Rais Samia katika Uzinduzi Zanzibar akosoa kuchukua waliofeli kuwa walimu asema ndio wanadumisha elimu nchini

Mnawalipa mshahara wa Mama Ntilie halafu mnataka waliofaulu?
 

Rais Samia anafanana na Vasco dagama.​


Vasco Dagama unamfahua au unasoma tu kwenye historia. Kwa kuingia kwa rais Samia mm mwenyewe nimepiga hatua 20 mail. Ukilinganisha na Magufuli. Kwanza mkopo wangu wa Chuo Kikuu umeisha mapema. Namshukuru Mungu sana kwa Rais Samia kuwa Rais.
 
Nipo kusini mwa Tanzania huku kwakweli wananchi hawaridhishwi na awamu hii ya sita.
 
Walimu wa St Francis, Feza, Canossa, Marian wote wana division I point 3 ?
 
Kada ipi ichukue waliofeli?
 
Yaani nipate div one pcm au cbg then nikawe mwalimu serious kwa mshahara upi wkt engineer wa tanrod anakula milioon 6 kwa mwezi hapa

Itabakia hvyo hvyo kuwa waliofelinndio wawe waaLimu wetu na pia waanzishe performance appraisal kwa walimu wasiopaerfomu vzr
 
Nipo kusini mwa Tanzania huku kwakweli wananchi hawaridhishwi na awamu hii ya sita.
Hawana elimu huko ata huku kanda ya ziwa raia wanasema amesanabisha vitu kupanda bei yaan nawaangalia nabaki kuwaacha na ujinga wao
 
[emoji625]GOLDEN TULIP, Zanzibar. Juni 19, 2022.

RAIS SAMIA AZINDUA TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo yenye saini 50 za Wanafunzi Wanawake waliofaidika na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

#KaziIendelee
#AlipoMamaVijanaTupo
#JiandaeKuhesabiwa2022
 
Kwa hiyo Rais, ameona sababu ni kuajiriwa tu kwa walimu waliofeli! Na anaposema walimu waliofeli, anafahamu anacho kizungumza? Maana NECTA inamtambua mtahiniwa aliyepata daraja 0 pekee au yule aliyepata F kwenye somo; ndiye aliyefeli!
Kuanzia daraja la 1-IV, hawa wote ni watahiniwa walio faulu! Sasa atuambie kama kina mwalimu aliye ajiriwa huku akiwa amepata division 0!!

Siku nyingine aseme labda 'walimu wenye ufaulu hafifu'!!! Na siyo walimu waliofeli.

By the way, anatambua pia changamoto nyingine zinazo wakabili walimu wake wa huko Zanzibar? Au ameamua tu na yeye kuongea ili aonekane? Mfano mazingira duni ya kufanyia kazi, mishahara midogo na isiyokidhi mahitaji, kutokupandishwa madaraja kwa wakati, jamii kutokuwa na muamko wa kusoma; na hasa elimu dunia! nk!
 
Walimu wenye three na four wameghushi utumishi, wafukuzwe tuajiri degree za first class kuanzia msingi
Mna hela za kuwalipa hao walimu mishahara inayo endana na elimu yao? Au na wewe una akili kama za Rais wako? Unataka ng'ombe atoe maziwa, huku ukiwa humpi chakula kinacho stahili?
 
mshahara wa wapi huo.kwani tannroad wana special scheme au.ninachojua ni kwamba tanroad wanapokea sana rushwa kutoka kwa wakandarasi lkn si kuwa na mishahara minono.
 
Eng tanroad anakula mil 6?? [emoji23][emoji23]
Story za vijiweni hizo
 
Engineer wa halmshauri anapokea TGS E, 940000 kabla ya makato. Huko TANROAD unakosema sio rahisi kupata nafasi kizembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…