Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Hii nchi ngumu *****!!! Bongo ni ya kuikimbia, bora vijana wote tukiondoka tukaawaachia nchi yao maccm yajitawale enyewe
 
Ukweli ni kwamba amechoka wala hata haelewi analoongea ni vema angeomba msaada wa kuelimishwa afanye nini kuwapatia vijana fursa za kujiajiri na namna gani anaweza kuwapatia mitaji ya kujiajiri. Wale washauri wake muelimisheni jamani laa sivyo hii nafasi pia itangazwe ipo wazi
 
Tatizo mtaji. Hata kulima yenyewe lazima ununue mbegu. Mbolea bei juu.
Umwajiliaji ndio mtihani hata nyanya haiwezi kukua.
Mchina kalima kando ya ruvu anamwagilia tayari amekamatwa. Sasa hizo furusa mama zikoje??.
Mkopo benki hipati kama huna senti moja mle.

Viongozi mnapotamka mfikirie na nje ya kapu pia.
Asante
 
Aliposema kazi iendelee watu hawakujua ni kazi gani aliyotaka kuiendeleza,

Kifupi mama alitaka kuendeleza zile kazi za kifisadi zilizokwamishwa na awamu ya 5 chini ya JPM.
 
Sasa uko kwenye JF kutwa una post uta export vipi pamba na katani? Toka hapo sebuleni kwa shemeji yako nenda Kibaigwa, Sumbawanga, Mbozi, Tunduma, Longido, Rombo uone vijana wanavyochemka.

Serikali inatengeneza mazingira kupitia sera za viwanda, biashara na kilimo.

Acha kumtegemea shemeji akupe hela ya bundle na sabuni, toka kahangike, fursa zipo
 
Tatiz la nchi yetu halijaanzia kwa leo. Mama tutamshambulia saana lkn sion km yeye kama yeye ataeza aje na suluhu yene faida zaid ya kusikia maneno km hayo.

Tukubali km nchi,mfumo wa elimu yetu ufumuliwe ili uendane na mazingira ya dunia sasa.
Hivi kama mtoto kuanzia std I had F6 anakaririshwa jinsi ya kujib mtihan tu,na hata huko versity kwenyewe it's the same! Tumtarajie mhitimu aingie dunia ya ujasiriamali kwa urahisi upi tuliomjengea tokea utoto wake?

Binafs sichukulii km kuwapa mikopo kuna tija coz kusudio la mkopo ni baadye fedha zirejeshwe,zitarejeshwaje km mkopaji hana uelewa wa kutosha kwa project aliyoiombea huo mkopo???? It's obvious hizo fedha zitaangamia na mtaanza kufukuzana na maafisa mikopo mitaan tuu mithili ya paka na panya na lawama juu kuona wameshindwa kurejesha.
Na ukiwatangazia mikopo vijana watakujia na business plan zao za viwango kabisa coz nadharia ndiyo kitu mliwafundisha zaidi mashuleni. Kaa usubirie utekelezaji wa vitendo km kilichoandikwa kwenye andiko mradi wao😂😂😂😂😂😂

Tubadilishe mfumo wa elimu yetu iwe inayoegemea practical zaidi na tuwe na shule zenye michepuko inayogusa maisha halisia ya kitanzania.

Hapo mama mnatarajia kwa nafasi yake mama asemeje,zaidi ya kukuhamasisha even if huenda hata yy moyon anatambua ugumu wa jambo lenyewe!
 
Sikuelewai kabisa
 
Naona hapo Mwisho ukamalizia na maneno ya motivational speaker.

Kwani maza yeye akiona watu wanasogelea urais wake hapo 2025 anakua mkali Sana,si aachane na urais aje kitaa kazi ziko nyingi Sana.
Ajikute tu anakuja kitaa atapagawa hata ushungi anaweza akasahau kuvaa
 
Mazingira yapi yaliotengenezwa bwana korosho to ku export imekuwa historia anasafirisha waziri tu wenye mashamba ya mikorosho wako hoi😅 ndio sera nzuri hizo?

Inaonekana naongea na mtoto wa Bhakressa ambaye hajui tumbo likishinda siku 2 bila chochote linakuwa na hali gani!
 
Ndio sera nzuri za viwanda na biashara hizo za watu ambao wanakinga 10M kwa mwezi na marupu rupu kibwena😅

Kimsingi bila mtaji hata uwe na idea kama za Elon Musk hutoboi.
 
Na mtoto wake yule ambae mbunge na yule mkwe wake ambae Ni waziri nao watakuja kujiajiri lini?maana nafasi ziko mtaani nyingi tu Ni uvivu wao tu 😄😄😄
Hahahahahah huyu maza anatuchezea, waje mtaani wanae waone balaa kama ndoa itatoboa hata miezi 6
 
Hata zingekuwepo. Bongo kwa kazi hio hio mtu atataka ufanye siku nzima akulipe 5,000/=??? Ni unyama ulioje yani umfanyishe mtu kazi masaa 12 halafu umlipe 5,000. Kazi nyingi za bongo ni level ya vibarua kimaslahi.

Ndio maana wao wanakomaa wawapachike watoto wao huko NSSF, NHIF, TRA, GSPA,TASAC,TRA,BOT n.k ambako mishahara ni ya kuridhisha ukiwa na kisomo chako. Kwanini wasiwapeleke kuosha masufuria hotelini kama ni kazi nzuri hizo?

Hapo hujala, familia haijala na nauli ya kesho unatakiwa uwahi kibaruani. Hivyo vibarua vya aina hio wenzetu wanaolipana laki na nusu mpaka laki 3 kwa siku wao wanaziita ajira. Ooh wawekezaji wameongezeka mtapata ajira muwekezaji wa kuja kukulipa 5,000 kwa kukutumia siku nzima?

Ulaya walau mtu atakulipa 5000 kila lisaa limoja...Masaa 12 ni elfu 60. Hakuna mtu ambaye angebaki mtaani kama kuna kazi ya aina hio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…