Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Katiba ya warioba ilikuwa miaka kumi iliyopita,
Unadhani watu walioongezeka hawastahili kutoa maoni yao? Watoto wenye miaka 8 kipindi hicho now wana 18, huoni kama ni muda mrefu sana?

..katiba ya warioba iende kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni.

..kutakuwa na kampeni ambazo ni fursa kwa vyama vinavyounga mkono au kupinga kutoa elimu kwa wananchi.
 
Anayenufaika na KATIBA iliyopo ni ngumu kutaka kuibadilisha........na sidhani kama itapatikana siku za karibuni kwasababu hata bunge likija watawala wataweka vipengele vinavyowapendeza wao na itakuwa kama kilichofanyika kipindi kile, kusema ukweli katiba ni muhimu kulinda Rasilimali zetu,ila bado Wananchi wengi na wanaojiita wasomi wengi ni wachumia tumbo na wananufaika na mifumo iliyopo ndiyo maana tunakwama....... kesho huwezi ona gazeti lolote linapinga kauli ya Rais,zaidi ya kusifia tu......... sometimes nikiwaangalia kina Lissu,Slaa na Mwambukusi nawengine wanapambania katiba.....nawaonea huruma cos wanahubiri jambo la muhimu kwa watu wasio tayari.
 
Kumbe Samia ndie alikuwa mwenyekiti wakati ule?

Hapa ndipo utakapoiona nia yake ovu dhidi ya watanganyika na pesa zetu walipakodi, anazichezea tu.

Huyu mtu tangu alivyoanza kuwafukuza uwaziri wakina Lukuvi na Kabudi, tayari alikuwa anajitengenezea mazingira ya 2025, akawasogeza awapendao karibu yake zaidi kina Nape, yale yalikuwa maandalizi...

Hata hili la kutufundisha Katiba iliyopo ni mbinu yake ya kutuchelewesha ili ahakikishe tunaenda uchaguzi mkuu wa 2025 tukiwa na hii Katiba mbovu itakayombeba, hasa baada ya kujua hapendwi wala kuaminiwa na watanganyika kwa asilimia kubwa.
Hamieni Burundi[emoji1787]
 
Aliyemwambia hatuja soma katiba mpya na kuielewa ni nani, hivi huyu bado anatuona sisi wajinga. Kwani zoezi la katiba mpya limeanza jana ?? Mwambieni huyo bi ushingi,,, katiba mpya haijaanza leo wala jana toka enzi za Jk watu tunadai katiba mpya,,, hivi huyu anadhani kipindi chote hicho watu hawajasoma hio katiba. Tafadhali asitupande kichwani, tushamstukia anataka kutuletea janjajanja
 
Mkinipapasa nami ntawapapasa na mkiniparura nami ntawaparura

Katiba mpya ndio hiyooooo …boko la 2014 limetokea tena 2023
Ujumbe wangu kwa Raisi ni Samia chonde chonde usiupore uchaguzi muogope Mungu je Raisi wangu mpendwa unajua kama Maulana hapendi wanaozulumu HAKI za wenzao?
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Nonsense
 
Hamna mabadliko ya sheria hadi zilizopo wananchi waache kuzivunja, mitaala ibaki ilivyo hadi pasiwepo na watoto wanaofeli, tusipitishe mabadiliko ya kodi mpaka wananchi waelewe zilizopo, na DP world wangoje wale wa Mpitimbi wasowahi kuagiza hata t-shirt wajue kuendesha bandari.
Asante philosopher. Umeongea deep Sana.
 
Ushauri wangu kwa wataalam wote tz, achaneni na habari za katoboa mpya wala uchaguzi, tuishi Tu maisha yaendelee. Kwa sababu hofu yenu ni kubwa ya kuondokewa madarakani. Mnooo. Tuokos hizi fedha B.13 za elimu ya katiba tukajenge MADARASA ya SM huko vijijini. Na mapesa ya uchaguzi yoooote jengeni lami
 
Kipindi cha JK na Rasimu ya Warioba ilikuwa ni ufujaji tu wa pesa za Umma ! Au ??!!
Jk.alikua na lengo zuri tu mkuu...

Hao wanaomdhibiti samia leo ndio waliomdhibiti jk.

Kuna watu wamekula viapo vya kazi ya kuilinda hii nchi maisha yao yote..

Wakati wewe na Cheo chako cha urais wa miaka mitano unataka kuwaletea msumbuvu katika kazi yao?
 
Rais yuko sahihi. Kuna watu hawajui hata kitabu cha katiba kinafananaje. Hao wanaodai katiba mpya (CHADEMA) wanachofanya ni kuwaburuza nyumbu kwa kuwaambia katiba imeruhusu maandamano na uhuru wa kutoa maoni hata kama ni matusi. Wanachopigania ni kushika tu dola ili kujineemesha na sio kubadili katiba kwa manufaa ya kila mwananchi. CHADEMA hawana nia yoyote zaidi ya kwamba wanawaonea wivu CCM kuongoza nchi. Watu ambao ukiwauliza michango ya join the chain wanaishia kutukana hatuwezi kuwachagua kutuongoza. Chama kilichotumia bilioni 1 na nusu kununua pagale huko Mikocheni hakiwezi kushika dola kamwe. Zitto Kabwe alishauri wapinzani wenzake wapiganie tume huru kwanza ila nyumbu kwa ujuaji wao wakataka katiba. CCM nayo pia inataka katiba mpya ila hadi wananchi wapate elimu kwanza.
Hiyo katiba ya mwaka 1977, mwananchi gani alioewa elimu?. Yani katiba Ina miaka 46 ndio Leo tuanze kupewa elimu yake ili iweje?. Tupunguze utapeli.
 
Na ndio maana wanawaona watu ni wajinga sio! Hayo ni mawazo yake! Katiba tunaifahamu vizuri sana na haitufai kwa wkt wa Sasa. Kama tusingekuwa tunaielewa tusingetoa maoni ya katiba mpya kwenye time ya Jaji Warioba. Period!
Naona Jaji Warioba na Tume Zote zilizopita hawa kuwa waelewa kama Dr WA Sasa , ambaye ameona ili tupate katiba Bora Kwanza wananchi wapate digirii ya "katiba"
 
Hiyo katiba ya mwaka 1977, mwananchi gani alioewa elimu?. Yani katiba Ina miaka 46 ndio Leo tuanze kupewa elimu yake ili iweje?. Tupunguze utapeli.
Wewe unajua au unaielewa kwahiyo hawa wengine wasio ijua unawaweka wapi?

Au nikipi kinakufanya uwe na haraka ya katiba mpya?
 
Elimu gani?. Huyo Rais alikuwa makamu mwenyekiti kwenye bunge la katiba, Leo ndio anadai watu wapewe elimu. Acheni utapeli.
Unajuaje kama hakutoa ilo wazo wengi mnataka katiba mpya kwa masilahi yenu peke yenu na sio nchi kama taifa
 
Back
Top Bottom