Rais Samia kakubali Tume Huru ya Uchaguzi. Sasa ole wenu mtoke nje tena wakati wa Majadiliano

Rais Samia kakubali Tume Huru ya Uchaguzi. Sasa ole wenu mtoke nje tena wakati wa Majadiliano

Salaam Wakuu,

Nawashauri Wadau wa Siasa, mujifunze kuvumiliana na reconciliation. Si tabia njema kususasusa. Tangu hii tabia ya kususa ianze Kwama 2010, sijaona tija yoyote.

Yaani mnasusia nyani Shamba la mahindi?

Rais Samia Kasikia Kilio chenu cha Tume huru ya Uchaguzi.

Siku taratibu zikikamilika, mkashiriki kwa manufaa ya Nchi sio vyama vyenu.

Natanguliza Shukrani kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu.

Happy New year.
Tume huru ya uchaguzi siyo keki au soda, tume huru hutolewa na katiba ya nchi na katiba ni sheria ya nchi si hisani ya mtu mmoja, usikurupuke jifunze siasa.
 
... kwa dhati ya moyo wako unaamini pana tume huru pale? Jinsi itakavyopatikana na muundo wake automatically sio huru!
 
Hii inayoenda kujazwa wasiojulikana ?!. Tume huru ilitakiwa ije kwa mujibu wa katiba siyo hisani za Rais.

Bila katiba kuidhibiti serikali na watawala kuiingilia tume ni kazi bure.
Comment yako hii iwekewe lamination kisha ijengewe mnara kwenye lango la kuingia ikulu
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Salaam Wakuu,

Nawashauri Wadau wa Siasa, mujifunze kuvumiliana na reconciliation. Si tabia njema kususasusa. Tangu hii tabia ya kususa ianze Kwama 2010, sijaona tija yoyote.

Yaani mnasusia nyani Shamba la mahindi?

Rais Samia Kasikia Kilio chenu cha Tume huru ya Uchaguzi.

Siku taratibu zikikamilika, mkashiriki kwa manufaa ya Nchi sio vyama vyenu.

Natanguliza Shukrani kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu.

Happy New year.
Tunataka katiba mpya
 
Huko Ethiopia baada ya Abiy Ahmed kufanywa waziri mkuu Ethiopia walianza mabadiliko na tume huru ya uchaguzi hadi kiongozi wa upinzani akaitwa toka uhamishoni akafanywa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi lakini nchi bado ikaishia kuparanganyika kwa migogoro mikubwa. Kubadilisha muundo mzima wa utawala kwanza kwa katiba mpya katika mageuzi ni jambo lisiloepukika na linapaswa kuwa la kwanza.
 
Hii itajayojazwa wasiojulikana wanaocheza fair na aliyeshikilia shilingi wanaokaba kuanzia Voters IDs, kuchagua wasimamizi, kufuatilia matokeo, kupiga kura hadi kutangazwa wana mbinu nyingi na wanajitanua na kodi za wapiga kura. Mmmmmmh
 
Taifa na Wananchi sio mali ya mtawala
Maamuzi ya nini Taifa linahitaji ni la Wananchi sio watawala
Tume Huru na Katiba Mpya sio hiyari huruma au hisani toka kwa watawala
Bali ni

Haki ya Taifa
Haki ya Wananchi
 
Kwa Africa ninayoijua mimi,Tume huwa huru kwa aliyeshinda tu.

Ghana pamoja na kutajwa kuwa kinara wa chaguzi huru na haki Africa ila kila uchaguzi aliyeshindwa huyakataa matokeo.

Edgar Lungu alipobwagwa na Hichilema juzi hapa alidai uchaguzi haukuwa huru pamoja na kwamba mkurugenzi wa Tume alimteua yeye miaka miwili kabla ya uchaguzi.

Hata Kenya yenye katiba mpya na muundo mpya wa Tume ya uchaguzi ila bado mambo ni yaleyale tu.

Upinzani wenye nguvu unashika dola kwa Tume yoyote tu hata kama CEO wake ni mke wa Rais.

Tume iliyomtangaza George Weah mshindi haina tofauti yoyote na hii yetu iliyojaa wateule wa Rais.

Tume huru kwa wote haijawahi ku-exist Africa.
 
Usimpangishe mpangaji nyumba yako kwa muda mrefu bila kumbadilisha nymba ataigeuza yake wewe mwenyenyumba utakua mpangaji angalia ma ccm wanavyofanya
 
Kwa Africa ninayoijua mimi,Tume huwa huru kwa aliyeshinda tu.

Ghana pamoja na kutajwa kuwa kinara wa chaguzi huru na haki Africa ila kila uchaguzi aliyeshindwa huyakataa matokeo.

Edgar Lungu alipobwagwa na Hichilema juzi hapa alidai uchaguzi haukuwa huru pamoja na kwamba mkurugenzi wa Tume alimteua yeye miaka miwili kabla ya uchaguzi.

Hata Kenya yenye katiba mpya na muundo mpya wa Tume ya uchaguzi ila bado mambo ni yaleyale tu.

Upinzani wenye nguvu unashika dola kwa Tume yoyote tu hata kama CEO wake ni mke wa Rais.

Tume iliyomtangaza George Weah mshindi haina tofauti yoyote na hii yetu iliyojaa wateule wa Rais.

Tume huru kwa wote haijawahi ku-exist Africa.
Kwa hiyo unapendekezaJe labda ?!. Naona unajaribu kuhalalisha haramu kwa sababu wengine wameshindwa !! AKILI MATOPE
 
Taifa na Wananchi sio mali ya mtawala
Maamuzi ya nini Taifa linahitaji ni la Wananchi sio watawala
Tume Huru na Katiba Mpya sio hiyari huruma au hisani toka kwa watawala
Bali ni

Haki ya Taifa
Haki ya Wananchi
Hili ndilo Ccm hawalijui na hawataki kulijua. Akili zao lazima Rais awe mwenyekiti wao .
 
Back
Top Bottom