Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Kipindi cha JK na Rasimu ya Warioba ilikuwa ni ufujaji tu wa pesa za Umma ! Au ??!!
 
Katiba mpya hadi watu wasome na mimi Mama Abdul pia niielewe
 
Tena watu kama Chadema hakuna wanachoelewa,kwao Katiba Mpya ni kuingia madarakani.

Lowasa: Elimu,Elimu,Elimu 🤣🤣
 
Nani ambae haijui hii katiba ya sasa.
 
OK, KWENYE KATIBA LAZIMA KILA MTU ASOME AELEWE, KWENYE MKATABA WA DP WORLD Watu 78 TU WALITOA MAONI YAO KATI YA milioni 60, Kwanini isiwe hivyo na kwenye katiba sasa.
 
Hata siku moja hautowahi kupata maoni ya watanzania wote, kila siku watu wanazaliwa na kufa. Hivo kwa lugha rahisi sana ni kwamba katiba mpya kwa CCM hilo haliwezekani. Lazima kuwe na kundi la watu watakaowakilisha wengine, mbona leo hajakutana na watanzania wote bali kakutana na kikundi cha watu anachokiita wadau. Alafu kwa nini nchi za kiafrika viongozi wanajiona wao ndo wenye akili kuliko wale wanaowaongoza? Leo anasema huko vijijini watu hawaijui katiba ya JMTZ wataijua vipi ikiwa miaka michache kukutwa na katiba ilikuwa ni kosa la jinai? KATIBA iliochwa kuzunguka kwa kila mtu ni katiba ya CCM?
Rais yeye mwenyewe binafsi anapaswa kuwa wa kwanza kuijua katiba aliyoapa kuisimamia na badala yake anaikanyaga.
 
Haiwezekani kila mtu akatoa maoni yake kuhusu katiba, labda ipigwe kura ya maoni.
 
Hebu tuambie, ukiwa kama advocate wa Samia; ni kitu gani tunachotakiwa kukijua kuhusu hii Katiba iliyopo ya 1977?
 
Hivi rasimu ya warioba na katiba pendekezwa ilipatikanaje?

Hayakuhusishwa makundi mbalimbali nchini kote?

We chawa hebu kuwa serious kidogo
 
Elimu ya katiba bado sana nchi hii wanasiasa uchwara na wanaharakati wanadai katiba ili iwawezeshe kuingia ikulu wakati mambo ya muhimu mengi hakuna mwenye habari nayo. Namuunga mkono rais bado elimu inahitajika sana.
Kumbe na Samia anaiogopa Katiba Mpya akidhani ndio itamuondoa ikulu?!

Sasa hivi visingizio vyenu vya mpaka tufundishwe Katiba ya 1977 leo 2023, vina maana gani?
 
Huyo inajichimbia kabuli lake mwenyewe. Kipindi akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba ya jaji Warioba, alikuwa anafanya nini pale mpaka tukapata rasimu ya katiba. Ameamua kuvujisha pesa za watanganyika kwa wizi unaoitwa elimu ya katiba kwa miaka 3
Kumbe Samia ndie alikuwa mwenyekiti wakati ule?

Hapa ndipo utakapoiona nia yake ovu dhidi ya watanganyika na pesa zetu walipakodi, anazichezea tu.

Huyu mtu tangu alivyoanza kuwafukuza uwaziri wakina Lukuvi na Kabudi, tayari alikuwa anajitengenezea mazingira ya 2025, akawasogeza awapendao karibu yake zaidi kina Nape, yale yalikuwa maandalizi...

Hata hili la kutufundisha Katiba iliyopo ni mbinu yake ya kutuchelewesha ili ahakikishe tunaenda uchaguzi mkuu wa 2025 tukiwa na hii Katiba mbovu itakayombeba, hasa baada ya kujua hapendwi wala kuaminiwa na watanganyika kwa asilimia kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…