Rais Samia kakopa trillion 1 kujenga airport, Hospitali, VETA na Depo ya mafuta Zanzibar

Yapo mambo ya muungano na yasiyo ya muungano, haiwezekani zanzibar iwe na ruhusa ya kukopa separately then bado wapate share kwenye mikopo ya Tanganyika
Nimekuuliza unaelewa unachoongea au huelewi?

Aliyeweka huo utaratibu ni watu wa Bara kwa sababu mliwalazimisha Wazanzibar kwenye Muungano.

Mkiona inawakata rudini kwenye meza ya mazungumzo.It is very interesting kwamba kwa sasa wanaolalamikia terms za Muungano ni WA Bara na sio Wazanzibar kama ilivyokuwa miaka yote 🤣🤣..

Kwa kukusaidia Zanzibar haina exclusive rights za Kukopa kama unavyodai wewe,wakaitaka lazima wa consult serikali ya JMT ila Wana haki ya kupata share kwenye mikopo yote ambayo SJMT inachukua na ndicho Samia anakisimamia .
 



 
Bora huyu anakopa na anaweka wazi na kila mwanachi anajua kama raisi kakopa pesa, kuliko kudanganya wanachi kuwa tunajenga miradi kwa pesa zetu wenyewe ilhali tunajua hadi kikwete anaachia nchi tulikuwa na deni la trillion 39 ila hadi December mwaka (2020) Jana tulikuwa na deni la trillion 54 jiulize kama angemaliza awamu zote mbili deni lingefika kiasi gani na je wanachi tungelipokeaje hilo deni baada ya yeye kumaliza muda wake na ngojera za kutuhadaa kuwa tunajiendesha kwa fedha zetu na Tanzania ni Nchi Tajiri sana

Kwa mujibu wa waziri wa fedha, tulikopa kutoka standard chartered bank trillion 3.3 2019 kwa ajili ya ujenzi wa SGR, ila tukisimama mbele ya wanachi tunasema ni fedha zetu zinajenga, je ni miradi mingapi tulikopa na hatukusema ukweli, je ni fedha kiasi gani zilitumika pasipo kujulikana chanzo chake kama ujenzi wa chato ila tulinyamaza tu ila Leo hii Mmama wa watu Kila anachofanya tunakosoa, bora yake yeye ameamua kuwa mkweli maana sometimes kujua ukweli ni tiba tosha ya satisfaction ya wanadamu

Huyu mama atapata tabu sana maana anaongoza watu ambao walizoea kuongopewa tu mwanzo mwisho bila kuhoji kama Leo manavofanya humu kwenye majukwaa, Kila akijaribu kuwa mkweli watu tunamkosoa maana hatukuzoea ukweli, as long anakopa na kutuambia kwa upande wangu sioni shida maana amekuwa honest na wanachi watajua ukweli kwamba tunadaiwa, na weka record zako sawa sawa mkopo wa covid-19 amepata msamaha
 
Naona watu wamechefukwa sana kwa maendeleo ya ndugu zao
Ila mimi nasema ni sawa tu

Hata ikitokea wakiomba wabadili fedha sawa tu wawe na hela zao
Muungano huu wamechomoa na kuchomeka mambo mengi tu ya muafaka na mengine lazima

Fursa hiyo acha nao wale Keki
Ikiuma unapoza na soda
 
Kelele zote hizi ni matunda ya Zanzibar kuungana na nchi fukara Tanganyika na kuvamiwa kijeshi. Zanzibar ingeungana na Oman kama zamani kwenye historia, leo Zanzibar ingekuwa kama Muscat. Zanzibar ingefaidi utajiri wa mafuta ya Oman. Lakini Zanzibar ilifanya makosa kuungana na Tanganyika matokeo yake tumegawana umaskini na kuoneana wivu na chuki zimezidi.
 
Tanzania ni Muungano wa zilizokuwa nchi 2 za Tanganyika na Zanzibar.

Muungani ukivunjika kila nchi litatumia majina yake ya Tanganyika na Zanzibar
 
Zanzibar si ni nchi na wanakatiba yao..kwanini wasiende kukopa wao.

#MaendeleoHayanaChama
 
tumesha zoea saivi zamu ya pemba baada ya chato, mama kaza
 
Nani kakuambia Airport ya chato haina umuhimu,fuatilia kwanza sio unaongea tu chato ipo mkoa wa Geita na geita kuna Gold mines,izo Gold unadhani zinasafirishwa na nini? ndo Airport inaingia apo
 
Nani kakuambia Airport ya chato haina umuhimu,fuatilia kwanza sio unaongea tu chato ipo mkoa wa Geita na geita kuna Gold mines,izo Gold unadhani zinasafirishwa na nini? ndo Airport inaingia apo
Mkoa wa chato hauundwi tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…