Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

Raisi kaongea leo na Polisi na kuwaambia Camera za barabarani zinakuja. Mimi nazijua hizi Camera vizuri na nilifanikiwa kuishi Houston, Texas wakati zikiwepo. Haya ni mambo ya kuangalia na serikali iwe muhimu

1. Angalieni sana faini na mfumo wake. Mkiweka faini kubwa mtaongeza malalamiko sana kwa wananchi wakati hakuna mifumo mingi ya barabarani.

2. Watanzania wengi waendesha magari na wananchi hawaheshimu sheria hivyo toeni elimu.

3. Serikali muwe makini na mkataba na kampuni. Kuna kampuni zinafunga camera na kutaka asilimia fualani kwenye malipo muwe makini na hilo. Ni bora muweke wenyewe badala ya kutoa 30% ya mapato kwa kampuni! Hizi kampuni za Camera zinajua sana kuhonga. Moja ya kampuni kubwa ina makao makuu San Antonio, Texas ilikuwa inahonga hadi hapa USA.

Lakini kitu kingine huu mfumo ili ufanye kazi ni lazima sheria zirekebishwe mfano mtu asiko lipa faini inakuwaje? Wakati sheria zinatungwa hizi teknologia walikuwa hawazijui.
 
Asante bwana Kamundu!

Unashauri kipi kifanyike hapo kwenye asilimia za makusanyo kama serikali haiwezi kugharamia ufangaji na uendeshaji
 
Faini lazima ziwe kubwa ili watu wafuate sheria faini iaiyoumiza ni utani
 
Sawa nishaandaa nguo na mapozi yangu ya kutosha.. ziwe tu lens nzuri.
 
Faini lazima ziwe kubwa ili watu wafuate sheria faini iaiyoumiza ni utani

Ndiyo maana upo kwenye keyboard. Ni wapi umeona faini kubwa zinatowesha makosa.?

Tunasheria hadi zitoazo adhabu za kifo, achilia mbali maisha na kifungo cha muda mrefu.

Umeona makosa yameacha kufanyika?
 
Tuna sheria kuu inayosema kutokujua sheria si kigezo cha kufanya kosa.

Eti waweke faini rahisi kisa watu wamezoea kufanya makosa, no, tutajifunza mbele ya safari, tukifanya kosa weka bill ya faini kwenye bank au simu zetu, nikiweka hela fyeka deni kidogo kidogo. Lazima tustaraabike bwana , pia itapunguza polisi kutudai rushwa.

Cha msingi ni kusimamia uhalisia wa makosa na kuweza kuachia hizo videoz, Wamarekani wanaweka wazi video za matukio ya uhalifu na uvunjaji wa sheria. They should do the same for transparency.
 
Ndiyo maana upo kwenye keyboard. Ni wapi umeona faini kubwa zinatowesha makosa.?

Tunasheria hadi zitoazo adhabu za kifo, achilia mbali maisha na kifungo cha muda mrefu.

Umeona makosa yameacha kufanyika?
Likely tungekuwa worse bila hizo sheria, lawless country is a failed country.
 
Naishauri serikali; Kwa kuwa teknolojia ya sasa imeenda mbali zaidi, licha ya hizo camera za barabarani, kila polisi avalishwe kamera ya mwilini ambayo itaambatana na kila kesi na kila faini. Askari ambae kamshika mtu au kamlamba faini bila kuwasha kamera iwe hakuna kesi na askari aadhibiwe kisheria.

Kamera hizi zimekuwa bei ya kawaida sana, kiasi serikali haitashindwa kuzinunuwa. Na zina rekodi na kupeleka data zote makao makuu, kwenye file la huyo askari na hiyo kesi:

1693864904281.png

Katika vifaa vya polisi, kamera ya mwili au kamera inayoweza kuvaliwa, pia inajulikana kama video ya mwili (BWV), kamera ya mwili (BWC), au kamera ya mwili, ni mfumo wa kurekodi sauti, video, au picha unaotumiwa na polisi kurekodi matukio ambayo maafisa wa utekelezaji wa sheria wanahusika, kwa mtazamo wa afisa aliyevaa. Kwa kawaida huvaliwa kwenye torso ya mwili, iliyobandikwa kwenye sare ya afisa. Kamera za mwili wa polisi mara nyingi ni sawa na kamera za mwili zinazotumiwa na raia, wazima moto, au jeshi, lakini zimeundwa kushughulikia mahitaji maalum yanayohusiana na utekelezaji wa sheria. Kamera za mwili zilivaliwa kwanza na polisi nchini Uingereza mnamo 2005, na tangu wakati huo zimepitishwa na idara nyingi za polisi na vikosi ulimwenguni.

Soma zaidi: Police body camera - Wikipedia
 
Kwa kweli walete tu
Maana hawa madaladala na bodaboda sijui bajaji, wanatukosesha raha ya kuendesha magari yetu mazuri....na pia ziwepo za camera za siri ambazo matrafiki hawazijui ili tuwakamatishe..
Hizo za siri si nunuwa yako binafsi. Zipo mtandaoni aina nyingi tu.
 
Bila kubadili Mfumo wa elimu, Uongozi bora+uwajibikaji+nidhamu kwa raia+ uzalendo hayo yote wafanyayo ni kazi bure, kuna wahuni watang'oa hizo camera zenu wakaziuze kwa mafundi.
 
Sasa ndio wakati wa ku clone plate numbers za magari ya michepuko ya Mawaziri halafu natembea usiku kama kawaida yangu nikipigwa kamera tiketi watailipa wao.

Huwezi kuwa na Mabams millioni ishirini rasta za kuvunja vunja millioni hamsini Matrafiki wamezagaa mabarabarani na kila mmoja anakupiga mkwala wa kukubambikia tiketi hadi umtoe.

Nikaamua kutembea usiku na sasa wamekuja na huu mradi wa TRA ya polisi kukusanya mapato.
 
Bila kubadili Mfumo wa elimu, Uongozi bora+uwajibikaji+nidhamu kwa raia+ uzalendo hayo yote wafanyayo ni kazi bure, kuna wahuni watang'oa hizo camera zenu wakaziuze kwa mafundi.
Something is better than nothing.

Huwezi kungoja watu wote waelimike ndiyo ufanye maendeleo. Haijawahi kutokea duniani hiyo dhanna yako.

Hata sheria zipo lakini si wote tunaozijuwa na si kisingizio cha kufanya makosa kwa kuwa huijuwi sheria.

Hiyo yako ni akili ya ubishi wa "nini kilianza kwanza, yai au kuku".
 
Naishauri serikali; Kwa kuwa teknolojia ya sasa imeenda mbali zaidi, licha ya hizo camera za barabarani, kila polisi avalishwe kamera ya mwilini ambayo itaambatana na kila kesi na kila faini. Askari ambae kamshika mtu au kamlamba faini bila kuwasha kamera iwe hakuna kesi na askari aadhibiwe kisheria.

Kamera hizi zimekuwa bei ya kawaida sana, kiasi serikali haitashindwa kuzinunuwa. Na zina rekodi na kupeleka data zote makao makuu, kwenye file la huyo askari na hiyo kesi:

View attachment 2739246

Katika vifaa vya polisi, kamera ya mwili au kamera inayoweza kuvaliwa, pia inajulikana kama video ya mwili (BWV), kamera ya mwili (BWC), au kamera ya mwili, ni mfumo wa kurekodi sauti, video, au picha unaotumiwa na polisi kurekodi matukio ambayo maafisa wa utekelezaji wa sheria wanahusika, kwa mtazamo wa afisa aliyevaa. Kwa kawaida huvaliwa kwenye torso ya mwili, iliyobandikwa kwenye sare ya afisa. Kamera za mwili wa polisi mara nyingi ni sawa na kamera za mwili zinazotumiwa na raia, wazima moto, au jeshi, lakini zimeundwa kushughulikia mahitaji maalum yanayohusiana na utekelezaji wa sheria. Kamera za mwili zilivaliwa kwanza na polisi nchini Uingereza mnamo 2005, na tangu wakati huo zimepitishwa na idara nyingi za polisi na vikosi ulimwenguni.

Soma zaidi: Police body camera - Wikipedia
Serikali yako ya KIHALIFU ya CCM kamwe haiwezi kukubaliana na hilo, nimekaa pale nachakata..
 
Back
Top Bottom