Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Muda wote walikiwa wapi? Yani kusikia CHADEMA wanataka mchakato wa katiba mpya uanze wamekimbilia single ya kutoa elimu miaka mitatu.
 
Wakina nani watakuwa na wajibu wa kuitoa hiyo elimu ya Katiba?
 
Wewe kwanini unataka katiba mpya?
Nina sababu hamsini. Sababu ya kwanza nimejifunza Madagascar, uchaguzi ukikaribia Rais aliyepo madarakani anajiuzulu kabla ya kampeni kuanza ili asiweze kutumia madaraka yake vibaya kuiba uchaguzi.
 
Inabidi tutambue jambo moja hata nusu ya watz hawatokuja kuelewa Juu ya vipengele vyote ktk katiba hata baada ya kupata elimu mchakato wa maoni ulishafanyika majority wakatoa maoni yao na pesa nyingi ikatumika wananchi tunaitaji katiba mpya
 
Expecting results from what you know (kutetegemea matokeo kwa jambo unalijua) I like this proverb Ostracism
 
Subirini wananchi wapate elimu kwa miaka mitatu. Katiba sio ya vyama ni ya wananchi.
Kama anasema katiba yenye zaidi ya miaka 50 Watanzania hawailewi.
Hiyo mpya ndiyo itaeleweka katika kipindi cha miaka 3.
Kumbe tume ya Warioba ilikuwa inawahoji Watanzania au Warundi.
 
Kwani ilipoandikwa hii yasasa watanzania walikuwa wanawelewa kuihusu?
Viongozi wa Afrika ni aibu kwa wenye akili na welewa!!
Tume iloundwa na mamilioni waliyotumia kwenye mchakato wa katiba Tena akiwa mwenyekiti ilikiwa nimchezo wakutafuna Kodi zetu?
Ni lini alijua waTz hawaijui katiba naye kama rais Toka aingie ikulu alifanya nini ili waijue??
Kwa ajuavyo otachikuwa miaka mingapi iliwote tuijue alafu tuandike hiyo nyingine??
Tunaviongozi wa ajabu na wa aibu kwelikweli...
 
Tunasema wananchi ndio wanaodai katiba mpya. Rais anasema wananchi wengi hawaijui katiba iliyopo hivyo wanashindwa kuonyesha katiba hii ina kasoro zipi! Dawa ni kutoa elimu kwa wananchi wote kwanza! A major paradox.

Hii ni kuanzisha mchezo usio na mwisho (a vicious circle). Tatizo kubwa la katiba hii ni madaraka yaliyopitiliza ya Rais yanayomuweka juu ya katiba na sheria. Marekebisho ya vifungu muhimu kuhakikisha viongozi wote, serikali nzima na vyombo vya dola vinakuwa na kutenda kazi ndani ya mzingo wa katiba, sheria na kanuni kuu za nchi ndicho kinachotakiwa. Wananchi hawahitaji elimu katika hilo. Wanalijua sana na linaathiri maisha yao ya siku kwa siku. Ukusanyaji wa maoni wa kamati ya Jaji Warioba ulithibitisha hayo na mifano ipo tele.

Rais na makundi yake ndani na nje ya serikali ndio wanaoogopa marekebisho hayo ya katiba na kukimbilia kisingizio cha “ujinga wa wananchi” na “wanasiasa kutaka kujimilikisha katiba”! Vyote si sawa. Anyway, serikali ifanye kama ilivyozoea. Watanzania hawana ubavu wa kuipinga. Lakini ni wazi wengi tunajua hii ni janja janja ya wazi kabisa iliyozoeleka nchini.
 
Yaani una maana wameapa pia na hao wa vyeo vya miaka mitano watakuwa wanatokea upande wa wananzengo wenzetu tu ??!! 😅😅🙏🙏
 
Kwakweli !! Lakini mbona TEC hawalizungumzii suala hili kama walivyofanya kwa suala la Bandari ??!
 
Sipati picha.
Hiiyo elimu ya Katina itatolewa kwa utaratibu gani?
Muhtasari wake utakuwaje?
Walimu Gani?
Madarasa yepi?
Nanusa harufu ya upigaji wa Yale mabilioni bila matokeo chanya.
 
Abracadabra !! Ili tuendelee kweri kweri tunahitaji Dikiteta MUADILIFU !!
Hii kuachiana kwa miaka mitano mitano ni kazi bure tu !
 
Sipati picha.
Hiiyo elimu ya Katina itatolewa kwa utaratibu gani?
Muhtasari wake utakuwaje?
Walimu Gani?
Madarasa yepi?
Nanusa harufu ya upigaji wa Yale mabilioni bila matokeo chanya.
Ng’hana ong’wafaza 😍🙏🙏😅😅
 
Sijui priorities za TEC. Pengine hawana interest na masuala ya demokrasia 😳. I really don’t know.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…