Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Sio nchi hii mtu anaiba mabilioni ya pesa anakaa miaka yake mitano jela, anapigwa faini ya milioni 8 anaenda kutumia uswahilini.
Hilo sasa ni suala la tabia na ukosefu wa uadilifu wa hao watendaji na suala la viwango vya adhabu kwa mijizi hiyo ni suala la watunga sheria na serikali katika kuwapa adhabu mijizi hiyo. Haya hayana uhusiano na tozo na kodi tunazopaswa kuchangia kwa ajili ya maendeleo yetu.
 
Kupanga ni kuchagua. Rais wetu kaamua kuanzia na majirani zetu na huko unakotaka wewe subiri tu utaona.
Tuna uzoefu na jiwe na ukichukulia alisema yeye na jiwe ni kitu kimoja.
Mienendo yake inafanana na jiwe.
Sitegemei sana kama atakuwa na ujasiri wa kutembelea nchi zenye demokrasia iliyokomaa.Kwa mtazamo wangu ni kuwa anaogopa maswali.
 
Siyo kweli kwamba nchi za Magharibi huwa zinatupa mikopo ya gharama kubwa kwa kuwa tumeshuhudia mara nyingi nchi hizi zikitoa mikopo ya gharama nafuu hata mara nyingine kutusamehe mikopo hiyo.
Kwahiyo hoja yako ni unataka asafiri kwenda nchi za magharibi aua asisafiri amezidi kuzurura?
 
Kwahiyo hoja yako ni unataka asafiri kwenda nchi za magharibi aua asisafiri amezidi kuzurura?
Hoja yangu ni kwamba asafiri kwa kuangalia nchi ambazo ni vipaumbele vyetu kwa maana ya nchi zenye tija zaidi kwetu.Unakumbuka Magufuli aliwahi kusafiri kwenda Zimbabwe?Zimbambwe ilikuwa ni nchi yenye tija kwetu kuliko nchi zote duniani?
 
Kweli tunahitaji kubishana on this kuwa nchi za magharibi huwa zinatupa au hazitupi mikopo migumu na yenye masharti magumu!? Kweli hakuna ajuaye haya na namna walivyotuwekea ngumu juu ya ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere huko Rufiji, eti kwa kigezo cha kuharibu mazingira ya Selous Gama Reserve!? Hakuna ajuaye hili na mengine mengi!? Tusijifanye hamnazo kwa mambo yaliyo wazi!
Suala la Bwawa la Nyerere ni suala la kimazingira zaidi ambalo ni controversial na ambalo pia ni mada nyingine.Hapa tunazungumzia suala la nchi za magharibi kutoa mikopo nafuu na wala siyo ishu ya mazingira ya bwawa la mwalimu Nyerere ambalo ni controversial tokea enzi hizo.
 
Hoja yangu ni kwamba asafiri kwa kuangalia nchi ambazo ni vipaumbele vyetu kwa maana ya nchi zenye tija zaidi kwetu.Unakumbuka Magufuli aliwahi kusafiri kwenda Zimbabwe?Zimbambwe ilikuwa ni nchi yenye tija kwetu kuliko nchi zote duniani?
Mimi ni muumini wa regional intergration zaidi kuliko inter-continental, nawaona hao jamaa zako walioendelea kama ni watu wa kutafuta fursa za kunyonya nchi zinazoendelea tu ( Refer masharti ya bandari ya bagamoyo). Hizi nchi jirani tunafanya biashara yenye kuaminiana zaidi kila pande ikipata maslahi halali kulingana na huduma inayoitoa kwa mwenzake.

Kwenda kuwapigia magoti wazungu na kopo la misaada zama zake naona kama zimeshapitwa na wakati.
 
Wakuu Kazi Iendeleee.

Taarifa zilizopo ni kwamba Rais Samia ana ziara ya kikazi nchini Congo.

Ataanza ziara hiyo wakati atakapotoka Zambia kwenye inauguration ya Hakainde Hichilema.

Akifika Congo atapokekewa na Mwenyeji Wake Rais Felix Tshisekedi.

Hakika Ziara zimeanza na Zimetaradadi
Mkuu jina la Rais wa Zambia liki sahihi kweli?
 
Hii ziara inaweza kuwa ya kimkakati na ya muhimu pengine kuliko ziara zote zilizofanyika toka mama aingie ikulu. Ni jambo la wazi kuwa katika nchi zote za maziwa makuu, DRC imejaaliwa kuwa na idadi kubwa ya watu takriban watu 120,000,000.

Itakumbukwa kuwa Tanzania tumejaaliwa kuwa na bandari, ambapo miongoni mwa nchi zinazotumia bandari yetu ni DRC.

Tanzania imekuwa ujenzi mkubwa wa reli ya mwendokasi ambayo inategemewa kuwa msaada mkubwa wa usafirishaji wa watu na mizigo kuelekea nchi za Rwanda, Burundi na DRC. Kimkakati, kama ujenzi huo utakamilika, Tanzania itakuwa imalamba dume kwa sababu tutaweza kujiinua kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji pamoja na kufaidika na masoko ya bidhaa zetu kupitia wato miliuoni miamoja waliopo mashariki mwa Kongo.

Mnyonge mnyongeni lakini haki haki yake apewe. Ziara ya Rais wetu huko DRC haipaswi kubezwa kwa sababu kiuchumi inalipa tofauti na nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda ambazo zinapitisha mizigo yao katika bandari yetu ya Dar Es Salaam lakini, mizigo yao kidogo kuliko ile DRC kutokana na idadi ya watu katika nchi hizo ni ndogo.

Hongera Mh. Raisi wetu kwa kupanga ziara ya kimkakati ya DRC ambayo ni muhimu sana kwa musakabali wa uchumi wa nchi yetu.
Uganda tupo vizuri mapato ya kupitisha bomba la mafuta muhimu sana. Ziara ya Uganda anyway ilikuwa imepangwa wakati wa Hayati JPM tuombe uzima Covid-19 ipo. Tuendelee kujikinga.
 
Umepotosha uma kwa sababu huwezi kuibuka tu na kusema kuwa Congo au Burundi ina tija kuliko nchi nyingine duniani kwa hiyo inafaa kupewa kipaumbele katika ziara za Rais wakati huna ushahidi unaosupport kauli yako hiyo.

Unapoongea masuala yanayohitaji shahidi za data bila kuwa na shahidi hizo ni upotoshaji.
Wapi nimeandika Kongo ,Burundi ,Rwanda na Kenya kuna tija kwetu kiuchumi kuliko nchi NYINGINE ?!!!

Unaniwekea mdomoni mwangu yanayopita kichwani mwako?!!

Sikuweka hizo STATISTICS za kusupport hoja yangu....haya nazisubiri STATISTICS zako "kinzani"......
 
Wanamkimbizakimbiza ili wapige kiulaini sana
wapigaji wakiwa humu humu safi sana, watajenga humu, kwa kutumia mafundi wahumuhumu,,,, na fundi ujenzi hajapata chake?? mtoto wake akiumwa ataenda kwa Dr fish, na Dr fish ataenda Supermarket, je hela si imerudi nyumbani? kuliko walee wanaendaga kujenga uswiss
 
Tuna uzoefu na jiwe na ukichukulia alisema yeye na jiwe ni kitu kimoja.
Mienendo yake inafanana na jiwe.
Sitegemei sana kama atakuwa na ujasiri wa kutembelea nchi zenye demokrasia iliyokomaa.Kwa mtazamo wangu ni kuwa anaogopa maswali.
Marekebisho kidogo ya Kiswahili, ni hivi sema "hutarajii" siyo "sitegemei"! Sasa kwenye hoja ni kuwa hata kama SSH alisema yeye na JPM ni kitu kimoja, lakini kwenye utendaji kila mmoja ana staili yake. Ndio maana tunaona approach tofauti katika utendaji wao. Kuhusu hayo maswali wewe subiri tu utaona hao "wazungu" watakavyo haha wakati wakijibiwa hivyo viswali vyao. Si ulimwona nani yule - Kikeke alivyojibiwa hadi akakubali mwenyewe na yule bosi wake wa BBC. Au umeshasahau mara hii tu?
 
Suala la Bwawa la Nyerere ni suala la kimazingira zaidi ambalo ni controversial na ambalo pia ni mada nyingine.Hapa tunazungumzia suala la nchi za magharibi kutoa mikopo nafuu na wala siyo ishu ya mazingira ya bwawa la mwalimu Nyerere ambalo ni controversial tokea enzi hizo.
Sawa. Lakini siwalikataa kutukopesha on those slim and flimsy reasons za mazingira! Bwawa linatumia 2% ya eneo lote la hiyo hifadhi wanayo pigia kelele. Ujenzi wa hili Bwawa has never been a controversial issue kwetu, limekuwa hivyo kwao chini ya msingi mkubwa wa kutaka tusijitegemee kwa upande wa nishati nafuu na jadidifu na badala yake tuendelee kutumia mimashine yao ya umeme kama ile ya yule Sighasingha pale Tegeta na akina Symbion! Acheni hizo, TUMEWASITUKIA!
 
Back
Top Bottom