Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Apumzishwe na nani ??!!😅😅🙏
Nina matumaini madogo sana na chama chetu CCM. Hakika haya ni matumaini yangu ya muda mfupi na yanaweza badilika palipo na pale patakapo tokea Viongozi mahiri miongoni mwetu.

Kwa kifupi, nimekosa imani na Viongozi wakuu wa Chama chetu, na kwa msingi huo, nadhani ni wakati mwingine, muafaka wa Kutanguliza nchi kwanza badala ya matumbo yetu(bila dira) kwanza, na katika mlolongo huo huo, naamini tupo Wana CCM wengi sana ambao tunaamini, SSH hana Uwezo wala dhamira ya kutanguliza Nchi yake kwanza, kwamba amekosa Uzalendo unaohitajika karne hii, kupambana na Ukoloni Mamboleo unaoathiri Nchi nyingi za Kiafrika.

Kukujibu swali lako,Chama chetu cha Mapinduzi na Wananchi wazalendo wa Nchi hii, tunao uwezo huo ifikapo 2025 Atapumzishwa na kura, ndani ya CCM na nje ya CCM.

Aluta Continua.
 
Kigenge ndani ya CCM kilichojipachika jina system ndio huamua nani awe kiongozi. Wananchi huishia kupoteza muda kwenda kusimama kwenye mstari wa kura.
Jitahidini wananchi wawaelewe laa sivyo mtaendelea kumtafuta mchawi kumbe wachawi ni nyie wenyewe.
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Hii ni namna fulani ya 'escapism' na inaonyesha wazi kuwa hakuna nia ya kupata katiba mpya. Waliomadarakani wananufaika na katiba ya sasa hivi. Mbona kutunga sheria hakusubiri watu waelewe kwanza maana ya sheria inayotungwa au marekebisho yanayofanywa kwenye sheria? Ni kipimo gani kitatumika kuonyesha sasa watu wameelewa maana ya katiba na ni nani atakayepima huo uelewa? Je, ikitokea baadhi ya wananchi hawajaelewa maana ya katiba ina maana katiba mpya haitakuwepo?
 
Jitahidini wananchi wawaelewe laa sivyo mtaendelea kumtafuta mchawi kumbe wachawi ni nyie wenyewe.
Wananchi gani labda, wangekuwa hawatuelewi mngekuwa mnaiba kura? Ukitaka kujua wananchi wanatuelewa, nenda kwenye uchaguzi mdogo wa Mbarali ambao CDM wamesema hawashiriki kisha uone mwamko uliopo. Hapo ndio utajua kiwango cha uelewa wa hao wananchi.
 
Unawaambia watu na akili zao jambo la kijinga namna hii, halafu bado wewe unajiona kuwa ni kiongozi kweli wa watu hao?

Hawa viongozi wamekosa hata njia ya kudangania watu waonekane kuwa na akili kidogo vichwani mwao?
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Siku zote mtu mbumbumbu hudhani kila mtu ni mbumbumbu kama yeye alivyo mbumbumbu.Ndio maana tunaendelea kusema na kupaza sauti kwamba hii nchi kabla haijaharibika TUACHE SAUTI YA WANANCHI IONGEE. WAO WENYEWE WALICHAGILIE TAIFA UONGOZI NDIO TUTAFIKA SALAMA TUENDAKO NJE YA HAPO TUJUE TUNAJITEKENYA WENYEWE NA KUCHEKA.RAIS KWA KAULI ZAKE HIZI INAONYESHA HAIJUI NCHI VZR.Na wanao mzunguka hawamwambii ukweli ila wanasubiri atoke kwenye uongozi ili wafungue turbo zao.
 
Yote aya yalifanyika kwenye mchakato wa warioba , kwa nini tusiboreshe huo kwa muda mfupi tukaja na katiba mpya
Katiba ya warioba ilikuwa miaka kumi iliyopita,
Unadhani watu walioongezeka hawastahili kutoa maoni yao? Watoto wenye miaka 8 kipindi hicho now wana 18, huoni kama ni muda mrefu sana?
 
Hiyo ikulu iliyojazwa matambiko nayo ni takatifu?
Duh, hiyo ligi na huyo mtu kweli utaiweza?

hawa ni watu walioko ligi yao wenyewe, hata ufanye nini hakuna utakachobadilisha kwao.

Anakwambia "Ikulu ni mahala patakatifu..." akijua shetani kapateka mahala patakatifu!
 
Katiba ya warioba ilikuwa miaka kumi iliyopita,
Unadhani watu walioongezeka hawastahili kutoa maoni yao? Watoto wenye miaka 8 kipindi hicho now wana 18, huoni kama ni muda mrefu sana?

Je umesoma nilipoandika tusiboreshe, hao ambao hawakupewa nafasi watoe maoni Maana population ya si kubwa
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
CCM muache mara moja kutuona wananchi ni wajinga! Hii ni dharau kubwa sana na mtaigharamia.
 
Mie japo huwa siuelewi uongozi wake ila kwa namna fulani yupo sawa maana kati ya hawa watz milioni 62 sidhani kama wenye uelewa wa katiba wanafika hata milioni 1...watu wajue hii iliopo inaupungufu gani sio kelele za katiba na wakati hawafahamu hata unahusu nini.
 
Nina matumaini madogo sana na chama chetu CCM. Hakika haya ni matumaini yangu ya muda mfupi na yanaweza badilika palipo na pale patakapo tokea Viongozi mahiri miongoni mwetu.

Kwa kifupi, nimekosa imani na Viongozi wakuu wa Chama chetu, na kwa msingi huo, nadhani ni wakati mwingine, muafaka wa Kutanguliza nchi kwanza badala ya matumbo yetu(bila dira) kwanza, na katika mlolongo huo huo, naamini tupo Wana CCM wengi sana ambao tunaamini, SSH hana Uwezo wala dhamira ya kutanguliza Nchi yake kwanza, kwamba amekosa Uzalendo unaohitajika karne hii, kupambana na Ukoloni Mamboleo unaoathiri Nchi nyingi za Kiafrika.

Kukujibu swali lako,Chama chetu cha Mapinduzi na Wananchi wazalendo wa Nchi hii, tunao uwezo huo ifikapo 2025 Atapumzishwa na kura, ndani ya CCM na nje ya CCM.

Aluta Continua.
Utamaduni kama huo haujawahi kushuhudiwa katika Chama chetu !
Itakuwa ni maajabu makubwa sana mtu ajitokeze kumpinga Mwenyekiti wa Chama !!
 
Dude linaloitwa katiba Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Suluhu hassan amesema kwamba watu wa nchi hii hakuna anaejuwa maana ya katiba kwa hiyo ni vizuri watu kwanza wafundishwe waelewe maana ya katiba kwani hata tuliyonayo hakuna anayeifahamu.

kuhusu katiba mpya jambo hilo litafanyika hadi pale watu watakapo kuwa wanaelewa hata hii tuliyonayo hii maana yake ni kwamba vyama vya upinzani ingawa vimeendelea kusisitiza kuwepo umhimu wa katiba mpya wajue kuwa kwa sasa hilo suala halipo.

Jambo pekee ambalo serikali inaenda kulifanya ni kuwepo kwa somo la katiba mashuleni na vyuoni pamoja na taasisi zote za dini na serikali kuelemishwa maana ya katiba kwani watanzania hawana uelewa na katiba hiyo.

Ndugu zangu vyama vya upinzani mjue kuwa tunaenda kufanya uchaguzi mkuu bila kuwepo kwa tume huru wala katiba mpya! je mko tayari kwenye mashindano? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Hii katiba ni ya hovyo! Hatuhitaji kujifunza chochote, Ndani yake kuna madudu mengi!Rais anakuwa,kama mungu MTU!
 
Maza, huo "ujununu fununu" wetu sisi CHADEMA uko wapi?
 
Tatizo wananchi hawapewi nafasi ya kujua mambo ya msingi wanayohitaji serikali iwafanyie. Walioshika kidedea mabadiliko wao wanaangalia ni namna gani wataingia ikulu. Rais yupo sahihi elimu kwanza itolewe.

..unaweza kuwa sahihi.

..Je, kama Taifa tunakubaliana kuhusu " mtaala " wa elimu inayopaswa kutolewa?

..Je, tunakubaliana ni kina nani wawe " wakufunzi " watakaokwenda kuelimisha wananchi?

..Je, tutatumia kigezo gani kupima uelewa wa wananchi kuhusu somo la Katiba mpya?

..Kuna ulazima gani wa wananchi kufundishwa kuhusu Katiba iliyopo wakati tunakubaliana kwamba tunahitaji Katiba Mpya?

..Utaelimisha vipi wananchi kuhusu Katiba mpya wakati bado hatunayo hiyo Katiba.

..Je, kuna mfano wa nchi yoyote iliyotoa elimu ya Katiba kabla ya kuandika Katiba mpya? Je, Afrika Kusini, South Sudan, nchi zilizoandika Katiba hivi karibuni zilitumia utaratibu gani kutoa elimu?
 
Back
Top Bottom