DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza hayo katika kilele cha matembezi maalum ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi.
Amesema Mapinduzi ya Kisiasa tumeshajikomboa, kuanzia 64 mpaka leo siasa imetufikisha mbali sana, lakini Mapinduzi ya Kiuchumi na Ustawi wa Jamii bado ndio mapambano tunakwenda nayo.
“Na katika hili kuna ubunifu na weledi kwa vijana. Uchumi wa Buluu baada ya kutambua dhana na rasilimali tulizonazo, naomba vijana mkajiweke makundi ili muufanyie kazi uchumi wa buluu.
“Lakini la kwanza kubwa ni fikra za mageuzi ya kiuchumi, tumezoea katika taifa letu, suala la ukusanyaji mapato na kutafuta fedha ni suala la Serikali, kwa maana hiyo chochote kinachokwenda upande ni Serikali.
“Nilikuwa naangalia kwenye TV, Watanzania wanahojiwa kuhusu ajira, kila anayehojiwa anasema Serikali itengeneze ajira, nataka kuwaambia kazi ya Serikali si kutengeneza ajira, ni kuweka mazingira mazuri ili vijana myatumie kutengeneza ajira.
“Hiyo kazi tunaifanya vya kutosha, naomba muende mkatengeneza ajira kwa mazingira yaliyopo."
Mikutano ya hadhara
Tumetoa ruhusa ya mikutano ya hadhara, wapo watakaokuja na kasi, niwaombe vijana wa Chama Cha Mapinduzi, msiende kulumbana, jibuni hoja kwa ushahidi na takwimu.
“Ukisema kwa ustaarabu na uchagua maneno ya kusema, wewe unajiamini na huna haja ya kupayuka, lakini unapopayuka na kubwabwaja ni ishara ya uwoga, nendeni kajibuni hoja.
“Mkaitumie fursa mikutano ya hadhara kwa kueleza yale Serikali yenu iliyofanya.”
Ameongeza kuwa: “Sisi CCM tumejipanga hivyo, kuna vyama ambavyo haijajipanga, wapo watakaokuja kutukosoa, yale ya kweli tuyafanyie kazi, ambayo si ya kweli tuyajibu kwa hoja.
“Kubwa ni ustahamilivu, kama huna ustahimilivu utapandishwa jukwaani kujibu hoja, utapayuka kama yule aliyekupandisha jukwaani.
“Pia mfanye mabadiliko ndani ya chama, mrudi kuwa wamoja, tuwe chama kiongozi, wengine tumewazaa sisi, tuoneshe kuwa sisi ni viongozi, uongozi ni kuonesha njia."