Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Samia amesema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi. Ameeleza, "Kazi zipo nyingi Tanzania, ni Vijana kuchakarika, kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia"

Ametoa rai hiyo leo Januari 07, 2022 wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesisitiza, "Naombeni kaangalieni fursa za kazi. Fursa zipo nyingi na ni aibu kijana kukaa bila kazi"

Ameongeza, "Na hapa nitazungumzia changamoto inayofuata ambayo ni nyie Vijana kutokujua au kutotumia fursa zilizopo. Hamzitumii kabisa! Niwaombe sana Vijana, kuna fursa nyingi. Piteni Vyuoni mtaelekezwa jinsi ya kuziona fursa hizo"

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana

Sikiliza sehemu ya hotuba yake kuhusu Vijana na Kazi:

Rais Samia amesema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi. Ameeleza, "Kazi zipo nyingi Tanzania, ni Vijana kuchakarika, kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia"

Ametoa rai hiyo leo Januari 07, 2022 wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana
Mbona watoto wao wanawapatia ajira za serikalini?
 
Kuna watu wengi sana hawana ajira mtaani, kuanzia vijana mpaka wazee.
Kuanzia wasomi mpaka wasiokuwa wasomi.

Hivi hakuna kampuni au namna yoyote ile inaweza kufanywa na watu au mtu mwenye uwezo akawatumia hawa watu wasio na ajira?
Watu wasio na ajira ni wengi sana, hakuna namna ya kuwatumia watu hawa kutengeneza pesa?
 
Back
Top Bottom