Rais Samia ingilia kati utoaji wa mikopo mwaka 2023. Kwa Trend hii ya HESLB, wengi hawatakwenda vyuoni

Rais Samia ingilia kati utoaji wa mikopo mwaka 2023. Kwa Trend hii ya HESLB, wengi hawatakwenda vyuoni

Nyinyi wasomi wa vyuo vikuu wa miaka na siku hizi, hovyo kabisa. I.Q. zenu mmejikita kujifunza na kuimba nyimbo za akina Diamond, Kiba, n.k., kushabikia Yanga, Simba, Man City, n.k., "uchawa" kwa Chama tawala, uasherati, na kadhalika. Hayo ndiyo maeneo mumebobea. Kuwa "think tank" ya nchi, ... mmh!
Sasa kama vyuo hivi vikuu walimu wao ni akina Profesa Kabudi, Mkumbo, unategemea kupata mazao gani? Ni kupata mazao waoga, wezi, wanafiki, waongo, vigeugeu, wazinzi, wenye uwezo wa chini sana wa kufikiri, na sifa nyingine zinazoambatana na hizo. Ni shida Tanzania na Afrika!
Watu "mnapigwa" Bodi ya Mikopo kwa uwazi kabisa, mnalia lia badala ya kuchukuwa hatua. Hovyoo!
Pindueni meza 2025; ebo!
Wahamasisheni na wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, majirani meza ipinduliwe 2024 na 2025.
Ninyi ndio wasomi tunawategemea, tunashangaa mnalialia kutafuta huruma; mnaboa mjue eeh!
Andamaneni kwa amani; Daadeki!
Mkipata boom, kazi kushindana kununua tv na subufa na mademu. Tuna wahitimu wa vyuo vikuu wa ajabu sana Nchi hii. Hata ukiingia ofisini, uwezo wao mdogoo! Kutaka pesa za rushwa sasa!
Hata viwango vya elimu vitolewavyo na vyuo vikuu kwa sasa vinatia mashaka na kichefuchefu; wewe kijana anahitimu form IV daraja la IV la pointi 30 huko, anaungaunga na baada ya miaka mitano au sita unamkuta na shahada ya uzamili! Form IV failure! Ndio wakurugenzi na DCs wengi tulionao kwenye H/Shauri na wilaya zetu Nchini. Hii ni through recategorization policy. Ni sheeda!
Halafu hapo hapo wanajiita CHAWA WA MAMA"utawasaidiaje hapo?!!
 
kijana anahitimu form IV daraja la IV la pointi 30 huko, anaungaunga na baada ya miaka mitano au sita unamkuta na shahada ya uzamili! Form IV failure!
kaka hii nimeishuhudia sana. Tunatengeneza wasomi wajinga mnooo sijui itakuaje vizazi vyetu vya huko mbele. Inasikitisha sana.
 
Poleni sana madogo,mikopo inaumiza mgejua mge achana nayo au kufurahia hicho kidogo mnachopata.
 
Moderator asante sana kwa kurekebisha heading.
JF ina impact naona sasa hata inbox msg za waombaji zimerekebishwa. Mfano walikuwa wanatoa msg hii
Conglatulation your application is verified complete wait for ALLOCATION PROCESS

Sasa wanasema: Your application is being processed! which makes sense kuliko hiyo hapo juu ya congratulations!
 
Back
Top Bottom