Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Washajua hakuna chochote anachojua.
Washamsoma kuwa huyu hamna kitu, aisee Ila safari hii tumepatikana. CCM watavuna kwa kadri ya watavyoweza.
Hebu fikiria mwenyekiti wa CCM mkoa nae anahudhuria sherehe ya uapisho wa raisi
Hii hata the late mwalimu alikuwa anafanya,fanyeni utafiti kwanza

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Safari ya Oman naisubiri kwa hamu sana ili Nisikie yatakayojiri, Nadhani inaahirishwa tu hadi muda muafaka utakapofika. 😎
 
Ukiona mwanamke aliyeolewa siku za karibuni halafu kutwa nzima anazurura kwenye nyumba za watu basi ujue umepigwa. Huyo atakuwa mmbeya au malaya.
Mkuu unavuka mipaka aisee! Ukiachilia mbali cheo chake lakini kwa umri wake tu anastahili heshima. Sio poa aisee
 
Raisi akiwa hasafiri mnaongea pumba😅 huyu anaesafiri nae mshaanza mashudu kabisa
Umesoma nilichoandika?Wapi nimepinga Rais kusafiri?Hoja yangu ni kwamba Rais anapotoa kipaumbele cha kusafiri kwenda Congo,Burundi sijui Zimbabwe,je hizo ndiyo nchi zenye tija kwa Taifa letu kuliko nchi nyingine duniani?
 
Wakuu Kazi Iendeleee.

Taarifa zilizopo ni kwamba Rais Samia ana ziara ya kikazi nchini Congo.

Ataanza ziara hiyo wakati atakapotoka Zambia kwenye inauguration ya Hakainde Hichilema.

Akifika Congo atapokekewa na Mwenyeji Wake Rais Felix Tshisekedi.

Hakika Ziara zimeanza na Zimetaradadi
Ubadhirifu mtupu. Eti anaenda kujitambulisha kwa majirani. Hiyo ndio tofauti ya washauri wa jpm aliyowatoa na hawa wenzake aliyowaweka. Akili ya upigaji tu. 'Ukipata tumia ukikosa jutia' ndio namna wanavyofikiri.
 
Mizigo mingi ya DRC inapitia mpaka wa Tunduma, inaingia Zambia, Ndola, kisha Lubumbashi, siyo Kigoma. Kuna reli inajengwa kuelekea Tunduma?
Sio kweli hujui kitu tulia wewe, DRC ni kubwa saana. Hiyo mizigo inayopitia tunduma ni inayoelekea Jimbo la kusini la Katanga ambalo makao makuu yake ni Lubumbashi. Nikuulize mizigo inayoelekea majimbo ya Kivu kusini na Kaskazini miji ya Goma na Bukavu inapitia wapi?
 
Umesoma nilichoandika?Wapi nimepinga Rais kusafiri?Hoja yangu ni kwamba Rais anapotoa kipaumbele cha kusafiri kwenda Congo,Burundi sijui Zimbabwe,je hizo ndiyo nchi zenye tija kwa Taifa letu kuliko nchi nyingine duniani?
Zina tija ndio kwani hawalipi hela za huduma mnazowapa?
 
Mie huyu sioni kama kuna rais hapa, anatupotezea muda tu mzanzibar huyu, hana uchungu kabisa na hii nchi. Jambo kubwa la kufanya 2025 ni kuipiga chini CCM. Wapinzani anzeni kuwafikia wananchi sasa hivi ili ikifika 2025 huyu kilaza na genge lake la msoga asirudi kutuongoza. Yaani kawafanya wabongo mbumbumbu anaahidi kila kitu tume, halafu hizo tume hazileti majibu. toka ile tume ya kuchunguza Benki kuu hadi hii ya tozo hamna majibu..muhuni tu huyu hana sifa hata moja ya kua rais wa nchi,.
 
Hivi kweli unakumbuka tulikoanzia?!

Mjadala usio na "argumentum ad hominem" ni ule uendao kwa NIDHAMU...

Ulinipinga kuwa ninaongea "pang'ang'a" kwa kutoweka statistics ya jinsi tunavyonufaika na uhusiano na nchi zinazotuzunguka(anazokwenda mh.Rais)....

Kwa kuwa hatuko mahakamani...nikategemea utakuja na STATISTICS zako...
Hoja yangu ni kwamba mtu hapaswi kutoa taarifa za kupotosha katika jukwaa hili.Kwa kuwa ulitoa taarifa za kupotosha na ambazo hazina evidence unapaswa kwanza kukiri kuwa umekosea na uwaombe msamaha wana jukwaa hili halafu baada ya hapo ndipo mimi nikusaidie kuweka evidences zinazoonyesha ni nchi gani zinapaswa kuwa kipaumbele chetu.
sijaziona bado zaidi ya tabia yako koko ya matusi ,kedi na dhihaka....

Matusi hayauzwi mzeya....
Mimi sijakutukana popote pale labda uniwekee ushahidi hapa kuwa nimekutukana.
 
1.Uganda
2.Kenya
3.Burundi
4.Rwanda
5.Zambia
Ashatembelea nchi tano hadi sasa
 
Safari za nje zinajumuisha za karibu na za mbali....

Mathalani ughaibuni...CHINA kuna mh.balozi Mbelwa Kairuki...anaupiga mwingi sana kiuchumi....amekuwa akiwavuta watanzania kusafirisha KAHAWA NA CHAI YENYE UBORA..

Sasa mh.Rais aanze na ziara nchini China?!!

#KaziIendelee
#SiempreJMT
 
Yule mwingine alikuwa hasafiri watu wakasema anasababisha nchi kuwa na mahusiano mabaya ya nje,sasa huyu mwingine anatoka naye wanasema anatafuna kodi za wananchi,sijajua bado watanzania tunataka raisi wa aina gani...
 
Hebu angalia uteuzi wa waziri wa mambo ya nje ,mh.Liberata Mulamula....uteuzi bora kabisa....

Mh.Mulamula ana uwezo mkubwa na masuala ya DIPLOMASIA...uchumi wa kidiplomasia.....na ndio maana TEUZI ZA MABALOZI zimesimama kwenda KUTUINUA KIUCHUMI HUKO ughaibuni(nchi zilizoendelea)....

Wacha mh.Rais aanze na ziara za hapa karibu.....
 
Back
Top Bottom