Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Elimu ya katiba bado sana nchi hii wanasiasa uchwara na wanaharakati wanadai katiba ili iwawezeshe kuingia ikulu wakati mambo ya muhimu mengi hakuna mwenye habari nayo. Namuunga mkono rais bado elimu inahitajika sana.
Hakuna ulazima vyama vya upinzani kuingia ikulu kama katiba mpya itapatikana jambo la msingi kila muhimili ujitegemee kama itatokea mbunge kazulumiwa ushindi wake basi atapata haki yake
 
Umejitahidi kupotosha mkuu,

Alichosema ni kuwa, watu wapewe shule vizuri ya katiba hii tulionayo, na pia kasema vizuri kabisa, katiba ni ya watanzania, hatuwez sema tuchukue maoni ya wanasiasa tu ndio tuunde katiba, lazima kila mtu atoe maoni, na ili kila mtu atoe maoni ni lazima watu waijue hii katiba iliyopo, na yupo sahihi.

Yote aya yalifanyika kwenye mchakato wa warioba , kwa nini tusiboreshe huo kwa muda mfupi tukaja na katiba mpya
 
Mama si aliwahi kuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba? Wakati ule hakujua kwamba watanzania hawaijui katiba hata hii iliyopo? Kingine Rasimu ya katiba ya warioba ndio maoni halisi ga watanzania...

Tuijue au tusiijue atupatie katiba mpya. Aache uoga.
 
Tunakwenda kusomea chuo gani. Hii iliyopo waliekimishwa?
Swali la uzushi ni elimu ipi itafaa kwa hii katiba ya 1977 au ile mpya itakayoundwa. mimi nadhani katiba mpya yes itakapo pitishwa wananchi waelemishwe kwa vile hiyo ndiyo itakuwa hai na kitendea kazi kuendesha maisha yao. Busara, Tutunge katiba mpya elimu baadaye,Kamati ya Prof Mkandala nayo imebaini na kupendekeza hivyo kuhusu kipindi cha utoaji elimu
 
Mimi mama Abdul sijaielewa vizuri iliyopo! Nipeni muda angalau kila mwaka niwe nasoma ukurasa mmoja nikimaliza twende kwa wananchi. Hiyo itakuwa 2098, wote tuseme CCM HOYEE
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Huyu mama ana ubongo wa Ki-Zanzibar;
 
Hakuna ulazima vyama vya upinzani kuingia ikulu kama katiba mpya itapatikana jambo la msingi kila muhimili ujitegemee kama itatokea mbunge kazulumiwa ushindi wake basi atapata haki yake
Sasa wenzako wa vyama wanataka katiba ibadilishwe ili waingie ikulu which ofcorse siyo mbaya lakini hawana nia njema na wananchi.
 
Ni bora CDM hawajashiriki huo mkutano wa kupotezeana muda. Acha washiriki hao wenye muda wa kupoteza.
 
..Ccm waachwe wang'ang'anie madarakani lakini wasiwanyime Watz mambo mengi mazuri yatakayopatikana kutokana na Katiba Mpya na Bora. Masuala ya chama kipi kitatawala ni component ndogo sana ktk Katiba nzima.
Tatizo wananchi hawapewi nafasi ya kujua mambo ya msingi wanayohitaji serikali iwafanyie. Walioshika kidedea mabadiliko wao wanaangalia ni namna gani wataingia ikulu. Rais yupo sahihi elimu kwanza itolewe.
 
Acha watu wakapige hela watakaopata nafasi ya kuzunguka kutoa elimu kwa wananchi
 
Umejitahidi kupotosha mkuu,

Alichosema ni kuwa, watu wapewe shule vizuri ya katiba hii tulionayo, na pia kasema vizuri kabisa, katiba ni ya watanzania, hatuwez sema tuchukue maoni ya wanasiasa tu ndio tuunde katiba, lazima kila mtu atoe maoni, na ili kila mtu atoe maoni ni lazima watu waijue hii katiba iliyopo, na yupo sahihi.
We form two hukusoma mada ya constitution kwenye somo la civics??
 
Back
Top Bottom