Hoja na ujumbe umefika.
Matokeo ya upendeleo wa jinsi ya ke uko wazi karne hii ambapo maadili yanamomonyoka kwa sababu mama wamekuwa wanaharakati zaidi kuliko mama walezi wa watoto. Tunachoshuhudia ni vijana wasiozingatia mila na desturi zetu za kiafrika kwa kukosa malezi sahihi wallipokuwa watoto.
Hivyo basi, kuendeleza upendeleo wa jinsi ya ke kutazidisha uhanarakati wao na wakati wa umama wao kupunguza muda wao wa kulea watoto katika mila na tamaduni zetu. Km kumetokea mtindo wasichana kuona fahari ya kuwa "single mother" ati kwa sababu "ndoa ni ndoano".
Tanzania ya kesho inafikirisha hivyo basi, tusilaumu mataifa ya nje kuhusu ndoa za jinsi moja. Naamini nao walipitia katika mifumo ya upendeleo wa jinsi ya kike.
Ikumbukwe kuwa mwanamke aliumbwa kuwa msaidizi wa mwanamme na si vinginevyo. Nanukuu Maandiko Matakatifu:
Mwanzo 2:7, 15, 16, 18, 21- 23 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula. Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
Kwa maandiko hayo mwanamke wajibu wake mkuu ni kumsadia mwanamme kuitunza bustani iliyoumbwa na Mungu (kwa maana ya mazingira yatakayodumisha uhai wake, kijamii - utamaduni na mila; kisiasa; kiuchumi; kiteknolojia, nk) kama ilivyoandikwa: Mwanzo 2:15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.