Rais Samia: Kama haumpendi Rais aliyeko, penda nchi yako

Yeye mwenyewe hana mapenzi na danganyika zaidi ya kule kwenye urojo......ndo maana kapiga pasu pesa ya uviko ikajenge himaya huko.
hamna ushahidi kwenye hili................na hata kama ipo hivyo ni kwa vile tuu Magufuli alimteua kuwa makamu wake na Maraisi wote wamekuwa wakiiamarisha mambo ya kwao hata kwa uchache tukumbuke hata Chato ipo vile kwasababu gani na ni ndani ya miaka mi5 ya kwanza ......ilishapendeza ,mpeni kijiji basi huku bara abadilishe kabila na ubini...........
 
What if they are not mutually exclusive ?
 
Mi ni chadema kindakindaki lakini najikuta nampenda Mama automatically.,
 
Utakuwa hauko sawa kichwani wewe
 

Watu wangapi Kati ya 60 m
 
Mama piga kazi, Mtangulizi wako Mh. JPM aliwahi kusema kuwa binadamu mwenye husuda hata kama wewe unaoga maji yeye kwa husuda zake atasema unamtimulia vumbi,wengi ya watanzania wanakuunga mkono mama , worry not.

Binadamu tumejawa husuda ambayo hupelekea upofu ndani ya mioyo ya wengi,hata akifanya jema gani hawaoni.


Wazungu wanasema, jealous is like a sand in your eyes ,it can stop someone from seeing things clearly.

#Kazi iendelee
 
Sawa waendelee ameruhusu WAENDELEE KUMCHUKIA.....

Serikali ipo....
Nchi ipo......

#Siempre JMT🙏
 
😍
 
Ndio hulka za binadamu,Musa alichukiwa japo aliwatoa utumwani wana wa Israel. Hata Yesu alichukiwa na Wayahudi japo aliwafanyia mambo mengi na miujiza nyingi.
Watanzania nasi ni binadamu na bahati mbaya tumezoea kutawaliwa na mkono wa chuma na mtu mwenye ndevu.Ila huko mbeleni watu wale wale wanaokuchukia leo,miaka mitatu ijayo wanaweza wakakuelewa.
 
Mi nafikiri aendelee kuchapa kazi. Aachie wasaidizi kumjibia au kumtetea.

Wasio mtakia mema wakigundua kila neno anatafuta fursa ya kujibu, watazidisha mashambulizi na wengi wao hawana cha kupoteza.
 
Uyu mama ni dhaifu sana kila siku ana uongelea u Raisi tu bogus kweli
 
Binafsi simchukii Samia.

Ila kuna baadhi ya mambo yasipokwenda sawa tunakosoa hapa.

Kwa Kikwete nilifanya hivyo.

Kwa Magufuli pia nilikosoa.

Hata kwa samia pia.

Ni mshauri Rais tu kuwa aachane na swala la kutafuta kupendwa .

Yeye afanya mambo sahihi tu akishauriana na washauri yake ila iwe for the National Interest.

Nchi hii ina watu Milioni 60 sio rahisi kila mmoja kumpenda na sio rahisi kila mmoja akaridhika na anachokifanya yeye.

The principle is do what is right always.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…