#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

Sema yote mom wetu. Yule Dictator tunajua ya ndani alivyo Ku treat. Mungu akupe nguvu. Unayo support kubwa nyuma yako. Ningekuwa Mimi ni wewe katika hiyo nafasi na Yule Jamaa ningekimbikla uhamishoni kabisa. Lakini ulivumilia. Siku zote mvumilivu hula mbivu💅💅💅💅

KAZI Iendelee. Endelea kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya nchi. Tanzania siyo kisiwa.
Tudokezee kidogo yaliyojiri mkuu...ututoe matongotongo
 
Kwenye swala la covid Jiwe alikuwa sahihi
 
Ifike wakati ccm thinktanks na political strategists na hapa ndio unaona pengo la dr Bashiru Ally. Waliopo wakina Kinana, Mndolwa , mama Kamba , mkuchika wamshauri mama aachane kabisa na kumtaja Hayati JPM chuma negatively kisiasa hii itawapa wakati mgumu huko mbele.
 
Kama kweli walitofautiana lakini akashindwa kusimamia alichokiamini mpaka mwisho basi hakuwa na msimamo.

Sikuwahi kumuona Samia akiwa amevaa barakoa wakati wa Magufuli, mtu pekee niliyemuona amevaa barakoa alikuwa ni Kikwete pekee, au kama, yupo aliyemuona Samia kuvaa barakoa wakati ule hata anioneshe picha na Magufuli akionekana.

Inawezekana Samia aliogopa kitumbua chake kisiingie mchanga akawa tayari kuweka reheni afya yake.
Kwamba Rais anaweza kumfuta kazi Makamu wake?
 
Rais Samia amewambia wamarekani kuwa ilikuwa ni vigumu kwake kufanya kazi na Magufuli...
Na alikuwa ana tofautiana nae sana kwenye mambo mengi hasa jinsi alivyokuwa ana kabiliana na swala la UVIKO 19
View attachment 2188625
Haya, sasa utamuamini kiongozi wa namna hii kwa jambo lolote?

Wakati ule wa Magufuli, alikuwepowepo tu, pamoja na kutokubaliana na kiongozi mwenzake, na akionekana kushiriki yale yale ambayo alikuwa hakubaliani nayo.

Sasa yeye ndiye mkuu wa nchi, ni yapi ambayo hayaweki wazi kwa wananchi anayoyafanya kuhujumu taifa hili?

Kwa vile siyo kiongozi mwenye msimamo thabiti, kwake kila kitu kinawezekana, mradi aonekane yupo.

Huyu atauza taifa zima, kwa sababu hana uchungu na jambo lolote kuhusu taifa hili.

Atapewa masharti huko na kuyatekeleza, halafu atakuja kung'aka, hakukubaliana na masharti yale!

Bure Kabisa!
 
Ifike wakati ccm thinktanks na political strategists na hapa ndio unaona pengo la dr Bashiru Ally. Waliopo wakina Kinana, Mndolwa , mama Kamba , mkuchika wamshauri mama aachane kabisa na kumtaja Hayati JPM chuma negatively kisiasa hii itawapa wakati mgumu huko mbele.
Wanatabia ya kumsifia aliyepo kwa wakati huo kwa kila kitu .... nimeamini Tz inaweza kuwa kitovu cha unafiki Duniani khaa 😅
 
Kama kweli walitofautiana lakini akashindwa kusimamia alichokiamini mpaka mwisho basi hakuwa na msimamo.

Sikuwahi kumuona Samia akiwa amevaa barakoa wakati wa Magufuli, mtu pekee niliyemuona amevaa barakoa alikuwa ni Kikwete pekee, au kama, yupo aliyemuona Samia kuvaa barakoa wakati ule hata anioneshe picha na Magufuli akionekana.

Inawezekana Samia aliogopa kitumbua chake kisiingie mchanga akawa tayari kuweka reheni afya yake.
Labda alikataa nyungu! Hatuwezi kujua mpaka aseme ni tofauti ipo hasa! Kauli nyingine mtihani sana nyakati hizi.
 
hivi kwa akili yako ya kawaida tu . unataka kusema angeamua kujiuzuru mbele ya bwana yule angekuwa hai huyu?
Unajiuzuru kwa kuangalia nature ya kiongozi wako .
sasa mnaokoteza visabau vya kijinga kabisa!

Kwa hiyo, sasa anayasema haya, tena huko nje ya nchi, kwa manufaa gani na kwa nani?

Kwa hiyo yeye anajisafisha, aonekane hakuwa sehemu ya utawala wa kidhalimu?
 
Back
Top Bottom