Ni jambo la kawaida kutofatiana kama binadamu, pia kweli unajikuta huna jinsi ya kufanya, na si mara ya kwanza kueleza haya, aliwahi kueleza mbele yake akitumia misemo kuwa alitunyoosha.
Napenda anavyosema ukweli, wengi walitofautiana na Magu, ngumu kumuelewa hasa anapochukuwa maamuzi mabaya na kulazimisha kuwa yuko sahihi! Maswala ya Covid-19, kupora ushindi, kuchoma vifaranga, kuzuia Kenya kuzika Mkapa, kupeleka miradi mikubwa kwao, lugha mbaya, kutimua au kusamehe kusiko fuata sheria wala utu, kusitisha mikataba na makampuni bila kufuata sheria, mambo mengi, na inafaa tuyaseme ili yasijirudie kwa viongozi wa baadae!