Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii, mwaka huu tunaanza na chaguzi za serikali za mitaa kwa sababu tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa kwahiyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitogeza.
Hatusemi tukafanye chaguzi za kutumia nguvu hapana, taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi itafuatwa lakini Jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vikae tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza, mwakani tunaenda kwenye uchaguzi mkuu na ule ndiyo wenye vishindo vikubwa basi ikabidi nitoe tu taarifa na kuwaweka 'alert' kwamba hayo mambo yanakwenda kutokea na jeshi hatuna budi kujiweka tayari.