Rais Samia kaona hatari ya Sukuma gang na CHADEMA kuungana, anawatenganisha

Simaanishi muungano rasmi wa vyama vya siasa, muungano wa ku share na kusambaza taarifa hasi dhidi ya serikali mtandaoni na mtaani

Haya makundi mawili, Sukuma Gang na Chadema ni maadui wakubwa sana kisiasa, hasa ukizingatia utawala wa Magufuli ulivyofanya unyama mkubwa kwa Chadema

Lakini hivi sasa haya makundi yanaunganishwa na kitu kimoja, kumpinga Samia

Licha ya uhasama walio nao wanaweza kusahau yaliyopita na kuungana na kuunda Timu kali ya propaganda mtandaoni

Propaganda za mtandaoni zina nguvu sana kama zikiwa organized,

Sukuma gang walikuwa sehemu ya kundi lililoitwa MATAGA na walijijenga sana kipindi cha Magufuli kusambaza propaganda za kuisifu serikali
Chadema nao wana mtandao mkubwa online na wakiungana na hao maadui zao, Serikali ya Samia itakuwa na wakati mgumu

Sasa Samia naona kama ameshtuka, anawavuta Chadema mdogo mdogo, na anaweza kuwapa haki ambazo ziliporwa na Magufuli

Hili litafanya Chadema wamuone Mama kama mtu muungwana na anayestahili kuungwa mkono huku wakiendelea kumlaani Magufuli

Litafanya Sukuma gang wataona Chadema na CCM ya Samia kama kitu kimoja na watakuwa wanawaahambulia wote, utakua mpango mzuri wa kuwazuia kuungana S

Je atafanikiwa? Kikwazo cha huu mpango ni Chadema ya sasa kutekwa na wanaharakati na sidhani kama Mbowe anaweza kuwadhibiti kwa 100%
Kikao cha CHADEMA kinachokuja ndo kitahitimisha ama kuipangua hoja hii.

Mimi naomba tu wawatimue wale wabunge 19 ili ngoma inoge.

Huu ni wakati wa kuikomboa Tanzania na siyo muda wa kuikomboa CCM
 
Supporter's wengi wa Chadema tunamuunga mama mkono na miguu, hatuwezi kuungana na genge la wauwaji.
Wow..!!

So, no need ya Katiba Mpya!

Samia mpaka 2030?!

Wacha utani.
 
Wow..!!

So no need ya Katiba Mpya!

Samia mpaka 2030?!

Wacha utani.
Freeman Mbowe alikuwa na kikao na Rais jana Ikulu, hivi mnataka Rais wa aina gani?

Au mnadhani hawa watu wanakutana tu kujifurahisha, tusipojifunza kuona dhamira njema kwa wenzetu basi hata na sisi ni vigumu kuaminika.

Hakuna kipindi kizuri kwa ajenda nyingi za upinzani kupenyezwa kama kwenye utawala wa huyu mama.

Hata hao Covid 19 waliokuwa wanawasumbuwa huenda tayari kimeeleweka inasubiliwa process tu baraza kuu na kupeleka majina mapya kwa spika wa bunge.
 
Huyo sio supporter wa chadema ni mlamba asali. Supporter wa chadema atasupport chadema na sio chama tawala
Hapa ndio mnafelisana makamanda, hapa namsapoti mama individual, mimi siyo mwanachama wa Chadema lakini tangu nimeanza kupiga kura ni opposition tu, nilimpigia Lamwai, nilimpigia Mrema, nilimpigia Lipumba Chadema hawakuwa na mgombea Urais, nilimpigia Freeman Mbowe, nilimpigia Dr Slaa, nilimpigia Lowasa.

Mgombea wa ccm niliyewahi kumpigia kura ni mzee Mwinyi peke yake na hapakuwepo na vyama vingi.

Siasa zenu za kiharakati haziwasaidii, halafu mimi huwa nachaguwa mtu sichagui chama, mama akienda vizuri naweza kumpigia kura vilevile 2025.

Mimi niko hivyo kama ulikuwa unaniangalia kwa woga yani hivyo ndivyo mimi nilivyo, sitaki utumwa wa vyama.
 
Freeman Mbowe alikuwa na kikao na Rais jana Ikulu, hivi mnataka Rais wa aina gani?

Au mnadhani hawa watu wanakutana tu kujifurahisha, tusipojifunza kuona dhamira njema kwa wenzetu basi hata na sisi ni vigumu kuaminika.

Hakuna kipindi kizuri kwa ajenda nyingi za upinzani kupenyezwa kama kwenye utawala wa huyu mama.

Hata hao Covid 19 waliokuwa wanawasumbuwa huenda tayari kimeeleweka inasubiliwa process tu baraza kuu na kupeleka majina mapya kwa spika wa bunge.
Kwanza utambue lengo la kuanzishwa Chadema sio kukutana na Rais yoyote ikulu, Chadema kama chama cha siasa kinaanzishwa ili kutimiza matakwa yake kwa kufuata sheria ili kufikia lengo walilojiwekea - kushika madaraka. Kwenda ikulu kama kukiwepo, kuwe kusalimiana tu lakini sio kubembelezana.

Huko kwenda ikulu unakokufurahia kunatokea kama matokeo ya mmoja wao kuamua kutofuata sheria na kujifanyia mambo yake kwa mapenzi yake, kwasababu tu ana mamlaka.

Mfano wa hili ni kutoruhusu mikutano ya vyama vya siasa kunyume cha sheria. Hili lilianzia kwa Magufuli lakini linaendelea mpaka kwa Samia wakati ana mamlaka ya kuondoa hii hali, na wala sio lazima mpaka kwenda ikulu kubembelezana, Covid 19 the same.

Sasa nakushangaa wewe unaefurahia safari za Mbowe kwenda ikulu lakini hukemei kwa nini Rais hafuati sheria, ubongo wako umefunikwa na mahaba huyaoni tena haya, ndio maana unaitwa chawa, wake up.
 
Hapa ndio mnafelisana makamanda, hapa namsapoti mama individual, mimi siyo mwanachama wa Chadema lakini tangu nimeanza kupiga kura ni opposition tu, nilimpigia Lamwai, nilimpigia Mrema, nilimpigia Lipumba Chadema hawakuwa na mgombea Urais, nilimpigia Freeman Mbowe, nilimpigia Dr Slaa, nilimpigia Lowasa.

Mgombea wa ccm niliyewahi kumpigia kura ni mzee Mwinyi peke yake na hapakuwepo na vyama vingi.

Siasa zenu za kiharakati haziwasaidii, halafu mimi huwa nachaguwa mtu sichagui chama, mama akienda vizuri naweza kumpigia kura vilevile 2025.

Mimi niko hivyo kama ulikuwa unaniangalia kwa woga yani hivyo ndivyo mimi nilivyo, sitaki utumwa wa vyama.
Ona sasa unavyokosa msimamo.

Pale juu ulisema; "supporters wengi wa Chadema tunamuunga mkono mama", ndio maana nikashangaa kwa hiyo kauli yako, ila umebanwa kidogo umeshabadilika unadai uko "individual" labda kule juu ulivyoweka neno "tu" ulikuwa hujui maana yake.
 
Simaanishi muungano rasmi wa vyama vya siasa, muungano wa ku share na kusambaza taarifa hasi dhidi ya serikali mtandaoni na mtaani

Haya makundi mawili, Sukuma Gang na Chadema ni maadui wakubwa sana kisiasa, hasa ukizingatia utawala wa Magufuli ulivyofanya unyama mkubwa kwa Chadema

Lakini hivi sasa haya makundi yanaunganishwa na kitu kimoja, kumpinga Samia

Licha ya uhasama walio nao wanaweza kusahau yaliyopita na kuungana na kuunda Timu kali ya propaganda mtandaoni

Propaganda za mtandaoni zina nguvu sana kama zikiwa organized,

Sukuma gang walikuwa sehemu ya kundi lililoitwa MATAGA na walijijenga sana kipindi cha Magufuli kusambaza propaganda za kuisifu serikali
Chadema nao wana mtandao mkubwa online na wakiungana na hao maadui zao, Serikali ya Samia itakuwa na wakati mgumu

Sasa Samia naona kama ameshtuka, anawavuta Chadema mdogo mdogo, na anaweza kuwapa haki ambazo ziliporwa na Magufuli

Hili litafanya Chadema wamuone Mama kama mtu muungwana na anayestahili kuungwa mkono huku wakiendelea kumlaani Magufuli

Litafanya Sukuma gang wataona Chadema na CCM ya Samia kama kitu kimoja na watakuwa wanawaahambulia wote, utakua mpango mzuri wa kuwazuia kuungana S

Je atafanikiwa? Kikwazo cha huu mpango ni Chadema ya sasa kutekwa na wanaharakati na sidhani kama Mbowe anaweza kuwadhibiti kwa 100%
Mawazo yako tu.Tukukatalie wakati ndivyo ulivyowaza?
 
Kwanza utambue lengo la kuanzishwa Chadema sio kukutana na Rais yoyote ikulu, Chadema kama chama cha siasa kinaanzishwa ili kutimiza matakwa yake kisheria ili kuelekea lengo walilojiwekea - kushika madaraka.

Huko kwenda ikulu unakokufurahia kunatokea kama matokeo ya mmoja wao kuamua kutofuata sheria na kujifanyia mambo yake kwa mapenzi yake, kwasababu tu ana mamlaka.

Mfano wa hili ni kutoruhusu mikutano ya vyama vya siasa kunyume cha sheria. Hili lilianzia kwa Magufuli lakini linaendelea mpaka kwa Samia wakati ana mamlaka ya kuondoa hii hali, na wala sio lazima mpaka kwenda ikulu kubembelezana.

Sasa nakushangaa wewe unaefurahia safari za Mbowe kwenda ikulu lakini hukemei kwa nini Rais hafuati sheria, ubongo wako umefunikwa na mahaba huyaoni tena haya, ndio maana unaitwa chawa, wake up.
Huyo ni kumpuuza alafu ni kama hajiamini. Kwani akisema mm ni supporter wa CCM nani atamkataza ikiwa ni hiari yake.
Anamaanisha mbowe kwenda ikulu, basi chadema haipaswi kuendeleza siasa zake za kushika dola. Chadema na mbowe walienda ikulu kwa JK, lakini bado 2015 walitaka kuitoa madarakani.
 
Ona sasa unavyokosa msimamo.

Pale juu ulisema; "supporters wengi wa Chadema tunamuunga mkono mama", ndio maana nikashangaa kwa hiyo kauli yako, ila umebanwa kidogo umeshabadilika unadai uko "individual" labda kule juu ulivyoweka neno "tu" ulikuwa hujui maana yake.
Supporter wa chadema Ila anaahidi kumpigia kura mgombea wa CCM[emoji23][emoji23][emoji23], inashangaza kwa huyu supporter.

Hakuna supporter wa hivi, Ila ni hajiamini tu.
 
Hata samwel sitta aliungana na akawapa mileage ya kumshambulia lowasa, mwisho wa siku wakaenda na lowasa wakimsafisha huku sitta akionekana alikuwa na chuki binafsi.

Magufuli aliwajua hao ni watu wa maslahi. Sifa za upinzani wa tanzania;
1. Hawana misimamo inayodumu.
2. Ukiwapa nafasi ya kufanya siasa huru ujue umewapa mbegu ya uharibifu wako hata JK anajua.
3. Ni wapinzani wa majira, kwamba huwa wapinzani wakikosa fursa za ulaji na upigaji.
4. Wengi wamegeuza vyama vyao vya siasa kama vitega uchumi vyao ndio maana vina turn over kubwa ya maafisa waandamizi wa vyama vyao maana huwa wanapishana linapokuja suala la ulaji.
Kwa hiyo Sukuma Gang mna mkakati gani wa kumkabili Samia kulinda legacy? Au ni Umoja Party?
 
Hapa ndio mnafelisana makamanda, hapa namsapoti mama individual, mimi siyo mwanachama wa Chadema lakini tangu nimeanza kupiga kura ni opposition tu, nilimpigia Lamwai, nilimpigia Mrema, nilimpigia Lipumba Chadema hawakuwa na mgombea Urais, nilimpigia Freeman Mbowe, nilimpigia Dr Slaa, nilimpigia Lowasa.

Mgombea wa ccm niliyewahi kumpigia kura ni mzee Mwinyi peke yake na hapakuwepo na vyama vingi.

Siasa zenu za kiharakati haziwasaidii, halafu mimi huwa nachaguwa mtu sichagui chama, mama akienda vizuri naweza kumpigia kura vilevile 2025.

Mimi niko hivyo kama ulikuwa unaniangalia kwa woga yani hivyo ndivyo mimi nilivyo, sitaki utumwa wa vyama.
Lengo la kuanzishwa chadema ni kushika dola. Raisi kukutana na upinzani sio hisani.

Lakini pia unaweza kusupport CCM na raisi wake bila tatizo lolote, maana ndio Uhuru wengi wanaupigania. Ni hiari yako, Ila usilazimishe wengine Wala kuwasemea wengine acha kila mtu awe upande anaoutaka
 
Mnasahau sisi, MATAGA na Sukuma Gang, sote ni wanasisiem.

Tanzania tuna kundi la wapigaji wanaojiita wapinzani.

2025 msijekulialia tumewaibia kura.
Kwa hiyo mmekubali yaishe na sasa mnamuunga mkono mama sio kutetea legacy tena?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Hakuna ambae yuko tayari kuungana na sukuma gang...wale ni wapuuzi wachache waliokuwa na illusion kuwa wao ni wengi..sukuma gang wakajiunge na suma jkt
 
Supporter wa chadema Ila anaahidi kumpigia kura mgombea wa CCM[emoji23][emoji23][emoji23], inashangaza kwa huyu supporter.

Hakuna supporter wa hivi, Ila ni hajiamini tu.
Cha ajabu kitu gani hapo? nyinyi ni watoto wa juzi mmetoka vyuoni na kurukia tu kujiita wanaharakati wakati uwezo wenu mdogo wa kuchanganuwa mambo.

Mimi si wa kwanza wala wa mwisho ngoja nikuingize darasa dogo tu la siasa.

Baba wa Taifa JK Nyerere kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 alimfanyia kampeni mgombea ubunge wa Nccr Mageuzi Paul Ndobho na yeye binafsi alitamka wazi kura yake ya ubunge atampigia Balozi Ndobho na alishinda ubunge kwenye jimbo la Baba wa Taifa la Musoma vijijini kabla halijagawanywa na kuzaliwa jimbo la Butiama.

Pili tukienda kwenye nchi iliyomfano wa kidemocrasia duniani Mrepublican Collin Powel alitamka wazi anamuunga mkono mgombea wa Democratic Barrack Obama na kura yake atampa Obama na alifanya hivyo.

Maalim Seif alimuacha mgombea wake Urais wa ACT na alimuunga mkono Tundu Lisu hamkuliona hilo?

Ni kipi kinachokushangaza kwangu nikikwambia mama namuunga mkono na akifanya vizuri nitampigia kura?

Vijana wa Chadema jitafakarini sana aina ya siasa zenu, muda si mrefu mtamuona hata Mbowe hafai wakati Mbowe anawazidi akili kwa mbali na hataki siasa za kiharakati, hii ni mara ya pili Freeman Mbowe anakutana na Rais, yule hana akili kama hizi zenu za kumpinga mtu kwa kila jambo halafu baadaye urudi tena kwa mtu yuleyule kumuomba jambo fulani.

Kama nyinyi ni wanaharakati kweli katiba inaruhusu mikutano na maandamano ni kwa nini mnataka ruhusa ya Rais ilihali ni haki yenu ya kikatiba? Ni lini haki ikawa inaombwa?
 
Lengo la kuanzishwa chadema ni kushika dola. Raisi kukutana na upinzani sio hisani.

Lakini pia unaweza kusupport CCM na raisi wake bila tatizo lolote, maana ndio Uhuru wengi wanaupigania. Ni hiari yako, Ila usilazimishe wengine Wala kuwasemea wengine acha kila mtu awe upande anaoutaka
Hata Hashimu Rungwe lengo lake ni kushika dola, hilo ndio lengo la vyama kuanzishwa kwake, ila siasa ina michakato yake huwezi kuikwepa kufikia malengo, hata kama hushiki dola lakini mnakuwa na taasisi imara ambayo inaheshimika na dola.
 
Back
Top Bottom