwa ana kabiliana na swala la UVIKO-19.

View attachment 2188625
Mm nafikiri bosi ndiye anafaa ,aone ngumu kufanya kazi na surbodinates wake.Sio surbodinates aone ngumu kufanya kaz na bosi.Kama surbodinates ataona ngumu kufanya kazi na bosi,anaondoka .Je ww Mama Samia Kama ilikuwa ngumu kufanya kazi na bosi wako,mbona uliendelea kuwepo.?Je ulikuwa unafanya kazi gani?Mbona unafiki mtupu huu.
 
Mbona Marehemu Idd Amini anasimangwa?
 
Uchaga umekujaa ndio maana hata urais mtaishia kutawala hapo machame tu
Nan alikwambia tunahitaj? Nyie mliotoa rais mbona mkoa wenu ndio miongoni mwa mikoa maskini hohehahe?
Sisi ni uchumi,pesa,elimu na biashara na maendeleo umesikia ewe sukuma gang?
 
Kuna watu huwezi waambia lolote juu ya Magufuli, hawaji kukuelewa. Kwa sababu aliyoyafanya yameeleweka zaidi.
Kuna kundi lipo na mtazamo tofauti, sijui kwa mwelekeo wao.

Huu ni mtaji wa kisiasa kwa kundi fulani,
Kuendelea kumsema marehemu ni kuimarisha mpasuko,
Na matokeo hata kama si sasa yatakuja kutokea.

Ni rahisi tu, kutomsema marehemu vibaya kunapunguza maumivu kwa wengine.
Otherwise tayari kuna kundi limeamua kuanza kupata mtaji kwa njia hiyo.
Lakini matokeo lazima yapatikane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…