Ziara ya nchi za maziwa makuu,Zina manufaa kwa nchi yetu,kibiashara (kuuza mazao yetu-Mahindi au kushawishi nchi hizo kupitishia bidhaa zao bandari ya Dar es Salaam. Serikali kuanzia awamu ya tano, imefanya uwekezaji mkubwa bandari ya Dar na reli ya SGR inayojengwa,ni busara kuanza kuingia mikataba ya kibiashara na nchi zinazo zunguka maziwa makuu watumie huduma zetu sasa na siku za usoni,vinginevyo uwekezaji wote unaweza usiwe na tija(white elephant).
Ninadhani kupitia jamiiforum, tunapoona Rais anatembelea nchi fulani, tunaweza kutoa maoni yetu ya kujenga (constructive idea) nchi yetu, kwa mfano nini Mheshimiwa akatuzungumzie wananchi wake huko ughaibuni (yenye kuleta tija kwa nchi), kwa maana wakati mwingine wasaidizi wake wanakuwa hawayajua matatizo ya huku chini (grassroot level) kwa mfano tumshauri Kama Kuna vikwazo vya biashara kati ya Tanzania na nchi anayokwenda,nk.