Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Kipindi hicho watendaji walifanya mambo kwa mzuka sana. Ndiyo pamoja na uchomaji nyavu, kupasua mitumbwi, kukamata ng'ombe na kutaifisha za wafugaji, kuvamia account za watu. Kwa ujumla kilikuwa Kipindi kigumu sana.

Leo kote huko kama hawapo?!. Ulikuwa ni upuuzi.
 
Do you really, from the deep bottom of your heart believe the guy could sign off on something like that?
Ukiwa kiongozi mkuu. Mambo yafanyika ya hovyo na hukemei wala kuwawajibisha wahusika. Ni kuwa umeshiriki kutenda jambo hilo.

Kwani Amini aliua watu mwenyewe?! Wasaidizi
 
Kuna namna Hayati Rais Magufuli anachafuliwa kwanini Rais Samia akiri kosa ambalo lilifanywa na Serikali ya ccm ambayo yeye mwenyewe Rais Samia kwa kipindi hicho alikuwa Makamu wa Rais au ndio tuseme bado mzimu wa Rais Magufuli unawaandama.
Yangesemwa mambo maovu ya enzi za Kikwete ni sawa, Ila akiguswa huyo mungu wenu anachafuliwa
 
Yangesemwa mambo maovu ya enzi za Kikwete ni sawa, Ila akiguswa huyo mungu wenu anachafuliwa
Kweli tumefikia kusahau matatizo ya kupanda vitu bei, umeme, maji na tunaongelea vifaranga, serious?

Sawa alifanya makosa, je vifaranga ndio vitaleta umeme au maji?
 
Aliyeagiza vichomwe. Aliyechoma wote walijipalia makaa ya moto.
 
Kweli tumefikia kusahau matatizo ya kupanda vitu bei, umeme, maji na tunaongelea vifaranga,serious?

Sawa alifanya makosa, je vifaranga ndio vitaleta umeme au maji?
Unamaanisha 24/7 tuongee kuhusu umeme na maji tu? Tusiongee kuhusu kitu kingine chochote kile?
 
Unamaanisha 24/7 tuongee kuhusu umeme na maji tu ? Tusiongee kuhusu kitu kingine chochote kile ?
Namaanisha wananchi wanashida zaidi uchomaji wa vifaranga, yeye kama mkuu wa nchi, analeta tumaini gani?

Au majanga yote yanayotekea yamesababishwa na uchomaji wa vifaranga awamu ya tano?

Ni petty issue ambayo anaongea waziri sawa au katibu tawala, wananchi wana shida lukuki.
 
Kwa hiyo hili analizungumzia sasa ili iweje hasa?
Anataka kuwalipa fidia wenye mali, pamoja na kwamba hawakufuata sheria ya kuingiza nchini?

Huyu mama ni pandikizi, ataiumiza sana nchi hii kabla hajaondoka.
 
Nadhani ni katika kutafuta sifa, ndio msukumo wake wa kuibua mambo kama haya wakati huu.
 
Angesema tulikosea kuchoma vifaranga
Hakuna kujitetea kwani wote mtaulizwa siku ya mwisho

Mimi ningekataa kwa kumuogopa Mungu au ningejiuzulu
 
Hii ilikuwa ni biashara haramu.
Waliouza hawakutaka tena kuvipokea, una taarifa hiyo?

Inapotokea hali ya namna hiyo, ni wajibu wa nchi kutumia njia zozote zinazofaa kuzuia kuingiza mali hiyo ambayo inaweza kuleta madhara, kama magonjwa.

Mbadala wa kuchoma ilikuwa ni kuweka karantini, sasa hatujui kama uwezekano huo haukuwepo. Lakini njia ya kuchoma ni halali kabisa katika hali kama hiyo.
 
Walio karibu nae wamwambie afanye yake, yaliyo pita hapaswi kuya zungumza tena kwa sababu kama ni machafu na yeye yana mchafua
 
Taja wezi wa BOT na wako wapi hivi sasa
 
Kwa kauli hizi kama wakenya wako makini wanaweza kuomba fidia. Lakini pia sidhani kama ni sahihi kwa chama tawala kuuponda utawala wa chama tawala uliokuwa unatekeleza sera za chama tawala. Hii ina maana kuwa chama kina mpasuko mkubwa na sasa kila chama kundi linajaribu kujioendekeza kwa wananchi kwa kulichafua kundi jingine. Kimsingi hii mbinu ilipasws ku-backfire kama vichwa vya watz vingekuwa vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…