Pre GE2025 Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

Pre GE2025 Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amri nyinginw inayoenda kuvuruga zoezi la uchaguzi.

Circumstantial ameongea neno la kitisho kwa wapigakura.

Rais ambaye anawaambia wanajeshi na wanausalama wajiandae kwa lolote, maana yake yeye na chama chake wamejipanga kuyokabidhi madaraka wakianguankwenye uchaguzi hivyo jeshi lisimamie hilo.

Mark my words, uchaguzi ujao tutawaona mabaka mabaka kwenye vituo vya kura. Hii ni kinyume na Katiba.

Wapenda DEMOKRASIA tunapinga na kulaani kauli ya rais kuwaalika wanajeshi kwenye michakato ya chaguzi. Wanajeshi wasihusishwe na siasa. Inatosha sasa
Samia ana roho mbaya sana
 
Nimeelewa sasa kauli ya member mmoja humu kuwa CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.
 
Amri nyinginw inayoenda kuvuruga zoezi la uchaguzi.

Circumstantial ameongea neno la kitisho kwa wapigakura.

Rais ambaye anawaambia wanajeshi na wanausalama wajiandae kwa lolote, maana yake yeye na chama chake wamejipanga kuyokabidhi madaraka wakianguankwenye uchaguzi hivyo jeshi lisimamie hilo.

Mark my words, uchaguzi ujao tutawaona mabaka mabaka kwenye vituo vya kura. Hii ni kinyume na Katiba.

Wapenda DEMOKRASIA tunapinga na kulaani kauli ya rais kuwaalika wanajeshi kwenye michakato ya chaguzi. Wanajeshi wasihusishwe na siasa. Inatosha sasa
Sijui kwanini Rais hashauriwi. Kwanini iwe uchaguzi tu ndiyo wawe alert na siyo usalama Kwa ujumla?
 
Haja ipo ila Vyama Vya kuleta vurugu marufuku Tanzania hii.
Hakukua na haja ya vyma vingi. Hii imeleta uroho si kwa xhama pinzani wala tawala. Wote ni walewale tu. Bora kingekuwepo kimoja wote mpambane umo umo kuliko hii fedheha inayoendelea
 
Kauli ni njema ispokuwa tunatofautiana kwenye tafsiri tu, "kauli hii inatofauti gani na kauli ya mzazi, ukifanya fujo nitakuchapa!, usifanye fujo "😀!
Hata ukiitafsiri hivyo sasa hapo amayeamini ni mzazi anaogopa mtoto asijekuleta kizaazaa kwa kufanya zaidi ya mzazi au kuharibu kabisa. Anaye aminiwa ni mtoto hajioni kama mtoto ila anaamini yeye na mwenzake ni watoto wa baba mmoja hivyo wanastahili haki sawa bila kaka mtu kujipendelea.

Sasa kivumbi kiko hapo
 
Samia ameshaona dalili ya kushindwa sasa anayaalika majeshi kuja kuokoa chama lake chakavu
 
Leo miongoni mwa habari zinazotawala kwenye vichwa vya habari ni kauli ya Mama Samia Suluhu anapoviasa vyombo vya ulinzi na usalama kukaa chonjo kutokana na uchaguzi uliopo siku za usoni.

Nadhani ingekua sahihi kuziasa tume za uchanguzi kuliko vyombo vya ulinzi na usalama. Kwani hofu ya Serikali hasa ni nini linapokuja suala la uchaguzi?

Hii imekua kawaida ya Serikali zote zilizoingia madarakani kuweka msisitizo na nguvu kubwa kwenye vyombo vya ulinzi wakati wa uchaguzi kuliko hata tume zinazosimamia chaguzi hizo.

Kama hofu ni vurugu, basi hakikisheni chaguzi zinakua za haki. Haki huleta amani; sio mitutu ya bunduki. Wananchi hawatoacha kuhoji endapo itaonekana kuna mawakala wa baadhi ya vyama wanaondolewa vituoni, maboksi ya kura yanabadilishwa kiholela, watu wanarudia kupiga kura na mambo mengi ya kifedhuli yanayofanana na hayo wakati wa uchaguzi.

HAKI HULETA AMANI.
 
Hapo dawa ni kuwaachia tu uchaguzi wao wachaguane wakimaliza maisha yaendelee, kwanini tufike mbali tuvunjane miguu na kura watuibie kisha tufungwe ndani.
Ntawashangaa sana watu wakishiriki uchaguz

Ova
 
KIGOGO alishatutaarifu kwamba jamaa mkae mkao mchukue hii mali tuu hamna namna.
 
Acha kuweweseka hapa. Hakuna cha nini wala nini. Rais wetu mpendwa yupo sahihi kabisa
Yes ni rais wenu mpendwa kwa kuwa anawavumilia nyie mliozoea kuvunja Katiba na sheria na kuhalalisha maisha ya kihalifu kuwa ndiyo staha ya nchi
maana wakati wa uchaguzi hata maadui wanaweza kujipenyeza kutaka kuvuruga amani ya Taifa letu. Kwa hiyo ni haki kwa Mh Rais kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu kuhakikisha kuwa amani na usalama vitakuwepo na kutawala kabla, wakati na baada ya uchaguzi kwa kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vipo chini yake kujiweka sawa na tayari kukabiliana na yeyote au kundi lolote lile linaloweza taka kuvuruga amani ya nchi yetu.
Tanzania ina maadui gani kutoka nje?
Uache ujinga maana usidhani unaongea kitu cha utu bali upuuzi mtupu unaotokana na shibe ya ufisadi.

Kwa hiyo kuna taifa ama mataifa yanapanga kuivamia Tanzania during elections? Rais anamaanisha kuwa raia hawapaswi kabisa kupewa haki yao hata kama kura zao zitaamua kinyume na matarajio yenu hivyo jeshi lijipange. na jeshi halina diplomasia ya kuhoji wao ni kuua na kusonga mbele.

Hizi kauli anazozitoa sasa zitatumika baadaye endapo CCM itafanya wizi wa kura kama ilivyozoea
 
Sijui kwanini Rais hashauriwi. Kwanini iwe uchaguzi tu ndiyo wawe alert na siyo usalama Kwa ujumla?
Agenda kuu ya CCM ni kubakia madarakani. Katibu Mkuu enzi zake Bashiru Ally Kakurwa alishawahi kusema Katu CCM haiwezi kuachia madaraka kwa sababu inamiliki dola na itatumia dola kubakia madarakani.

Spika wa sasa wa Bunge Tulia Akson ameshasema kabisaa kuwa CCM haitokabidhi madaraka kwa yeyote yule hata iweje...

Kauli ya leo ya Rais inatukumbusha kuwa haya ndo malengo na msimamo wa CCM. Hata nchi nzima mpige kura ya HAPANA, hawatoachia ngazi kwa sanduku la kura
 
Hiyo alart sijuwi ina maana gani kwamba wahakikishe ccm inabaki madarakani, Jeshi katika uchaguzi wa ndani linaingiliaje? wao shughuli zao ni mipakani huko kwanini wanaekwa alart chaguzi za ndani mbona kama kuna harufu mbaya
 
Agenda kuu ya CCM ni kubakia madarakani. Katibu Mkuu enzi zake Bashiru Ally Kakurwa alishawahi kusema Katu CCM haiwezi kuachia madaraka kwa sababu inamiliki dola na itatumia dola kubakia madarakani.

Spika wa sasa wa Bunge Tulia Akson ameshasema kabisaa kuwa CCM haitokabidhi madaraka kwa yeyote yule hata iweje...

Kauli ya leo ya Rais inatukumbusha kuwa haya ndo malengo na msimamo wa CCM. Hata nchi nzima mpige kura ya HAPANA, hawatoachia ngazi kwa sanduku la kura
Sidhani kama ni CCM sema watu wachache ambao maslahi Yao yako at stake CCM ikikosa ridhaa...Wapo Wana CCM wengi ambao hatupendi huu muundo wa wachache kujimilikisha nchi huku wakitumia CCM na dola kama cover.

Kauli ya CDF inabeba uzito mkubwa, so kwamfano mtu akawa nda ni ya serikali na kesho ndiyo akawa Rais huku tuna hii Katiba what will follow? Huoni mtu yeyote anayeipenda nchi hii hawezi kutamani hii Katiba kuendelea ku operate?
 
Back
Top Bottom