Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Nataka nichaneee...../
Na mizuka ikipanda mniruhusu nitukanee.
🎶Nay Wamitego
 
Hata mtu mzima mpumbavu naye huzeeka.

Hivi Mwanasiasa, na Tena wa CHAMA kikubwa, Tena katika Nchi iliyoingia mikataba ya kimataifa kuhusu Siasa ,, AUWAWE, yaan ichukuliwe kua ni Kifo Cha kawaida tu??.

Mpumbavu anatolea mfano Trump, Trump si Dunia nzima kila Chombo Cha habari kilisimama kazi zake na kuanza kufatilia habari za Trump?.kwann wasingempuuza tu kua ni mtu wa kawaida??.

Anashangaa nini Kwa Mzee Kibao??.

Kwann Mataifa yasiingilie Kati katika bara hili la kijinga ambalo víongozi ni madikteta?.
Mi nadhani ungeweza kuandika hoja yako na kueleweka bila kumuita Rais mpumbavu.
 
Mama bora kaongea,maana kuna watu wanafanya vitu vyao huko sirini ili kutafuta huruma ya wananchi ili wapate madaraka!!
Pengine tuliogopa kukemea watekaji kwa sababu tunawategemea kutubeba wakati wa uchaguzi
 
“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”

“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”

“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “

“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”

“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

My Take
Mautekaji ni kama yamechochewa tu, kutoka "drama"" mpaka "mtu mmoja tu".

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Eti Kifo ni Kifo tu!! Maajabu ya Musa.

Ya Trump aliyetaka kuyafanya walimpata hara na amesomewa mashitaka haraka kesho yake! Yule wa awali alipata adhabu yake palepale.
Sasa mheshimiwa Rais Hawa wa kwako hawajulikani na hawatendi wajibu wao tangu tuyaone ya Lissu hivyo usiwanange waliokimbia kumbe basi Kuna mkono sio bure.
 
Yule mwanamuziki anajiita ROMA aliponea chupu chupu naye alitupwa huko huko Ununio kama sikosei. Serikali huwa wanatoka nakujidai wameumia lakini, wanajua wao ndio wahusika.

Eti wanachunguza, uongo uliokithiri huu. Mawazo aliuwawa wakasema wanachunguza, Ben Saanane wanachunguza, yule muandishi kuli kibiti wanachunguza, alitekwa Mohamed Dewji wakasema wanachunguza.

wametekwa vijana wa Chadema, wanachunguza, katekwa aliyechoma picha ya Bi Chura, wanachunguza.

Bora Magufuli aliposema hawachunguzi shambulio la Tundu Lisu, maana hakuona umuhimu kupoteza muda.

Hata huyo asipotezee watu muda kwa kutudanganya, aseme tu hatuchunguzi.
 
Wakati familia yake ikiwa kwenye msiba mzito wa kupoteza mpendwa wao, watanzania wa kipindi hicho watakuwa nao wakigonga glasi na kukejeli "kifo ni kifo tu"

Bahati mbaya yeye atakufa kifo cha huzuni sana lakini watu hawatajali, pambio litakalotembea ni "KIFO NI KIFO TU"

* Maisha ya duniani tunapita kwa muda mfupi sana, hivyo tuishi kwa upendo na kumthamini kila mtu.
 
Back
Top Bottom