Mkuu 'Nsanzagee', mimi sikulaumu wewe kwa maoni yako uliyo wasilisha kwenye mada yako; pamoja na kwamba msingi wa mada hiyo sikubaliani nao.
Ninachokubaliana nawe ni maoni kama hili uliloliweka katika mstari nilionukuu hapo juu.
Sasa naomba nikuulize swali: wewe unadhani "tutajikomboa" lini, na kwa njia zipi? Kwenda kwako kufanya kazi Israel kwa muda na kupata utakachopata huko, inawezekana ikawa nafuu kidogo kwako kwa muda, lakini utakaporudi hapa utaikuta hali ni hiyo hiyo kama ulivyo iacha kama hatutachukua hatua zaidi ya hizi tunazofanya sasa za kutegemea kuwapeleka nguvu kazi wetu huko nje.
Hivi Israel kuna kipi hasa cha ziada tusichoweza kuwa nacho sisi hapa?
Ardhi nzuri sana tunayo. Maji yapo chungu nzima.
Ni nini hasa kinachokosekana hadi kilimo chetu kisiwe na manufaa kuweza kutusaidia kama kinavyo wasaidia hao Israel?
Naona hapo juu tayari uazungumzia ukosefu wa mitaji ya kuwekeza; na pengine utaalam wa kilimo kama walivyo vavyo Israel.
Kwa nini sis tusiwe navyo hivi? Tuna chuo kikuu cha Sokoine, na vyuo mbalimbali nchini, na kila mwaka watu wanahitimu huko. Hiyo elimu ya kilimo ya Israel wao wanaipata wapi?
Ngoja nimalize: Mazao yanayozalishwa kwa mazingira kama yalivyo Israel, yasingeweza kamwe kushindana na mazao yetu katika soko; kwa sababu mazao yetu yangekuwa na bei nafuu zaidi ya hiyo wanayouzia Israel
Kwa hiyo, sikulalamikii wewe katika msimamo wako wa kutaka kwenda kuwa kibarua. Ninawalalamikia hao wanaokunyima fursa ili usijitoe kwenda kuwa manamba. Na ninakuomba hili ulifikiri vizuri hata wakati ukiwa huko Israel.