Rais Samia kakopa trillion 1 kujenga airport, Hospitali, VETA na Depo ya mafuta Zanzibar

Rais Samia kakopa trillion 1 kujenga airport, Hospitali, VETA na Depo ya mafuta Zanzibar

Alafu wadanganyika ndo tutakuja kulipa hiyo pesa [emoji849]
Zanzibar haina uwezo wa kulipa tu bills za umeme wa Tanesco kutoka Bara ndio wataweza kulipa hii mikopo ya matrilioni?

Ni wavuja jasho walalahoi vijijini a mijini Tanganyika wanaokunywa tope ndio watawalipia wapemba airport ya trillion 1
 
Hizi pesa zimekopwa na Tanganyika na Tanganyika ndio italipa

Trillion 1 inaenda kujenga airport Pemba

Ikumbukwe pia katika ule mkopo wa covid, amechukua billion 400 na Tanganyika ikabaki na billion 700

Vile vile ameshachukua mkopo Mwingine WB wenye dhamani ya trillion 1 kwaajili ya zanzibar pia

Note, mikopo hii yote Tanganyika ndio italipa

View attachment 2040768

View attachment 2040766

Ushabiki mwingi

1. Hakuna nchi inaitwa Tanganyika
2. Miradi ni muhimu ni kweli airport ya Pemba ni muhimu kuliko ya Chato. Kwani Chato wana chato wanaweza kulipa? Wapi kuna watalii zaidi!!?
3. Hatujui kiasi gani ni grants ambazo sio mikopo hivyo hatuna habari za kutosha
 
Kibaya zaidi ndani ya miaka 100 sehemu kubwa ya tuvisiwa twenyewe tutakuwa tumemezwa na bahari sababu ya global warming. Wasije wakajisahau sana Tanganyika huku ndo watakakokimbilia.

Na sasa hivi jamaa wako kimyaaaa huwezi kusikia tena fyoko fyoko za sijui kero za muungano wala nini.

Yetu macho!

Siku hizi visiwa vinatengenezwa

Huoni mchina alivyotengeneza
Na sisi tutaboresha baada ya miaka 50

Hii China na USA kaufyata mkia
IMG_3529.jpg

IMG_3528.jpg
 
Ushabiki mwingi

1. Hakuna nchi inaitwa Tanganyika
2. Miradi ni muhimu ni kweli airport ya Pemba ni muhimu kuliko ya Chato. Kwani Chato wana chato wanaweza kulipa? Wapi kuna watalii zaidi!!?
3. Hatujui kiasi gani ni grants ambazo sio mikopo hivyo hatuna habari za kutosha
Uzuri ukienda chato leo ukanunua kiwanja uwe mkazi hakuna atakaetaka kujua umetokea wapi...Zanzibar ukitaka kufanya hilo utatendewa kama muwekezaji kutoka nje ... hii ni fair?
 
Uzuri ukienda chato leo ukanunua kiwanja uwe mkazi hakuna atakaetaka kujua umetokea wapi...Zanzibar ukitaka kufanya hilo utatendewa kama muwekezaji kutoka nje ... hii ni fair?

Kama una nia nzuri kwanini usi lalamikie sheria badala ya kuingiza vitu vingine
 
Mtu kwao jamani!Mimi namsifu kudos mazaa Fanya kweli usidharaulike...jifunze kwa mwendazake aliweka lami mpk sebuleni kwake,Kanda Ya ziwa yote lami!
 
Ushabiki mwingi

1. Hakuna nchi inaitwa Tanganyika
2. Miradi ni muhimu ni kweli airport ya Pemba ni muhimu kuliko ya Chato. Kwani Chato wana chato wanaweza kulipa? Wapi kuna watalii zaidi!!?
3. Hatujui kiasi gani ni grants ambazo sio mikopo hivyo hatuna habari za kutosha
Wengi mnaosema hakuna Tanganyika hamjawahi kufika zanzibar, fika zanzibar ujaribu kuishi kama mtanzania ndio utajua kumbe hizi ni nchi 2 tofauti kabisa

Tukiachana na ubaguzi wa hali ya juu kwa watanganyika kule zanzibar, usichojua ni kwamba wewe ni second citizen kule zanzibar, Huwezi kununua ardhi wala kuimiliki, namna mganda atavyotakiwa kufanya ili amiliki ardhi ndio hiyo hiyo njia utapitia wewe usietaka kusikia Tanganyika
 
Kibaya zaidi ndani ya miaka 100 sehemu kubwa ya tuvisiwa twenyewe tutakuwa tumemezwa na bahari sababu ya global warming. Wasije wakajisahau sana Tanganyika huku ndo watakakokimbilia.

Na sasa hivi jamaa wako kimyaaaa huwezi kusikia tena fyoko fyoko za sijui kero za muungano wala nini.

Yetu macho!
Wapo kimya kwa sababu ni muda wa maakuli.
 
Waache nao wafaidi kwa ujinga wa wadanganyika. Hapo ndiyo utaona umuhimu wa serikali 3. Kwani Tanganyika inafaidika na nini kutoka Zanzibar? Zaidi ni Wazanzibar wanaofaidi na huu muungano na hasa viongozi wa wa serikali wa CCM. Kwa sasa nafikiri wapinzani wa Zanzibar wameambiwa watulie ili Zanzibar ifaidike kwa rais kutoka Zanzibar na 2025 kwa ujinga CCM watampa tena Samia bila kuzingatia upelekaji huu wa pesa upande wa pili ambazo kiuhalisia ni Watanganyika watakaozilipa.

Wabunge wetu wa chama pendwa hawatathubutu kulisemea hilo zaidi ya kupiga meza.
 
Ushabiki mwingi

1. Hakuna nchi inaitwa Tanganyika
2. Miradi ni muhimu ni kweli airport ya Pemba ni muhimu kuliko ya Chato. Kwani Chato wana chato wanaweza kulipa? Wapi kuna watalii zaidi!!?
3. Hatujui kiasi gani ni grants ambazo sio mikopo hivyo hatuna habari za kutosha
No.3, acha uvivu kasome habari yote ya mkopo. Sio hatujui, wewe ndio hujui

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom