Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Kujiridjisha ni muhimu jawezi kuchukuwa hatua bila kuwa na ushahidi wa kutosha pili, hizo invoice zinapitia mikono mingi saana kwa wote walikosea ama kazi ya procurement inafanywa na mtu mmoja. Anyway yusubiri report ya TAKUKURU
Hizo ndio loopholes zinazotumiwa siku zote na mara zote upigaji unapofanywa !!
 
Imagine unamtoa mwizi kwenye nyumba kubwa na kumpeleka kwenye nyumba ndogo ukihisi unamkomoa, wakati zile pesa alizoiba bado anazo ndani, na mwisho wa mwezi anaendelea kupokea mshahara kutoka kwa aliowaibia.
Hatar sana
 
Kwakweli !!
 
CCM ni janga kubwa Sana hapa nchini.

Solution ya hiyo "laana" ni kuipiga chini CCM katika uchaguzi ujao
Uzuri wa CCM Siku zote huwa hawategemei kura Ili kuwepo madarakani..... That's why hawataki uwepo wa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.
 
Uzuri wa CCM Siku zote huwa hawategemei kura Ili kuwepo madarakani..... That's why hawataki uwepo wa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.
Hakuna marefu yasiokuwa na ncha. Waibe watakavyo, lakini kuna siku mambo yatabadilika tu.
 
sikiliza ndugu rais anafanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni hawezi kujurupuka ti na kufukuza watu hovyo
 
Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Na mimi inanitia shaka kwamba huyu Bi mkubwa kuendelea kulakamika tu kama raia wa kawaida wa mtaani isijekuwa anatupiga changa la jicho kumbe lao ni moja pamoja na hao mafisadi na wabadhirifu wa pesa yetu.

Mama asitake kituaminisha kwamba cheo chake amekipata kwa bahati mbaya, inampasa akitendee haki cheo chake, haiwezekani Wananchi tunalalamikia shida na Ugumu wa maisha ilhali kuna watu wanakwapua billions of Shillings zetu na iishie kuwasema tu kwenye podium na habari iishe kirahisi hivyo!!,

Our beloved Mom, with due respect, you seriously need to take concrete actions in accordance with the laws to pin those swindlers of Our money. Those culprits are tarnishing your political image not only within but also outside the country.
 
sikiliza ndugu rais anafanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni hawezi kujurupuka ti na kufukuza watu hovyo
Sikatai kwamba anafanya kazi kwa kuzingatia sheria. Lakini kama mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali amegundua kuwa kuna upotevu wa mamilioni ya pesa katika ofisi za serikali anayoiongoza, kwanini asiagize watuhumiwa waliohusika na upotevu huo wasimamishwe, wachunguzwe na ikibainika kuhusika na upoteaji huo wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria zetu?

Kwanini ashauri watuhumiwa wahamishwe ofisi au washushwe tu vyeo eti wakateseke? Hiyo ndio njia ya ku deal na mafisadi na ukawamaliza kweli?
 
Hajalalamika ametoa maagizo! Tusubiri utekelezaji kwa wasaidizi wake!

Sema rais kuna sehem hata mimi sijamuelewa anasemaje mtu aliyeharibu ahamishwe? Aende wap wanapopendwa kuibiwa? Serikal yote ni ya watz na kodi zote ni zetu iwe pemba au chato!
Kuna alosema warudishe walichoiba au wapelekwe mahakaman!yaan sijaelewa akirudisha anakua siyo mwizi ila alijikopesha au? Manake utakua mchezo acha niibe ntarudisha nikishtukiwa
 
Kama atashindwa kuchukua hatua katika hili, basi haina haja kwa siku zijazo kuwa wanatuonesha hotuba zake huko Ikulu. Maana hazina faida wala tija kwetu kuzisikia.

Sana sana anatuumiza mioyo kwa kugundua kuwa tunaibiwa bila wezi wetu kuwajibishwa.
 
Kwa upole huu wa Samia, Yawezekana ni njia ya CCM kuchota pesa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2025.
 
Kama atashindwa kuchukua hatua katika hili, basi haina haja kwa siku zijazo kuwa wanatuonesha hotuba zake huko Ikulu. Maana hazina faida wala tija kwetu kuzisikia.

Sana sana anatuumiza mioyo kwa kugundua kuwa tunaibiwa bila wezi wetu kuwajibishwa.
Chukua wewe hatua
 
CCM ni janga kubwa Sana hapa nchini.

Solution ya hiyo "laana" ni kuipiga chini CCM katika uchaguzi ujao
Nafikiri wengi tulisema JPM alikuwa mukali sana tukatamani Rais anaendesha nchi kwa sheria za nchi. Sheria hazisemi rais akiona mtu kaiba, basi amutaje hadharani alafu aamulishe afungwe jela. Wa Tz tunapenda kubembelezana ndo ustarabu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…