Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia Suluhu Hassan akishiriki Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation - Zanzibar
Rais ahuzunika kwa kufeli sana kwa mkoa anaotokea, Kusini Unguja.
Rais Samia azungumzia ubovu wa matokeo Zanzibar ambapo alitoa maelekezo na sasa ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka. Amezungumzia kufeli kwa wanafunzi Zanzibar na amepongeza juhudi za asasi za kiraia na serikali katika kuongeza ufaulu akitolea mfano wa matokeo ya 2020.
Rais amesema ni aibu kwa mkoa ambao anatoka Rais wa JMT(Kusini Unguja) kuwa na ufaulu duni ukilinganisha na mikoa mingine.
Rais ametoa wito wa kuwa na performance appraisal na vipimo tofauti na sasa ambapo walimu wamepewa ajira za maisha hivyo hubweteka na kusababisha elimu kuwa duni kwa kuwa hawajitumi kazini.
Rais amekosoa suala la kuchukua wanafunzi waliofanya vibaya darasani, badala yake walimu wazuri wawe ni wale ambao wamefaulu vizuri ili kuboresha elimu nchini.
Bila kulea watoto vizuri tutazalisha Panya Road
Rais atoa wito kwa wazazi kuhusu mkakati wa kutokomeza zero Zanzibar kwa kuwataka wazazi washiriki kutambua maendeleo ya elimu ya watoto wao, badala ya kuwaachia walimu peke yao.
Ili mwanafunzi aweze kufaulu inategemea pande tatu, wazazi, walimu na serikali. Rais amesema. Amesisitiza watu wote tushiriki kulea ili tung'ae bila kulea vizuri tutazalisha panya road wa kike na wa kiume.