Tetesi: Rais Samia, kama kuna upendeleo huu wa kielimu kwa Wasichana utaliangamiza Taifa

Ambaye husapoti si unaona hapa kwanini uchukui action na wewe unasema ni mwanaume?
 
Au wakilazimisha mtu awe Engineer wa ndege vipi siku akiangusha ndege?
Hakuna mtu yeyote analazimishwa kuwa chochote na serikali. Serikali inachofanya ni kuondoa au kusahihisha vikiwazo vya kimfumo "systematic" kwa wale wanaotaka kuwa engineer, Doctor, au chochote. Nyie local Andrew Tates mna hoja zilizo mufilisi sana.
 
Kwa sababu haina uwezo wa kuwafuatilia na kuwabeba wote, kwa sababu hivyo ndivyo serikali inavyofanya na inavyotakiwa kufanya mambo yake, kwa vipaumbele. Ndio maana unaona kuna sehemu zinapewa kipaumbele cha miradi mipya ya maji, umeme, barabara, hospitali n.k na maeno mengine hawapewei hivyo vipaumbele kwa sababu serikali inaona wako katika hali nzuri, sasa itashangaza mbunge mwenye kata 9 kati ya 10 zenye maji akianza kulalamika kwa sababu mwenzake mwenye kati 2 kati ya 10 ameongezewa miradi mipya ya maji katika kata zake nyingine 2.
Sasa mbona serikali yako tukufu imechukua maamuzi ya kuwabeba wasichana kabla ya kufanya upembuzi yakinifu na wewe unashangilia? Naona sasa umeanza kujipinga wewe mwenyewe. Bado kidogo tu utanielewa.
 
Bandiko zuri kabisa hili

Wanawapendelea Mabinti Kwny mitihani

Afu matokeo yakitoka wanasema wasichana ndo wameongoza kwa ufaulu[emoji848]
 
Shule nyingi sasa zina mabweni kwaajili ya wasichana.
Wavulana ni kama hawaangaliwi sasa.
Hata mwalimu mmoja wa sekondari aliniambia sasa ni too much.
Wasichana wamekuwa kama special group
 
Kwa namna umeongea umenikumbusha kuhusu story moja ya mashindanonya wanyama ambapo, zoezi la kwanza ilikuwa ni kukwea mti mrefu sana na mshindi apatikane.

Washiriki walikuwa ni tembo, nyani, samaki, nyoka, pundamilia na wengineo. Sasa jiulize hapo hili shindano lilikuwa linalenga nini maana hawa wanyama hawafanani hata kimaumbile na hata mazingira yao je wangeza kufanya jambo moja perfectly?

Jibu ni hapana.

Jamii ya sasa inaamini katika mfumo wa elimu bila hata kiquestion mfumo wa elimu umekuwa structured vipi. Je unaendana na mahitaji yetu, mwisho wa siku unatimiza malengo tunayotarajia.

Je huu mfumo walengwa wake ni akina nani by nature?!

Hivi mfano ukitangaza chuo cha urembo, mapambo ya kike, upishi, na fashion utategemea tuwe na 50/50 registration ya wanafunzi wa jinsia ya kiume na kike. Nini itakuwa target yetu?

Leo tunawaforce hawa mabinti kwenda shule katika mazingira ambayo hata wao hayawa accommodate, ili baada ya miaka 20 tupate nini, and tunawekeza mabilioni ya pesa katika hizi project hasara.

Sio kwamba tunakosea kulazimisha mtoto wa kike apitie trainings zile zile kama wa kiume ili tutegemee matokeo yale yale kwa mtoto wa kike na wakiume?

So mtoto wa kiume anapata hedhi for at least 5 days in a month, plus mtoto wa kike anatakiwa kukeep up na majukumu ya nyumbani sababu ni sehemu ya kumuandaa kijamii kuwa mwanamke, asipofanya hivi hata akimaliza shule unataka kunambia hatokuja kuwa mke wa mtu au mama wa familia so ni wapi wanatoa hayo mafunzo au kumuandaa kwa hilo?!

Kuna sehemu tunakosea aisee. Inabidi huu mfumo wa elimu ufumuliwe tujue tunakosea wapi. Pengine watoto wa kiume na wakike hawatakiwi kusoma at the same system maana kuwaweka sehemu moja why inaonekana kama wakike analazimika kusaidiwa ili awe kama wa kiume why isiwe naturally tu wa kike na wa kiume kuwe na vitu wawe wana click by nature sio human force au society Pressure?

Ina maana kama watoto wa kike wanatakiwa kupewa sapoti na empowerment it means this system kwao sio match they have to deal with another system for them.
 
Ukimpa kazi mwanaume ujue kuna wanawake kibao wananufaika kwanzia atakaeolewa plus wale michepuko sasa mpe ajira mwanamke kwanz hawatak tena kuolewa nakuna mwanaume atanufaika zaid yamchungaji
 
Wewe unasema nini wewe. Hivi mtu achaguliwe kindezi ndezi huku chini halafu aje kuwa na best performance huku juu inawezekana?!
Inawezekana sana tu, hasa kwa course za sayansi, nawajua wengi walilamba 2 na 3 na wakatoka na First class au Upper second with Honors ..
 
Ukimpa kazi mwanaume ujue kuna wanawake kibao wananufaika kwanzia atakaeolewa plus wale michepuko sasa mpe ajira mwanamke kwanz hawatak tena kuolewa nakuna mwanaume atanufaika zaid yamchungaji
Hizo ni personal choices, lakini ni vizur kama taifa tukakuza usawa wa kijinsi na kijinsia kwa manufaa ya kesho.
 
Sasa hapo Kwa hoja yako itakuwa unadahili wanafunzi kwa uwezo wao au kwa kuwaonea huruma. Na je nini matokeo ya kuwaonea huruma?
Ufikirie ufaulu wanafunzi katika mfumo "range" zilikubaliwa na sio "absolutes".

Yani C-A(C, B, B+, A), III-I badala ya F na A tu, au 1 na 0 tu. Kama umefikia chuo unaelewa maana ya GPA, ina range.

Mitihani ya wanafunzi wote huwa inasahihishwa kwa usawa, hakuna ambaye huwa anaongezewa au kupunguziwa maksi.
Utafauti huwa unakuja katika kuwachagua kwenda shule au vyuo, hapo ndipo watasema mwenye III kati ya jinsia mbili mwanamke atapewa kipaumbele, mwenye III kati ya mlemavu, albino na mtu asiye mlemavu hao walemavu ndio wanapewa kipaumbele.

Ni hivyo kwenye mikopo ya HESLB pia japo ni mkopo unaolipwa, ila siku serikali ikiwa na pesa za kuwapa wote wanaotaka hakutakuwa na hivyo vigezo sijui nyumba yenu ni ya makuti, bati au vigae, yatima n.k.
 
Mwanamke hawezi kumshinda Mwanaume, hata apewe favor kiasi gani
Ni kama binadamu kushindana na Mungu, binadamu hawezi kushinda.
 
Kwa hiyo unatengeneza taifa lenye madokta wa kupendelewe?
 
Na wewe ni mama? Basi taifa lina hasara?
 
Inasikitisha. Nchi jhii imaelekea mahali pabaya sana. Miaka michache iijayo kila jamii itakuwa multilineal. Ni shida kubwa!
Marekani na western world sasa wanaanza kulipia. matriarchal society huwa inazalisha vijana dhaifu na very emotional.

Sasa ukute mwanaume wa miraba minne halafu awe soft ndio wale maisha yakiwa magumu anashika gun anakwenda kumiminia risasi watu katika shopping centers au movie theaters, or worse anakuwa Serial killer.

Plus crime rates zinakuwa juu sana katika matriarchal society. Tazama marekani watoto wanaolelewa na familia ambazo ukitrace uzao wao unakuta ni generation ya single mothers kutoka bibi watatu nyuma. Matokeo watoto wanakuwa under disciplined na kuwa na jamii ya hovyo kupigana shaba nje nje, madawa ya kulevya, ubakaji, sodomy, na children molestations plus alot of jailed male members wa familia.

Haya tutakuja yaona hata hapa kwenye jamii hii ya sasa kwasababu ndicho kinachokwenda kutengenezwa na hii serikali pamoja na hawa wanaosapoti kila upumbavu.

Kwasasa wimbi la kwanza limeanza kuzaa hovyo bila Ndoa so its official ndoa imeanza kuwa myth kwa watoto wengi wa kike na wa kiume wameshakata tamaa wanafanya tu ngono na kuzaa ili wasipoteze jina la ukoo basi ndoa ni kero.

Ushoga ndio huo sasa mnaona umesambaa kila mkoa. Matendo ya ulawiti wa watoto tazama taarifa ya habari utajionea uhalisia.

Uhalifu nadhani sote tunajua Panya road tunaona balaa lake. Yote haya in the Span of just 10 and not more than 30 years.

Sasa ipo siku ndipo mtakuja sema Vitabu vya Dini vilikuwa sahihi kuwa mwanamke ni wa kuongozwa na mwanaume na mwanamke anatakiwa kutumia muda mwingi zaidi nyumbani kulea watoto na sio kutanga tanga huko nje akikimbizana na ndoto za alinacha za kuwa tajiri namba moja wa kike.

Upuuzi tu.
 
Niseme tu kuwa hili suala lilikuwepo tangu zamani ingawa miaka ya hivi karbuni liliondolewa km siyo kupungua. Mfano mzuri ni kwa Walimu. Huko nyuma kabla ya kufuta division 4 km kigezo Cha kujiunga na chuo kwa elimu ya Ualimu shule za Msingi (cheti aka certificate) utaratibu ulikuwa hivi;
1) Jinsia ya kiume walitakiwa wawe na division 4 ya point 26 kurudi chini.
2) Jinsia ya kike walitakiwa wawe na division 4 ya point 28 kurudi chini.

Hivyo kwa Mfano huo tu hapo juu ni dhahiri hili siyo jambo geni ingawa linatia ukakasi. Baada ya kuweka limit kuwa Ualimu wa shule za Msingi mwisho iwe division 3 ya point 25 kidogo ndiyo ikaleta usawa. Hata hivyo hadi sasa wanaochukiliwa wengi kuendelea na certificate ya Ualimu shule za Msingi ni tofauti na idadi ya Vijana wa kiume. Mfano, kwa sasa wote mnaweza kuwa na division 3 ya point 23, msichana atachukuliwa kwenda certificate hiyo na wewe mvulana utaachwa iwapo nafasi ni chache.

Hata mimi shule niliyosoma (ilikuwa shule binafsi ya Dini-RC) kwa wanafunzi wa O-level wavunana walitakiwa kufikisha wastani wa 48 wakati wasichana ilikuwa wastani wa 45 ili uweze kutoka darasa moja kwenda lingine. Kwa A-Level ilikuwa ni wastani wa 50 kwa wote bila kujali jinsia.

Mifano ipo mingi sn. Ila kumekuwa na sababu kadhaa zinazotolewa. Zingine unaweza kuona km zina materialize na zingine ni km they don't hold water.
Kwa mantiki hii tusishangae ni kawaida tu.
 
Afadhali umekuja mkuu Zemanda unisaidie kuwaelimisha hawa viumbe. Mwanzoni mtihani wa form II passmark ya kwenda form III ilikuwa marks 30. Baada ya wanafunzi wengi kuonekana wanafeli, serikali ikashusha marks hadi 21 lakini matokeo yakazidi kuwa mabaya. Ndipo wakashusha tena hadi marks 18 na bado wanafunzi wakaendelea wanafeli. Baadaye wakaona isiwe taabu.....waliofeli wote waendelee tu na masomo ya form III. Matokeo yake sasa wanafunzi hawajitumi tena kusoma kwa kuwa hawaogopi chochote......upass, ufell, unaenda form III. Hatimaye sasa mtihani wa FTNA hauna maana tena na watoto wamerelax hawasomi. Ndio maana utashangaa watoto wakienda sekondari wakiwa hawajui kusoma wala kuandika kwa sababu ya ujinga huu wa kulegeza mambo katika elimu kwa misingi ya kijinsia na kutafuta kiki za kisiasa.

Na kwa kuwa sasa wamezoea kubebwa tutegemee kupata digriii nyingi za chupi na hawo wanawake wakipatahizo digrii za chupa watakuja hapa mtaani kutusumbua na wengine wataenda kazini na ku-undeperform na hatimaye kushusha productivity. Na matokeo haya sharti yatamgusa kila raia, hata wale ambao wanashabikia upumbavu huu hii leo. It is just a matter of time. Namsubiri mkuu Mpwayungu Village aje atie neo hapa maana ana ujuzi mkubwa kwenye masuala ya elimu
 
Wakati wanaume wanapendelewa Taifa halikuangamia ila litaangamia baada ya wanawake kupewa kilicho Chao? [emoji2957][emoji2957]
Wewe unavyoona hali ya ustawi wa jamii miaka ya uhuru na sasa ni sawa?! Hebu tumia akili kidogo au ndio wale madogo wa kuzaliwa 2000 unabishana na watu tulioshuhudia babu akiwa na nguvu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…