Rais Samia kateleza ulimi. Kazi ya Mbunge si kuleta maendeleo wala kutoa huduma

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Rais Samia kateleza ulimi alipokuwa anatoa ufafanuzi wa hoja za Luhaga Mpina. Kazi ya Mbunge si kuleta maendeleo wala kutoa huduma kama alivyodai. Bali mbunge ni mwananchi anayewawakilisha wenzake Bungeni.

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majukumu yake yanatokana na Katiba ya Tanzania, Sheria za nchi, na Kanuni za Bunge.

Yafuatayo ni mamlaka na majukumu ya Mbunge:

1. Kutunga Sheria: Mbunge hushiriki katika mchakato wa kutunga, kurekebisha, au kufuta sheria zinazohusu masuala ya kitaifa.

2. Kusimamia Serikali: Kupitia Bunge, Mbunge ana mamlaka ya kuhoji na kusimamia utekelezaji wa bajeti na sera za serikali.

3. Uwajibikaji wa Serikali: Mbunge hushiriki katika kuisimamia serikali kuhakikisha inawajibika kwa wananchi.

4. Kuwasilisha Changamoto za Wananchi: Mbunge hupeleka hoja, matatizo, na maoni ya wananchi wa jimbo lake bungeni kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.

5. Kuhamasisha Maendeleo: Mbunge ana jukumu la kushirikiana na wadau mbalimbali kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jimbo lake.
 
View attachment 3373441

Hajateleza sema ana uelewa mdogo sana, inept
 
Back
Top Bottom