Pre GE2025 Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa kama umeamua kupoteza kura Yako itakusaidia nini?

Hakuna Rais wa upinzani Tzn hii na wewe unalijua Hili vizuri
We endelea kuwabrand wenye fikra mbadala kuwa ni CDM.

Kama kura yangu moja haina effect basi tuendelee kupuuza mambo ya msingi.

Hatuwezi kama nchi tukaendelea kuamini kuwa fisi ndiye mlinzi bora wa bucha
 
Reactions: Ame

Wewe huna fikra mbadala ila ni hater wa Samia 😆😆
 
Safi na hongera rais wetu mpendwa, idiot might thought negatives, lakini ni kauli safi kabisa na yenye nia safi kabisa katika kuyaweka majeshi yetu tayari dhidi ya wahalifu wa aina mbali mbali, uchaguzi huweza kutumika kama mlango wa mambo mengi ya hovyo hovyo....
Asante mama.
 
Wewe huna fikra mbadala ila ni hater wa Samia 😆😆
Endelea kufurahia na kunufaika na mfumuko wa bei, umeme wa mgao, ubadhirifu na serikali kugenisha tasilimali za nchi kinyume na Katiba.

Wanaopinga hayo, leo mnawaita hatters wa Samia.

Furahi kifutuhi
 
Sijui tulimkosea nini Mungu. Hivi kulikua na haja ya kuwa na vyama vingi kweli?naamini haya yasingekuwepo
Kauli ni njema ispokuwa tunatofautiana kwenye tafsiri tu, "kauli hii inatofauti gani na kauli ya mzazi, ukifanya fujo nitakuchapa!, usifanye fujo "😀!
 
Endelea kufurahia na kunufaika na mfumuko wa bei, umeme wa mgao, ubadhirifu na serikali kugenisha tasilimali za nchi kinyume na Katiba.

Wanaopinga hayo, leo mnawaita hatters wa Samia.

Furahi kifutuhi
Pole sana,Tanzania Ina mfumuko wa bei au unaropoka tuu?
 
Kuelekea maandamano hii ni kauli tata.
 
Maza akumbushwe kuwa TZ ni kisiwa cha amani. Hayo maandalizi wanaotaka kuyafanyia hayahitajiki nchi hii unless wana malengo yao tofauti.
 
Kama uchaguzi ni huru na haki kwa nini CIC awe na matarajio hasi kiasi hicho? Mpaka hapo Rais ameshonyesha dhamira ovu kwa chaguzi zijazo.
 
Acha kuweweseka hapa. Hakuna cha nini wala nini. Rais wetu mpendwa yupo sahihi kabisa maana wakati wa uchaguzi hata maadui wanaweza kujipenyeza kutaka kuvuruga amani ya Taifa letu. Kwa hiyo ni haki kwa Mh Rais kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu kuhakikisha kuwa amani na usalama vitakuwepo na kutawala kabla, wakati na baada ya uchaguzi kwa kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vipo chini yake kujiweka sawa na tayari kukabiliana na yeyote au kundi lolote lile linaloweza taka kuvuruga amani ya nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…