Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Huyu mwanamke aambiwe kila kitu kina mwanzo wake! Wananchi wamefikia ukomo wa uvumilivu!
Kwa lugha nyepesi na ufahamu wangu mdogo, Rais ana tulazimisha tuamini kwamba kifo cha Meddy ni sawa tuu. Alistahili kufa kifo cha aina ile. Ndio maana hataki hata tume huru kuchunguza mauaji yale..
Tuombe tu Mungu yeye huwa ana jibu maana huona hata yaliyo sirini.
 
Watekaji na wauaji watakamatwa lini ili usalama uwepo?
 
Kuna maneno mtu mzima kabla hujayazungumza unatakiwa utafakari vyema kumbuka mtu unayemzungumzia ana familia yake,familia isikie mtu wao katekwa na watu wasiojulikana mara kesho wasikie ameuawa na kutupwa vichakani kama mzoga watu wakaanza kusema kwa hasira kwa tukio baya kama hilo halafu anajitokeza mtu mwingine aseme anakerwa na vilio hivyo na kusema hakuna haja ya vilio hivyo kwa sababu kifo ni kifo tu! Je mtu huyo masaibu hayo yangemkuta yeye angejisikiaje? Angempoteza mtu wake wa karibu mathalani mzazi,mtoto au mwenza wake.
Angeweza kuvumilia maneno ya dhihaka kama hayo? Kwamba hakuna haja ya kelele nyingi kwa sababu kifo ni kifo tu?
 
Ukisikiliza katikati ya mstari utajua watekaji wanafanya kazi ya nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…