Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Kenya haina tija kwa uchumi wetu?

Rwanda, Burundi ,Kongo, Zambia hazina tija kwa uchumi wetu?

Kwa hiyo bandari ya Dar haina tija na uchumi wetu?!!![emoji44][emoji44]

"Regional economy" si tija kwa WANANCHI wa kawaida eee?
WaTZ tunapenda kujipa moyo, this country has 60 years of age.
 
Hii comment yako inathibitisha kuwa hizi taasisi za kimataifa mwanzoni zilikuwa zinakataa hilo bwawa lisijengwe kwa sababu Tanzania ilishindwa kuthibitisha kuwa hakuna athari za kimazingira.Kumbe tatizo lilikuwa kwa Tanzania na wala siyo kwa hao mabeberu.
Kusaini mikataba ni kitendo cha uungwana lakini kama kuna upotoshaji, mnayo haki ya kupinga na kutoa elimu sahihi ili Jumuiya ya Kimataifa iiuone ukweli na kutoa uamuzi sahihi.
Lakini kwa miaka mingi Tanzania ilishindwa kutoa elimu sahihi ndiyo maana Bwawa hili likaendelea kuzuiwa kujengwa hadi lilipokubaliwa juzi kama ulivyodai.Hii maana yake ni kwamba mwenye tatizo hapa ni Tanzania na wala siyo hao mabeberu.
 
Wanamkimbizakimbiza ili wapige kiulaini sana
Mkuu agiza chochote hapo ulipo nitumie bili huko PM!

Binadamu kwa sili yetu tangu tuache kuishi mapangoni na kujihami dhidi ya wanayama wakali miaka maelfu iliyopita ila bado maumbile na tabia zetu kwa ndani tunajihami sawa na mababu zetu wa mapangoni...

Nakumbuka nikiwa mdogo shule ya msingi huko kanda ya ziwa kulikuwa na mkaguzi wa shule aliyekuwa anaogopwa sana hadi jina lake nalikumbuka Mama KALIKUMASO, alipokuwa anakuja hadi walimu wanalazwa hospitali....ila wakaguzi wengine walipokuwa wanakuja, inapikwa misosi mitamu, pombe kali au Vimwana wakali(pisi kali wanaitwa siku hizi) kutegemea na jinsi mkaguzi anayekuja wapi ana udhaifu.

Kwa huyu kiranja wetu mkuu nasikia wajanja wameishafahamu udhaifu wake....mapambo na safari, ...nk. Anawekewa hizo chambo wajanja wanakwapua hasa maana hakuna anayefahamu 2025 kutakuchaje! Ubaya wa hawa watu wanaomtega huyu mama ni wale wale wa tangu awamu ya nne, tan! Kwanini tusiwataje hawa watu na jamii ikawafahamu?
URAIS NI TAASISI!
 
Kwanza hawatujui

Sent using Jamii Forums mobile app
Watatujua na kutufahamu tu hivi karibuni kwani Uganda iko tayari kuwapokea kama wakimbizi wale wanawaogopa Taliban huko kwao Afghanistan!
Hapana tatizo halikuwa kwetu bali lilikuwa kwa hizo taasisi za kimataifa kwa kusikiliza propaganda na uongo kutoka kwa akina TOBO na NYEPESI na kuyafanyia uamuzi hayo "matango pori" waliyolishwa. Lakini baada ya kutoa nafasi ya kutusikiliza na kujua ukweli basi mambo yakaenda sawa.
 
Watamfanya kama Kikwete ,wanaobaki ni kujipigia madili tu
 
Hii ziara inaweza kuwa ya kimkakati na ya muhimu pengine kuliko ziara zote zilizofanyika toka mama aingie ikulu. Ni jambo la wazi kuwa katika nchi zote za maziwa makuu, DRC imejaaliwa kuwa na idadi kubwa ya watu takriban watu 120,000,000.
Mbona kuna kipindi mlipandisha kodi pale bandarini mkakimbiwa na hao wakongo! Mambo yenu ya mikodi bila mpangilio na kufanya tathmini, chukua kidogo kwa wengi, kuliko kikubwa na kwa wachache!!?
 
Kitendo cha Serikali kuzidiwa nguvu na hao wazee wa kulisha matango pori tayari nchi ina shida mahali.Kwa nini serikali izidiwe nguvu na wazee wa matango pori?

Hii maana yake ni kwamba serikali iliyokuwa madarakani ilikuwa ni serikali dhaifu.Hiyo serikali ilikuwa ni dhaifu kwa sababu ilipaswa kuwa na ushawishi kwa Taasisi za kimataifa kuliko hao wazee wa matango pori.Hiyo serikali ilipaswa kujiuzulu haraka sana kupisha vyama vingine vyenye ushawishi zaidi kuongoza nchi.
 
Itapendeza kama atafanya ziara Ulaya na Marekani!
 
"Matango pori" ni UONGO ULIOKITHIRI, hivyo kuna wakati mwingine unawaacha waongope hadi utakapo pata muda sahihi na mahali sahihi ili uweze kujieleza na ueleweke kwa wenye akili wenzako. Siyo suala la kupayuka payuka all the time. Vyama gani vyenye ushawishi!?
 

Ni vizuri Congo wana soko kubwa sana. Cha maana ni mpangilio tu
 
Kwahiyo kwako kuonyesha kipaumbele ni ziara ya Rais kwenda nchi husika? Hatuna ubalozi huko Japan? Service gani tuna provide kwa japan kuchochea uchumi wa ndani ukilinganisha Burundi?

Rais Xi Jinping (2013 kama sikosei) alipoteuliwa kuwa Rais wa China kwa mara ya kwanza ziara yake alikwenda Russia jirani yake na mshirika wake then next stop akaja Tanzania kuangalia fursa za wananchi wake kuwekeza humu na namna ya kutupiga na mradi wa Bagamoyo. Ukiangalia ziara za mama kutembelea hizi nchi unazozipinga anaongozana na wafanyabiashara na huwa anawakutanisha wafanyabiashara wa pande zote mbili kujadili changamoto na kuangalia fursa. Japan sisi makapuku tuna nini cha ku-trade nao?Pia soko la regional ni jepesi zaidi kupata faida ya haraka kwa mwananchi kuliko hizo za magharibi na Asia unazozisemea.

Isitoshe huu ndiyo mwaka wake wa kwanza , kama ataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo mbeleni atakwenda tu, sijui kwanini unalazimisha aanze kwa kwenda huko?
 
Wanalindwa na hawa hawa watoza TOZO
 
Kwahiyo kwako kuonyesha kipaumbele ni ziara ya Rais kwenda nchi husika?
Nilichosema mimi mkuu ni kwamba ziara za Rais katika nchi mbalimbali zinapaswa kubase kwenye vipaumbele vyenye tija kwa Taifa.
Hatuna ubalozi huko Japan?
Kwani Rais anapoenda Congo hatuna ubalozi huko?
Service gani tuna provide kwa japan kuchochea uchumi wa ndani ukilinganisha Burundi?
Ohhh my Godness!!!Mkuu nimeitumia japani kama mfano tu wala sijamaanisha kuwa ina tija kuliko Burundi. Angalia andiko langu kuna neno "kwa mfano" kabla ya kuitaja Japan.
Sasa umejuaje kuwa alienda Russia kwa sababu ni jirani yake na wala siyo kwa sababu ni kipaumbele chenye tija kwa nchi yake?
Ukiangalia ziara za mama kutembelea hizi nchi unazozipinga anaongozana na wafanyabiashara na huwa anawakutanisha wafanyabiashara wa pande zote mbili kujadili changamoto na kuangalia fursa.
Mimi msimamo wangu ni uleule hata kama hutaki kuelewa; kuwa Taifa huwa linaongozwa kwa kuzingatia vipaumbele vyenye tija.Je,Congo Burundi na wengineo wana tija kwetu kuliko Mataifa mengine duniani hadi tuwape kipaumbele cha kuanza kuwatembelea?
Japan sisi makapuku tuna nini cha ku-trade nao?
Again,nilitumia japan kama mfano tu kama nilivyosema hapo juu.
Isitoshe huu ndiyo mwaka wake wa kwanza , kama ataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo mbeleni atakwenda tu, sijui kwanini unalazimisha aanze kwa kwenda huko?
Hoja yangu ni nyepesi sana ila ngumu sana kwako kuielewa.Mimi sijalazimisha aanze kwenda popote pale ila hoja yangu ya msingi ni kwamba anapaswa aanze kwenda kule ambapo ni kipaumbele chenye tija kwa Taifa letu kwa sababu Taifa huongozwa kwa kuzingatia vipaumbele.
 
Tulieni makamanda nchi ifunguliwe na ijengwe
 
Kusema nchi kama drc au Zambia zina mchango ndogo katika uchumi wa Tanzania ni kiashiria cha uelewa usio sahihi. Kwa mfano, bandari ya Dsm inahudumia kiasi gani cha mizigo kutoka mataifa hayo. Pia waulize wenye viwanda Dar na maduka Kariakoo juu ya idadi ya wateja kutoka mataifa hayo wanaofanya nao biashara. Natumaini ukipata takwimu sahihi utabadilisha kauli hasi juu ya ziara ya Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…