Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Mashamba yapo huku vijijini...vijana mnawaachia wazee. Njooni mjiajiri. Mlime kisasa.
Mkuu ni kweli kwamba fursa nyingi za maendeleo zipo mashambani lakini kwa sasa hali ni mbaya sana: Mabadiliko ya hali ya hewa haitabiliki, kiangazi, masika na vuli haya tabiliki; Serikali nayo imeongeza bei za pembejeo za kilimo mara dufu zaidi ya hiyo mikopo ya Halmashauri. Kwa mantiki hiyo FURSA za maisha kwa mwanachi wa kawaida haipo.
 
Rais Samia amesema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi. Ameeleza, "Kazi zipo nyingi Tanzania, ni Vijana kuchakarika, kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia"

Ametoa rai hiyo leo Januari 07, 2022 wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana
Huyu mama ni mpuuzi sana,atuonyeshe mtoto wa waziri,Mbunge,nk anayechakalika na kazi za jua kali,
Watoto wa wakubwa hutafutiwa kazi,voda,total,TRA,mifuko ya jamii,
Atuambie mtoto wa mkubwa gani anasoma shule za kata,kutibiwa hizi hospitari zetu za hovyo.
 
Rais Samia amesema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi. Ameeleza, "Kazi zipo nyingi Tanzania, ni Vijana kuchakarika, kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia"

Ametoa rai hiyo leo Januari 07, 2022 wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana
Yeye kila akilala anaota watu wanaonyang'anya urais na kuweweseka
 
Halafu utekelezaji wa hii operesheni unafanyika kinyume cha haki za binadamu kabisa.

Mtu anavamiwa kama vile mhalifu kwa marungu na kubebwa juu juu mpaka kwenye gari kuelekea kituoni.

Sijui tunajenga jamii ya aina gani jamani.
Hili gonjwa alilipalilia jiwe kwa kuwapa jeuri machinga kuwa hakuna atakaye waondoa mijini.

Leo hii jiwe hayupo mrithi wake anataka kuwaondoa ndiyo inakuwa mshike mshike
 
Kuna watu wengi sana hawana ajira mtaani, kuanzia vijana mpaka wazee.
Kuanzia wasomi mpaka wasiokuwa wasomi.

Hivi hakuna kampuni au namna yoyote ile inaweza kufanywa na watu au mtu mwenye uwezo akawatumia hawa watu wasio na ajira?
Watu wasio na ajira ni wengi sana, hakuna namna ya kuwatumia watu hawa kutengeneza pesa?
Namna ya kuwatumia ipo...anza kwa kuwa 'motivational speaker'...wengi watakusikiliza ila watoze pesa kidogo maana hali ya uchumi si nzuri.
 
Hahaha!!! Nahisi hujawahi kulima
kwahiyo kila mwaka utakuwa unafyeka msitu?
Anyway unaitendea haki 7000 yako, Shaka amekuona unaweza kwenda kuchukua.
Sisi watanzania hapa ndipo tunapo potea!Yaani kwa akili yako unamaanisha shamba jipya uchoka kwa msimu mmoja tu?Pili unamaanisha baada ya kulima msimu wa kwanza bado hautoweka mtaji kutokana na mavuno?.
Kwa taarifa yako tu,mimi mwaka jana nilianza na hekari 1 ya mpunga na sasa nimelima tatu na tayari nimezipanda.
Wewe subiria ajira ya mshahara tu,huku ukizidi kuchelewa mwenyewe.
 
Onyesha umama wako kwa kufanya yafuatayo nchini Ili sisi vijana tukikaa bila Kazi ndo utusimange.
Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.
1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.
2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.
3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele
4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao.
Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.
5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue.
Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.
6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa
Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana ccm imeshindwa nini.
Kwanza wewe hapo unalima hekari ngapi kwa mwaka?Mama ameongea na vijana ambao hata robo hekari hawezi lima.Sasa kijana huyu hata ukimpatia trekta na pembejeo bure,bado kwake anaamini kilimo ni kwa masikini na wasiofika vyuo vikuu.
 
Back
Top Bottom