Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
RAIS SAMIA AAWAAPISHA MAWAZIRI, MANAIBU WAZIRI NA KATIBU MKUU KIONGOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu amewaapisha mawaziri nane, na manaibu waziri 8 na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Katanga amechukua nafasi ya Bashiru Ally. Mwaziri walioapishwa ni Ummy Mwalimu, Palamagamba Kabudi, Mwigulu Nchemba, Selemani Jafo, Kitila Mkumbo, Geoffrey Mwambe, Liberata Mulamula na Mohamed Mchengerwa.
Manaibu wazri walioapishwa ni William Ole Nasha, Abdallah Ulega, Mwita Waitara, Pauline Gekul, Hamad Masauni, Mbarouk Nassoro Mbarouk, Mwanaidi Ally Hamis na Hamad Chande.
===
Updates:
- Baada ya viapo vya Mawaziri Viongozi wakuu wa kitaifa walipata wasaa wa kutoa hotuba fupi
MAKAMU WA RAIS AAGIZA WASTANI WA TRILIONI 2 KUKUSANYWA KWA MWEZI
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba kusimamia vizuri mapato
Amemtaka kukusanya maduhuli hadi kufikia wastani wa Tsh. Trilioni 2 kwa mwezi ikifika mwisho wa mwaka. Pia ameelekeza maagizo hayo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu
Amesema ikishindikana anaweza kumuambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa hawawezi kwenda na kasi iliyopo
Dkt. Mpango amesema hayo leo katika hafla ya uapisho wa Mawaziri, Manaibu Waziri na Katibu Mkuu kiongozi, Ikulu Dodoma
HOTUBA YA RAIS SAMIA HASSAN SULUHURais Samia awapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuapishwa na kuwasisitiza kuwa na mshikamano katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuwahudumia Wananchi.
Rais Samia amesema “Serikali ni moja pasitokee kuvutana, nendeni mkawatumikie Wananchi, mkafanye kazi baada ya Bunge la Katiba,kwa sasa mko kwenye Bunge la Katiba aah! hivi nina maradhi gani na Katiba!?, nadhani kwakuwa wameni-push push sana Katiba, Katiba lakini kwa sasa wasahau kidogo”
“Kwa sasa mpo kwenye Bunge la Bajeti, Bajeti tunayoitafuta ni ya Serikali kwahiyo Mawaziri wote lazima muwepo Bungeni, mmoja amekwama na hoja anayeijua anasaidia sio ‘hilo si lake atajijua mwenyewe’, bila Bajeti ya Serikali hatutokuwa na fedha” -Rais Samia
“Nafahamu 2025 ipo karibu na kawaida yetu inapoingia kipindi cha pili cha Rais aliyopo Watu kidogo mnakuwa na lile na hili kuelekea mbele, nataka kuwaambia acheni, twendeni tufanye kazi hili na lile tutajua mbele”
“Nataka kuwaambia rekodi yako inakufuata katika maisha yako, wengine wamekosa hizi nafasi kwa rekodi zao tu, na Mimi nitakuwa na jicho kubwa sana pamoja na kwamba yamelegea lakini yanaona, nitakuwa na jicho kubwa kuangalia rekodi zenu”
“Nitakuwa na jicho kubwa sana kuangalia rekodi zenu na safari ya mbele yetu lakini nataka kuwaambia kila yule mwenye nia ya 2025 aache mara moja”
RAIS SAMIA: AONGELEA KUHUSU MAKUSANYO YA KODI
“Waziri wa Fedha (Mwigulu Nchemba) umepewa kigezo hapa cha Trilioni mbili kwa Mwezi, tunataka Trilioni mbili kwa Mwezi muende mkatanue wigo wa kodi lakini pia mkatengeneze walipa kodi wengi zaidi”
“Mnaua Wafanyabiashara (kwa kutumia nguvu kukusanya kodi) mnapunguza walipa kodi, nendeni mkatengeneze na kutanua wigo wa walipa kodi, yale mengine yanayowapunguzia Watu ari ya kulipa kodi Waziri (Mwigulu Nchemba) naomba ukayasimamie”
“Trend mnayokwenda nayo sasa mnaua Wafanyabiashara, mnatumia nguvu zaidi kuliko akili na Maarifa kupata kodi, sasa wale mnaowakamua mkienda mkachukua vifaa vya kazi, mkafungia akaunti zao na kuchukua pesa kwenye akaunti, akitoka anafunga biashara anahamia Nchi ya Pili”
“Nawatakia Pasaka njema, tunamaliza Pasaka Jumatatu, pengine Jumanne tutakuja kuapishana hapa na wengine, niwatakie kila la kheri na Pasaka njema”
Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu amewaapisha mawaziri nane, na manaibu waziri 8 na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Katanga amechukua nafasi ya Bashiru Ally. Mwaziri walioapishwa ni Ummy Mwalimu, Palamagamba Kabudi, Mwigulu Nchemba, Selemani Jafo, Kitila Mkumbo, Geoffrey Mwambe, Liberata Mulamula na Mohamed Mchengerwa.
Manaibu wazri walioapishwa ni William Ole Nasha, Abdallah Ulega, Mwita Waitara, Pauline Gekul, Hamad Masauni, Mbarouk Nassoro Mbarouk, Mwanaidi Ally Hamis na Hamad Chande.
===
Updates:
- Baada ya viapo vya Mawaziri Viongozi wakuu wa kitaifa walipata wasaa wa kutoa hotuba fupi
HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO
MAKAMU WA RAIS AAGIZA WASTANI WA TRILIONI 2 KUKUSANYWA KWA MWEZI
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba kusimamia vizuri mapato
Amemtaka kukusanya maduhuli hadi kufikia wastani wa Tsh. Trilioni 2 kwa mwezi ikifika mwisho wa mwaka. Pia ameelekeza maagizo hayo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu
Amesema ikishindikana anaweza kumuambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa hawawezi kwenda na kasi iliyopo
Dkt. Mpango amesema hayo leo katika hafla ya uapisho wa Mawaziri, Manaibu Waziri na Katibu Mkuu kiongozi, Ikulu Dodoma
HOTUBA YA RAIS SAMIA HASSAN SULUHU