Raisi yupo sahihi kabisa kuhusu uelewa wa Watanzania bila ya Kusahau kwamba naye ni Mtanzania. Itoshe, imepita miaka miwili na ushee toka ashike dola na Bado haijaielewa.
Ikumbukwe au izangatiwe pia, kuwa, mwaka wake watatu wa kuisoma na kuilelewa Katiba utakuwa ndio mwaka wake wa kuingia kinyang'anyiro cha Uraisi- Je atafaa kuwa Rais wa JMT kama haonyeshi nia ya kulinda Katiba hiyo ya Jamhuri, asiyoielewa? Haijalishi....wabobezi wa sheria wanadai "ignorantia legis neminem excusat"
Kwamba," kwamba mtu asiyejua sheria hawezi kukwepa dhima kwa kukiuka sheria hiyo kwa kutojua maudhui yake"
SSH hawezi kujifunika katika wingu la kutokuwa na Uelewa wa Maudhui ya Katiba yetu, kwani yeye amekuwa ni miongoni mwa viongozi walioapa Kutii na Kuilinda katiba hiyo, unaapa kufanya hivyo bila ya Uelewa wa unachokiapia? Je, anataka kusema kuwa Watanzania wengine hawana akili ya kung'amua yaliyomo kwenye Katiba yao? Kwamba hawana uelewa wa Katiba yao?
Tunapozingatia SSH ni miongoni mwa Watanzania na tunapozingatia hayo aliyoyasema ni kweli, basi Yeye binafsi hana pakutokea, narudia, haya kwamba mtu asiyejua sheria hawezi kukwepa dhima kwa kukiuka sheria hiyo kwa kutojua maudhui yake
Akemewe kwa Vijembe vyake, akemewe kwa kuwatukana Watanzania
2025 apumzishwe.