Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia amesema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi. Ameeleza, "Kazi zipo nyingi Tanzania, ni Vijana kuchakarika, kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia"

Ametoa rai hiyo leo Januari 07, 2022 wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesisitiza, "Naombeni kaangalieni fursa za kazi. Fursa zipo nyingi na ni aibu kijana kukaa bila kazi"

Ameongeza, "Na hapa nitazungumzia changamoto inayofuata ambayo ni nyie Vijana kutokujua au kutotumia fursa zilizopo. Hamzitumii kabisa! Niwaombe sana Vijana, kuna fursa nyingi. Piteni Vyuoni mtaelekezwa jinsi ya kuziona fursa hizo"

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana

Sikiliza sehemu ya hotuba yake kuhusu Vijana na Kazi:

View attachment 2072394
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa
 
Kabla hajatangaza kifo cha JPM alikuwa Tanga anafungua viwanda,
Plan yao wilikuwa kutengezeza miundombinu ili irahisishe uwekezaji hasa viwanda vidogovidogo,
Leo hii kapandisha umeme, mbolea bei juu, kilimo chenye kubeba watu wengi na vijana walisha anza kuchangamkia hizo fursa, alichokifanya ni kuongeza bei ya mbolea na pembejeo!, sasa sijui mawazo yake yalilenga wapi???!
 
Samia anasahau kuwa Serikali yake ilishatoa ajira milioni 24 ikiwa ni ajira kwa vijana wote wenye vigezo vya kuajiriwa kwenye nchi hii pamoja na wazee juu!🤣🤣🤣
cHi.jpg
 
Mbona watoto wao wanawapatia ajira za serikalini?
Tena wanapewa hizo nafasi bila kuwa na sifa.

Kuna jamaa yangu anasononeka hadi leo kwa kukosa kazi wizara ya viwanda mwaka 2012. Interview ya mwisho wamebaki watu wawili, jamaa Mechanical Engineer na dada mmoja amesoma Food and Biochemical, anayehitajika ni Mechanical Engineer, jamaa alikuwa na uhakika ile kazi ni yake, kilichotokea hadi leo jamaa huwa haamini, yule dada alipata kazi na sasa ni mtu mkubwa huko wizarani.
 
Hawa majamaa ni sawa na wale wanyama wasiyo na huruma.
 
Mama aneongea kama watu wengi ambao hawajui uhalisia wa tatizo la ajira.

Kauli za mtu aliye kwenye ajira asiyejua hali halisi huku mitaani.
 
Yuko “out of touch”
Tunavurugwa ma jobless, mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa anahisi anafanya kusudi kubaki na njaa, ila kiukweli hali ni tete hata mtu asemeje hali ni ngumu nyie hakuna mtu anataka kuwa jobless ni basi tu inatokea mtu unakua huna pa kuchomokea...
 
Soma nilichoandika uelewe kabla ya kukurupuka kujibu. Kazi za chini siyo lazima u housegirl na u houseboy au kusugua masufuria au kusafisha hotelini. Hata hizo kazi za kilimo na uvuvi zilizozungumzwa na Rais ni za chini. Sasa kama unalipwa laki 1 si ni bora kuliko kutokuwa na ajira? Ndiyo maisha hayo chochote ni bora kuliko kutokuwa na ajira. Vijana kutokuwa na ajira zozote hata zile ambazo unaona za chini ni hatari. Kumbuka "an idle mind is the devil's playground".
Naona hapo Mwisho ukamalizia na maneno ya motivational speaker.

Kwani maza yeye akiona watu wanasogelea urais wake hapo 2025 anakua mkali Sana,si aachane na urais aje kitaa kazi ziko nyingi Sana.
 
Naona hapo Mwisho ukamalizia na maneno ya motivational speaker.

Kwani maza yeye akiona watu wanasogelea urais wake hapo 2025 anakua mkali Sana,si aachane na urais aje kitaa kazi ziko nyingi Sana.
Unafikiri hata akiachia ngazi 2025 ataishi maisha kama ya kwako? Tayari yuko set for life, serikali watamjengea, watamlisha, watamlinda mpaka mwisho wa maisha yake. Na post atapata nyingi tuu huko kwenye jumuiya za kimataifa na hata UN kwa sababu umri wake bado unaruhusu.
 
Anamaanisha umachinga, kuendesha bodaboda/bajaj n.k, ajira zinazowapa watu kula labda na kulipa pango la nyumba...
 
Unafikiri hata akiachia ngazi 2025 ataishi maisha kama ya kwako? Tayari yuko set for life, serikali watamjengea, watamlisha, watamlinda mpaka mwisho wa maisha yake. Na post atapata nyingi tuu huko kwenye jumuiya za kimataifa na hata UN kwa sababu umri wake bado unaruhusu.
Na mtoto wake yule ambae mbunge na yule mkwe wake ambae Ni waziri nao watakuja kujiajiri lini?maana nafasi ziko mtaani nyingi tu Ni uvivu wao tu 😄😄😄
 
Back
Top Bottom